Friday, February 8, 2013

MITAALA YA ELIMU TANZANIA IMEBORESHWA SI ZAIDI YA MARA TANO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Paul S. D. Mushi Kifafanua jinsi maboresho ya Mitaala ya Elimu ilivyo yalivyfanyika kwa Maafisa na wadau wa Elimu Mkoani Ruvuma hivi karibuni.


KWA mujibu wa  Kurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Paul S. D. Mushi alisema Maboresho ya pili yalitokea baada ya miaka sita ili kuingiza mapendekezo ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea mwaka 1967 katika mitaala na miaka 12 baadaye.Benki ya Dunia ilipendekeza kuanzishwa kwa Michapuo ya Ufundi,Kilimo na Biashara mwaka 1979 ambapo mitaala hiyo ilianzishwa.

Alisema mwaka 1982, Kamisheni ya Rais ilitoa mapendekezo ya kuboresha Mitaala,baada ya utafiti wanchi nzima chini ya Tume ya Makweta na maboresho ya katekelezwa kati ya miaka ya 1992 na 1997 ambapo baadhi ya masomo  na mada vilipunguzwa na mtaala kuboresha ili kwenda na wakati.

Aidha Dkt Mushi alisisitiza kuwa madiliko makubwa ya Kisekta yalitokea baada ya hapo na  wataalam wengi walishiriki kutoa mapendekezo ya Mpango kabambe wa Elimu mwaka 1999 na Mpango wa Kisekta wa Maendeleo ya Elimu wa mwaka 1999 – 2009.

Alisema kuwa kuzaliwa kwa Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi ( MMEM 2000-2006) ukafuatiwa na Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari  ( MMES 2004 2009 ), ambavyo vilielekeza maboresho ya elimu ya awali ,msingi, sekondari na  ualimu kati ya mwaka 2003 na 2004 hadi mwaka 2007 na 2008.

Alisema Taasisi  ya Elimu Tanzania iliongoza maboresho yote ya mitaala kuanzia ilivyo undwa mwaka 1964  na ilikuwa ilipokea malalamiko ya wadau hasa walimu kutoridhishwa na mchakato wa maboresho hayo .na kwamba walimu hao walihitaji mafunzo kuhusu namna ya kutekeleza mitaala iliyoboreshwa.

Na Taasisi hiyo imeridhia kwa kutoa mafunzo kwa kuwafuata walengwa waliko ili kuipunguzia serikali gharama na ,lengwa watagharimia vitini vya kujifunzia,TET itafika kokote pale walengwa walipo kutoa mafunzo ya maboresho ya  mitaala hiyo.

Sunday, February 3, 2013

MAKUNDI YA NG'MBEA YAMESHAMBULIA MASHAMBA YA MPUNGA KATIKA KIJIJI CHA MABWEHERE WILAYANI KILOSA NA KUSABABISHA HASARA KUBWA KWA WAKULIMA HAO

Kero ya wafugaji kulisha mashamba ya wakulima  hazijaanza leo au jana,bali ni kero ya muda mrefu imekuwa kilio cha samaki mchozi kwenda na maji, Serikali imeshindwa kuwadhibiti wafugaji hao kwa nguvu ya fedha huwenda.
Mkulima Mmoja Bw.Amadi Njole anasema wafugaji hao hulisha kwenye mashamba ya watu,huchoma nyumba za wakulima,huchukua mbegu za wakulima hao,na wakiuliza basi wanashambuliwa kwa fimbo,mishale na sime zao.
Je hali hiyo itaendelea mpaka lini,je serikali imeshindwa kutenga maeneo ya wakulima peke yao na wafugaji peke yao ? Kila miaka ni kero wa wafugaji na wakulima katika wilaya ya kilosa,mali na  uhai wa watu unapotea.
Wote wana umuhimu katika Taifa hili sasa kwanini hali inazidi kuwa mbaya kila mwaka na uongozi wa mkoa ,wilaya na vitongoji upo kwa nini unafumbia macho kero hizo ?

JUMAPILI YA NNE ,YA IBADA INAYOWATAKA WAUMINI WA MADHEHEBU YA ROMAN CATHOLIC KUSIMAMA KATIKA UKWELI.

Baadhi ya waumini wakitoka misa ya kwanza katika kanisa kuu la Jimbo kuu la Songea la Mt.Mathias Mlumba Kalemba leo.
 Bwana Thomas Lipuka kwa kushoto akiwa na mwenzake Foroma  kulia wakiwa nje ya kanisa hilo wakijadili ukweli,wakidai ukweli sikuhizi haupo.Ukweli umeshindikana miongoni mwa binadamu wengi wakiwemo wa madhehebu ya Catholic wenyewe.Kwa sababu ya Utanda wazi uliyoingiwa kwa kasi.
Kanisa la mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba Songea.

JE KUCHUKUA SHERIA MIKONONI KWA KUWACHOMA MOTO WAHALIFU NDIYO DAWA YA KUKOMESHA WIZI ?

Wananchi wamechoshwa na wizi wa vitu mbalimbali, na wakipelekwa polisi au mahakamani baada ya wiki yuko mitaani..kutokana na hali hiyo wananchi wa Jijini Dar es Salaam ,wameamua kuchukua sheria mikononi za kuwaadhibu wahalifu wote ambao wakikamatwa kwa wizi ni kuwa mwagia mafuta ya taa na kuwachoma moto.
Huyo kijana ni mtuhumiwa aliyekamatwa Jijini Dar es Salaam kwa wizi wa pikipiki na kuchomwa moto.Je kitendo cha kuchukua sheria mikononi za kuchoma moto wahalifu ndiyo dawa ya kukomesha wizi na uhalifu?

Friday, February 1, 2013

SERIKALI INAPOFANYA KAZI YA KUWAONDOLEA WANANCHI WAKE KERO YA MIUNDO MBINU NI VYEMA TUIPONGEZE HASA YA BARABARA KWETU KUSINI HEBU SHUHUDIA KWA MACHO YAKO

 Kwa kawaida wanaovaa miwani ya mbao kazi nzuri kama kizi hawaoni.basi hizo ni barabara ka kusini kutoka Tunduru hadi Dar es Salaam ni masaa machache ikilinganishwa na miaka ya nyuma  usafiri ulikuwa wa meli,na ndege.lakini sasa mambo ya usafiri ni poa.
 Mtwara Lindi -Dar es Salaam
 Eneo la mashamba ya chumvi Lindi
 Mingoyo Lindi kwenda Dar es Salaam kwa raha zako.sio siku tatu njiani,sasa ni masaa 9 upo Dar.

PAMOJA NA KILIMO KWANZA LAKINI BEI ZA PEMBEJEO ZIKO JUU HASA MBOLEA

Blog hii leo imepita pita kwa wakulima wa mazao ya mahindi Katika vijiji vya Masigila, na Litapwasi wakihaha jinsi ya kukuza mahindi yao kwa mbolea ambayo bei yake iko juu.
Mkazi mmoja ambaye jina lake hakutaka litajwe alisema Mbole ni shilingi 57,000 kwa mfuko na shilingi 59,000 kwa mfuko.na anasema hekari moja inaingia mfuko mmoja na nusu.akasema mkulima ili aweze kupata mavuno ya kutosha ni lazima awekee mbolea mahindi yake,je kwa bei hiyo kauli mbiu ya Kilimo kwanza itafanikiwa?

TUJIFUNZE KUSINI KWA MARA NYINGINE KUPATA UGENI KUTOKA MISA TANZANIA

 Bwana Andrew Marawiti kushoto akipata maelezo kutoka kwa Bw.Juma Nyumayo Mhariri msaidizi wa Mradi wa Magazeti Vijijini ( Rural Press Project Songea } hatua za awali ya maandalizi ya gazeti la kanda TUJIFUNZE .kuziandika habari ,kuzifanyia Editing ,Lay outing, Scaling,Picture cropping and designing to film kwa Computer.
 Mhariri mkuu wa gazeti hilo Bwana Christian Sikapundwa mwenye tai nyekundu akimwonyesha Bw. Marawiti Gazeti lililo andaliwa Page 1 na 12 ambalo linatoliwa film na kupelekwa kwenye hatua ya Plate ili hatua ya uchapaji ianze.
Hatua ya uchapaji Bw.Marawiti  mwenye kitabu anapata maelezo ya uchapaji wa rangi ( Headline}kutoka kwa fundi mchapaji Bw.Winifredy Kaimbe aliyeshika plate.
Bw. kaimbe aliyeshika plate akimwonyesha plate ya ukurasa wa 12 Master head ya rangi.


ANDREW Marawiti Kutoka  Media Institute of Southern Africa ( MISA ) akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Ruvuma kutembelea vyombo vya habari vilivyoko Songea Mjini na Peramiho ,ametembelea Kituo cha Magazeti Vijijini TUJIFUNZE Kanda ya Kusini Songea, Kuona jinsi wanavyo andaa gazeti lao,kuanzia hatua ya awalihadi kumalizia..
Bwana Marawiti ametembezwa sehemu zote muhimu katika kituo hicho na kupata maelezo na historia fupi ya Magazeti hayo ya kisomo ambayo Serikali iliyaanzisha kwa lengo la kusambaza vijijini kwa wanakisomo hasa watu wasiyo jua  kusoma,kuandika na kuhesabu kkk.
Kwa sasa Magazeti vijijini yanasomwa na wote kwa kuwa yana toa habari zenye viwango kama habari zinazoandikwa kwenye magazeti mengine yanayo tolewa kila siku kwa watu wa mjini peke yao.na vijijini hayawafikii walengwa wetu.
Gazeti hili linasambazwa Kanda ya Kusini katika mikoa ya Ruvuma,Mtwara na Lindi katika wilaya 19,kutokana ufinyu wa bajeti yetu tunachapisha nakala chache chache tunazo zisambaza kwa walengwa wote.Aidha kituo hakina waandishi wa habari wa kutosha na ufinyu wa bajeti inabidi kuwatumia waandishi wa habari wengine kukusanya habari.
Bw.Marawiti ametembelea Rural Press Project Songea TUJIFUNZE, Radio Jogo FM, Radio Maria na Peramoho Publishing House kunachapwa Gazeti la Mwenge na kuongea na baadhi ya waandishi wa habari.