Friday, December 21, 2012

TUJIFUNZE BLOG IMETOKANA NA JINA LA GAZETI LA KUSINI LA TUJIFUNZE TOLEO Na.6 LA OKTOBA - DASEMBA 2012

 Hilo ni toleo Na.6 la Oktoba - Desmba 2012 la TUJIFUNZE,Ambapo lead ni Kilio cha wakulima wa korosho nchini  kilio chao kimesikika - asema katibu Mkuu wa CCM Mhe.Abdulrahamn Kinana Mtwara.
Wakati  sub lead Dr.Huvisa atoa msaada wa vifaa tiba kwa hospitali za mkoa na wilaya, Mkoani Ruvuma.Front page.
Upande wa Mafunzo maalumu ,Makumbusho ya Majimaji ni kivutio kwa watalii,Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Bi.Maimuna Tarishi.Ambapo upande wa michezo Timu ya majimaji wafunguka kwa maandalizi ya kurejea Vodacom msimu ujao.

UPANUZI WA BARABARA JIJINI DAR ES SALAAM WAENDA SAMBAMBA NA UJENZI WA DARAJA LA JUU KIMALA KAMA LILE LA MANZESE

 Hilo ni daraja la juu  la Kimara Jijini Dar es Salaam kama lilivyo la Manzese,ikiwa ni upanuzi wa Barabara za Jijini Dar es Salaam ili kupunguza msongamano wa magari jijini humo.Ni juhudi za serikali za kuboresha miundombinu ya barabara zake nchini.
Ni nguzo za daraja hilo ambazo bado kuweka daraja hilo.

Merry Christmas and new year of 2013 for all Blogger readers

 Happy with Merry Xmas cards and coming of new year of 2013 together.



WASICHANA WA FANYA MAAJABU KATIKA MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2012 KWA ASILIMIA 8.8 KWA KUWAPIKU WAVULANA




WAZIRI wa  Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Dkt Shukuru Kawambwa  ametangaza matokeo ya darasa la saba mwaka 2012 ofisni kwake kwa waandishi wa habari na kusema wasichana wamefanya vizuri kuliko wavulana kwa asilimia 8.8,baada ya kuongoza kwa asilimia 50.20 kwa kuwapita wavulana kwa asilimia 49.80.
   Waziri huyo alisema kuwa wanafunzi 560,706 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za serikali,na kati yao wanafunzi 281,460 ni wasichana na 279,246 wavulana ambapo imefanya idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kuongezeka kwa asilimia 8.8, ikilinganishwa na wanafunzi 515,187 ya waliyochaguliwa mwaka uliyopita.
  Mhe. Kawambwa alisema mtihani wa mwaka huu umefanyika kwa mara ya kwanza kwa kutumia Teknolojia mpya ya ‘ optical mark reader’ ambao usahihishaji wake hutumia compyuta,njia ambayo imeipunguzia serikali gharama ikilinganishwa na mwaka jana.
   Alisema kuwa mwaka jana walimu 4,000 walitumika kusahihisha zaidi ya mwezi mmoja,ambapo mwaka huu 285 ndiyo walitumika kwa siku 15 kukamilisha kazi yote.
     Kuhusu matokeo hayo amesema kuwa alama ya juu kabisa ni 234 kati ya 250 kwa wavulana na wasichana, ambapo wanafunzi 3,087 wamepata alama daraja la ‘A’ na wanafunzi 40,683 alama daraja la ‘B’,wanafunzi 222,103 alama daraja la ‘C’ na wanafunzi 526,397 alama daraja ‘D’ ambapo waliobakia 73,264 alama daraja ‘E’
   Aidha alisema vitendo vya udaganyifu vimepungua kutoka wanafunzi 9,736 waliofutiwa matokeo yao mwaka jana ikilinganishwa na wanafunzi 293 waliofutiwa matokeo yao mwaka huu.

Monday, December 17, 2012

WAKUU WA VITUO VYA KANDA SABA ZA MAGAZETI YA KISOMO WAMETAKIWA KUSIMAMA NA KUJENGA USHIRIKIANO KATIKA UTENDAJI KAZI ZAO

 Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi Bwana Salumu Mnjagila akiwasomea vipengere vya fomu za PRAS   Wahariri wa Magazeti vijijini wa Kanda saba katika ofisi yake  Mkao Makuu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya washiriki katika kikao hicho cha kazi wakimsikiliza Mkurugenzi kwa makini
 Naibu Mkurugenzi Kisomo Mwanza Bibi Mary Joseph Salu
 Picha ya Pamoja ya viongozi wa Idara ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi na  Baadhi ya wahariri wa magazeti vjijini
 Mkurugenzi Msaidizi Utawala Bw.Gange akitoa mada ya OPRAS kwa Wahariri wa Vituo vya uchapaji




WAKUU  wa vituo wa Kanda  saba  za magazeti ya kisomo  nchini,wametakiwa kusimama kwa ushirikiano na mshikamano wao katika ufanisi wa kazi zao za kuelimisha wananchi kupitia magazeti yao ya kisomo yanayo chapwa katika Kanda zao.
     Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi EWW/ENMRA Bwana salumu Mnjagila alisema hayo wakati wa kikao cha kazi kilicho fanyika ofisni kwake leo Makao makuu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi JIjini Dar es Salaam.
     Bw.Mnjagila alisema kila mmoja atambue nafasi yake kituoni ili kuleta ufanisi wa kazi bila ya kusababisha migongano baina ya viongozi na watumishi katika vituo hivyo.
Aidha alisema vituo hivyo vitafanya kazi za maendeleo ya kuboresha  elimu nchini iwapo watafanya kazi kwa kuelewana  na kuwa wawazi katika maamuzi ya utekelezaji wa majukumu waliyo jipangia.
     Kikao hicho kilijumuishi Msaidizi Utawala Bwana Gange na Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji wa Taaluma Bibi Revilla na Wahariri  wa Vituo vya Uchapaji Magazeti Vijijini vya Mwanza,Tabora,Mbeya na Songea, ambao pia ni wakuu wa vituo hivyo.


Sunday, December 2, 2012

WAZAZI WATAKIWA KUWAPELEKA WATOTO WAO WADOGO SHULE ZA AWALI


Meya wa Manispaa ya Songea  Mstaiki Charles Mhagama amewataka wananchi na wazazi wa Manispaa yake kuwapeleka watoto wao wadogo kwenye shule za Awali ,ili wajengeke na msingi mzuri wa kujifunza.
Meya Mhagama alisema hayo katika mahafari ya shule ya Awali Charity iliyoko katika Uwanja wa sabasaba Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma jana,na kwamba katika harambee iliyofanyika katika mahafali hayo,Mstahiki Meya Mhagama aliahidi kutoa malori mawili ya mchanga yenye thamani ya shilingi laki tatu ( 300,000/= ),ambapo Yusufu Kufakunoga,kwa niaba ya Mhariri kanda ya kusini aliahidi kuchangia mifuko mitatu ( 3 ) ya sementi,Mtangazaji wa Star TV Songea Bwana Adam Nindi aliahidi kuchangia Shilingi 20,000/=.
Watoto 13 wamehitimu mafunzo ya Awali,ambapo mwakani watoto hao wataingia darasa la kwanza.Katika picha,wakwanza mwenye suti ya bluu ni mwalimu mkuu,pia ni mkurugenzi wa shule hiyo anayemfuatia mwenye kaunda suti mikono mifupi na Mstahiki Meya Charles Mhagama akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu.