Sunday, November 18, 2012

BREAKING NEWS !! ( USAJILI WA WAPIGA KURA NCHINI KENYA UNAANZA KESHO.

USAJILI wa wapiga kura nchini Kenya unaanza kesho tarehe 19 /11/2012 hadi  tarehe 18 /12/2012 kwa wananchi wenye umri wa miaka 18 katika vituo 25 ambapo vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 11 jioni ( chanzo cha habari ni Mchapuko wa Habari K 24 )

Friday, November 16, 2012

WATUMISHI WATATU WA KITUO CHA MAGAZETI VIJIJINI KANDA YA KUSINI SONGEA WAAGWA LEO KATIKA HOTELI YA NIPASHE MJINI SONGEA RUVUMA



 Hiyo ndiyo meza kuu waliyo kaa wastaafu na wenzi wao wa katika mwenye tai na mkewe nia Bw.Siprian Tawete mstaafu mwaka 206,anayefuata kulia kwake mwenye kitambaa cheupe Bibi Feblonia Banda aliyestaafu mwaka 2010 na Mmewe Mr.Banda na wa tatu ni kwenye suti nyeusi amezibwa na ua Bw.Joramu Mwaipopo kushoto kwake ni Mkewe Mrs Mwaipopo.
 Bwana na Bibi Tawete
 Bibi na Bwana Banda
 Bwana na Bibi Mwaipopo
 Mfanya kazi aliyebakia kituoni Bw.John Mponda mlinzi na Mkewe.
 Bwana Charles Lukoto Mpiga chapa
 Wageni waalikwa wa kwanza Mke wa Mhariri msaidizi Bw. Juma Nyumayo ( Mrs Nyumayo)
 Mke wa aliyekuwa Mkuu wa kituo hicho (Marehemu Enos Mwabina) Mrs Mwabina

 Mrs Nyumayo
 Mhariri wa kituo hicho Bw.Christian Sikapundwa
Baadhi ya wasaidizi wa kituo katika kuelemewa na kazi Bw. Yusufu Kufakunoga chumba cha giza ( dark room ).


Kituo cha uchapaji Magazeti Vijijini ,Kanda ya Kusini leo kimewaaga wafanya kazi watatu waliyostaafu kwa miaka tofauti.

KITUO cha magazeti vijijini Kanda ya Kusini Songea ,kimewaaga wafayakazi watatu waliyostaafu kwa mujibu wa utumishi baada ya kufikisha miaka 60 wa umri kwa kuwafanyia tafrija fupi katika Hoteli ya Nipashe maeneo ya Mabatini katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Watumishi waliyo staafu kulingana na kupishana kwao ni pamoja na Bwana Siprian Tawete aliyekuwa Mlinzi mwaka 2005,Feblonia Banda Mtunza ofisi mwaka 2010 na watau ni Bwana Joramu Mwaipopo mlinzi aliyestaafu mwezi Juni 2012.

Tafrija hiyo imejumuisha wataafu na wenzi wao ,ambao wote wemepatiwa zawadi wao na wenzi wao,kama motisha katika utumishi wao walipokuwa kituoni hapo.

Kituo kimewatakia maisha mapya ya kujitegemea baada ya ukomo wa utumishi wao kituoni,na kwamba wao pia wamewatakia wafanya kazi waliyokuwemo katika ajira amani na mshikamano kazini.

Baada ya kustaafu watumishi hao Kituo kimebakiwa na watumishi sita tu kitu ambacho kitafanya kituo kizidiwe na majukumu katika utndaji kazi wao.

Monday, November 12, 2012

HISTORIA YA KILWA KISIWANI IMEIWAKA KISIWA HICHO KATIKA HISTIRIA YA URITHI WA DUNIA AMBAPO WATALII WANAKWENDA KUJIONEA MAAJABU YA MAJENGO YA MISIKITI INATUPASA NA SISI KWENDA KUONA MAAJABU HAYO

 Mnara wa Kilwa kivinje katika mji wa Kilwa kivinje mji ambao wenye historia ya waarabu na ustaarabu wa kiarabu wenye utawala wa Kisultani.
 Hilo ni jengo ambalo lipo pwani ya Halmashauri ya Lindi ambalo lilijengwa enzi ya utawala wa Kisultani
 Mwandishi wa habari na Mhariri Msaidizi wa Magazeti Vijijini Kanda ya Kusini Bw.Juma Nyumayo akisoma kibao kinacho elezea urithi wa Dunia kilichowekwa na UNESCO.kilicho katika kivuko cha kuvushia wakazi wa Kilwa kisiwani  Katika Mji wa Kilwa Masoko.
Asubuhi Bw.Juma Nyumayo akiwa katika mji wa Kilwa Masoko baada ya kumaliza kazi ,akionekana akielekea Lindi Mjini kuelendelea na kazi.

Tuesday, November 6, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI – MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA RUVUMA. • Yafanya Maadhimisho ya sita ( 6 ) ya siku,wiki ya Mlipa kodi tarehe 7/11/2013 Mkoani Ruvuma ( Kauli Mbiu ni “ ULIPAJI KODI WA HIARI KWA TAIFA LENYE MAFANIKIO.”) • Mlipa kodi anao mchango kubwa katika mafanikio ya TRA.

 Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma Bwana Apili Mbaruku akitoa taarifa ya Mamlaka ya TRA Mkoa wa Ruvuma leo kwenye ofisi yake kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusu maadhimisho ya siku ya mlipa kodi yatakayo fanyika kesho.katika Manispaa ya Songea.
 Afisa Elimu kwa Mlipa kodi Bw.Mefti Jackson wa Mamlaka ya TRA Mkoa wa Ruvuma ,ambapo kwa ushirikiano na Timu nzima ya Mamlaka ya TRA mkoani humo ,wameweza kuwapatia leseni za udereva waendesha yeboyebo na madereva wa magali.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma Bw.Apili Mbaruku,ofisini kwake
Watumishi wa TRA .
 Waandishi wa TBC na Channel Ten
Bwana.Juma Nyumayo wa kwanza mwenye kitabu akielezea jins Mamlaka hiyo ilivyo fanikiwa katika utoaji wa leseni kwa Yebo yebo.


MAMLAKA ya mapato Tanzania inatambua na kuwapongeza walipa kodi wote kwa mchango wao mkubwa katika mapato ya Serikali kwa mafanikio ya Taifa,ambapo lengo la Mamlaka ni kuimarisha utendaji wa kazi katika kuongeza makusanyo ya kodi na kuboresha huduma kwa walipa kodi wote.

MENEJA wa TRA Mkoa wa Ruvuma Bwana Apili Mbaruku, akisema hayo wakati akiongea na  waandishi wa vyombo mbalimbali wa Mkoa wa Ruvuma ofisini kwake leo,na kwamba katika maadhimisho hayo kutatolewa mafunzo ya kodi kwa walipa kodi kwa mtindo wa kuuliza maswali na majibu kwa wadau wao.

Mamlaka ya TRA inategemea kutoa msaada wa magodoro 12   kwenye Ward ya watoto katika Hospitali ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma yenye thamani ya shilingi laki nane ( sh.800,000/= ).

Aidha Bw. Mbaruku alisema kuwa Mamlaka ya TRA Mkoani Ruvuma, katika mwaka wa fedha wa 2011/2012,ilikusanya kodi kwa kiwango cha asilimia 109.5 % kwa kodi za ndani na asilimia 96 % kwa kodi ya Forodha.

Kuhusu kodi za ndani ililenga kukusanya shilingi bilioni 5.001/=,badala yake ikavuka malengo kwa kusanya shilingi bilioni 5.476/=,ambapo kodi ya Forodha ilifikia malengo kwa kukusanya shilingi bilioni 223.8/= kama ilivyolengwa kukusanya na kwamba makusanyo halisi yalikuwa zaidi kwa asilimia 31 % ya makusanyo halisi ya mwaka wa fedha wa 2010/2011.

Alisema kuwa katika kuboresha wa ukusanyaji kodi kwa njia ya vitalu,Mamlaka ya TRA mkoani Ruvuma imeweza kuandikisha walipa kodi zaidi ya 1,094 kwa mwaka wa 2011/2012 ,ni pamoja na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa tatu ulioanza mwaka 2008/2009 na kuendelea mwaka 2012/2013.

Kama mpango huo ulivyoanishwa,mkoa wa Ruvuma umewekewa mtandao wa leseni za udereva uliyowezesha makusanyio ya shilingi milioni 424.2/= na leseni zaidi ya 8,500 zilizotolewa mpya au kubadilishwa.

Friday, November 2, 2012

MVUA ZILIZOANZA KUNYESHA KATIKA MANISPAA YA SONGEA KUANZIA JANA ZIMEKUWA MKOMBOZI KWA WAKAZI WA MANISPAA HIYO WALIYOKUWA WAKIHAHA KUTAFUTA MAJI YA KUNYWA NA KUPIKIA KUTOKANA NA UHABA ULIYOJITOKEZA KWA MUDA MREFU

 Leo mji wa Songea ulipata neema ya mvua ,ikiashiria kuwa tatizo la maji katibu litatuliwa.
Wakati mvua ikinyesha watu wenye vyombo vya usafiri walikuwa kwenye vyombo vyao vya usafili wkienda kununu mafuta ili wendelee na shughuli zao za kilasiku.

HUDUMA YA MAFUTA AINA YA PETROLI NA DIZELI KATIKA MANISPAA YA SONGEA BADO INAENDELEA KUWA MBAYA ZAIDI KAMA UTAKAVYOONA FOLENI YA MAGARI NA PIKIPIKI KUELEKEA KWENYE KITUO CHA KISUMA PAI FILLING STATION

LEO katika Manispaa ya Songea pamoja na kuwa na foleni kubwa/ndefu ya magari na pikipiki kuelekea kwenye kituo cha Kisumapai Filling Station kupata huduma ya mafuta,lakini pia kulikuwa na mvua,lakini watu hawakujali hiyo mvua ili mradi wapate huduma hiyo.

 Hiyo ni foleni ya magari kuelekea kwa Kisuma Pai Filling Station,kituo peke yake katika Manispaa ya Songea ndiyo kinatoa huduma hiyo adimu kwa wenye vyombo vya usafiri.
 Hiyo nayo ni foleni ya pikipiki ambayo imeanzia mbali ikiwa ni foleni ya pikipiki na magari kuelekea Kisuma Pai filling Station kupata petroli na dizeli Leo katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Manispaa ya Songea ina vituovingi vinavyouza mafuta lakini ni kimoja tu ndicho kinacho uza mafuta,cha Kisuma pai Filling Station,kwa hivyo foleni ya magari na pikipiki zinakuwa ndefu kwenye kituo hicho cha kuuzia mafuta mjini hapa.

PIKIPIKI NA MAGARI YAWEKA FOLENI YA MAFUTA YA PETROL ,KITUONI KUNA DISELI KISUMAPAI JANA MANISPAA YA SONGEA

 Ni kituo cha kuuza mafuta KISUMAPAI FILLING STATION katika manispaa ya Songea jana kilikua kikiuza mafuta ya Dizeli.lakini foleni kubwa kama ya magali na pikipiki ilikuwa ilisubili huduma ya petroli hapo jana bila kuelewa kuwa petroli wanayo hitaji haikuwepo.
 Hiyo ni foleni iliyoanzia jengo la Chuo kikuu cha SAUT mjini Songe ikielekea kwenye Filling Station ya Kisuma pai ili wapate walau lita moja ya petroli hapo jana.
Shida ya huduma ya mafuta ya petroli na Dizeli katika Manipaa ya Songea,imefanya wenye pikipiki walanguliwe lita moja kwa sh.3,000/= hadi sh.7,000./= ni kituo kimoja tu ndiyo kilikuwa kikiuza Dizeli.