Saturday, July 14, 2012

WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA MAKARANI WA SENSA SIKU YA TAREHE 25 /8/2012 SIKU YA KUHESABIWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda alisema kuwa siku ya tarehe 25 mwezi wa nane mwaka huu makarani wa sensa watapita katika kaya za watu kuhesabu,kuelewa siku ya kuamkia tarehe 25 ni watu wangapi wamelala katika nyumba ile.
Aidha Mhe.Pinda alisema kuwa wananchi wajitokeze kutoa maoni yao kuhusu Katiba mpya siku Tume ya Katiba ikifika katika maeneo yao.
Mhe.Pinda alisema hayo siku akizindua mradi wa matrekta katika uwanja wa Zimani moto katika Manispaa ya Songea hivi karibuni,siku ya pili ya ziara yake ya siku mbili ya kikazi Mkoani Ruvuma.

Sunday, July 8, 2012

CHUO KIKUU CHA SAUT SONGEA KUANZISHA EVINING CLASS KUANZIA MWEZI WA 9 MWAKA HUU

               CHUO KIKUU CHA SAUT SONGEA KUONGEZA VITIVO

MSHAURI wa wanachuo ( Dean of Student ) Michael Sinienga alisema hayo hivi karibuni kwa waandhishi wa habari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Kanda ya Kusini walipotembelea chuo hicho kwa lengo la kupata taarifa za mafanikio na changamoto kadhaa tangu chuo hicho kianze kudahili wanachuo wake.
     Bwana Sinienga alitaja vitivo vitakavyo ongezeka kuwa ni pamoja na ‘Business Administration, Law, Medicine, Mass Communication  and Education’ ambayo ndiyo iliyoanza.
   Matarajio mengine ya chuo hicho ni kutoa kozi fupifupi za ujasiliamali, kozi za jioni ‘Evening classes’  kwa watumishi na watu wengine wenye kutaka kusomea shahada wakiwa kazini.
    Matarajio mengine ni kutoa huduma kwa shule za sekondari ambazo zitakuwa na uhaba walimu na zikipenda kupata huduma hiyo kutoka katika Chuo Kikuu hicho, Pia kuwaandaa vijana kujiamini na kujitambua na maadili kuwekewa kipaumbele.






Ziara ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ya siku mbili mkoani Ruvuma





Serikali kuitoa asilimia 70 ya wakulima wa Tanzania wanaotumia jembe la mkono kwenda kwenye kilimo cha kisasa cha matrekta.

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda watatu kutoka kulia akipungia wananchi mkono  wa kwaheri jana katika uwanja wa zimanimoto Katika Manispaa ya Songea baada ya kuzindua matrekta 53 yaliyokopeshwa kwa wakulima wa Mkoa wa Ruvuma.
 Baadhi ya Matrekta yaliyo kabidhiwa jana kwa wakulima wa wilaya za Songea Manispaa,Songea Vijijini,Namtumbo ,Mbinga na Tunduru ambako wengi waliyachukua mayterkta hayo
 Mhe.Pinda akizindua trekta lililo kopwa na Mkuu wa Koa wa Ruvuma Mhe,Said Thabit Mwambungu.
 Waziri Mkuu akisalimiana na viongozi na baadhi ya wananchi waliofika kumpokea uwanjani katika uwanja wa ndege Songea Juzi alipoa anza ziar yake ya siku mbili mkoani Ruvuma juzi.
Mhe.Mizengo Pinda.


Ili kuitoa asilimia 70 ya Wa- Tanzania wanaotumia jembe la mkono kwa kilimo,
Serikali imeweka mkakati wa kuhamasisha wakulima kutumia matrekta katika kilimo chao badala jembe la mkono.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda alisema hayo jana katika uwanja wa Zimani moto katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ,wakati wa kuzindua mradi wa matrekata 53 ambayo yamekopeshwa kwa wananchi na wakulima kwa lengo la kumtoa mkulima kutoka matumizi ya jembe la mkono.
Alisema serikali imeagiza zaidi ya  amatrekta 1,600 kutoka nchini India kwa mkopo ambayo yapelekwa mikoani kwa mpango wa kuyakopesha wananchi kwa bei nafuu ambayo yatalipwa ndani ya miaka mnne.
   Aidha alisema kuwa uwezo wa trekta ni kulima heka 25 hivyo mmliki wa trekta anaweza akakodisha kwa wakulima wengine nao wakaachana na jembe la mkono.
  Alisema Halmashauri na vyama vya Ushirika wachukue matrekta hayo ili wawezi kukopesha wananchi wanye kutaka kutumia trekta katika kilimo.
         Pamoja na mambo mengine Waziri Mkuu waliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi wakati Tume ya Katiba inapofika katika mikoa yao ambapo Tume hiyo imeanza katika mikoa 8 isitosha alihimiza kwa wananchi usiku wa kumkia tarehe 25  mwezi wa 8 mwaka huu, kila mwananchi atahesabiwa ni siku ya Sensa Kitaifa ameomba wannanchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa sensa wanapopita katika kaya zao siku hiyo.

Saturday, July 7, 2012

MIZENGO PINDA ATUA SONGEA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI KUANZIA JANA HADI LEO

Ashuka kenye ndege jana katika uwanja wa ndege wa Songea ,Nakisha akasalimiana  na viongozi na kuvishwa Skafu na mwanafunzi Mercy Ngatunga wa Sekondari ya Matarawe.Baadaye akaelekea Ikuli kusomewa taarifa ya maendeleo ya Mkoa na Taarifa ya Chama Tawala ( CCM )



WAZIRI MKUU MHE,MIZENGO PINDA AZINDUA NA KUGAWA MATREKTA 33 KATI YA 53 YANAYOKOPESHWA KWA WAKULIMA WA MKOA WA RUVUMA,KUONDOKANA NA JEMBE LA MKONO

 Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda leo amezindua mradi wa matrekta 53 na kati ya hayo 33 yameshapata wanunuzi ambao wamekabidhiwa fungu na Mhe Waziri Mkuu katika viwanja vya Zimani Moto Songea leo.
Baada ya kukata utepe Waziri Mkuu alijaribu kuliwasha trekta lililokopwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Said Thabit Mwambungu.
Aidha alisema matrekta hayo lazima yapelekwe shambani,si vinginevyo,na kwamba amewataka Halmashauri zote nchini kupunguza utitiri wa vikwazo vya mazo katika barabara.
Waziri Mkuu alikuwa akiwaonyesha watu namna trekta linavyo weza kuwa msaada na ukombozi mkubwa kwa mkulima.

Thursday, July 5, 2012

CHUO KIKUU SAUT TAWI LA SONGEA KUONGEZA KUWA NA VITIVO VITANO KUANZIA SEPTEMBA 2012

Profesa Donatus Albert Komba akiwa Ofisini kwake katika Chuo Kikuu cha SAUT Tawi la chuo Kikuu cha SAUT Mwanza Mjini Songea.kk






\[CHUO KIKUU TAWI LA SAUT CHA SONKUANZIA SEPTEMBER 2012
MKURUGENZI  wa chuo hicho Profesa Donatus Albert Komba alisema hayo ofisini kwake leo kwa waandishi wa habari waliyotembelea chuoni hapo katika Manispaa ya Songea, kuona na kupata maelezo ya mafanikio ya chuo hicho ambacho ni tawi la chuo kikuu cha SAUT cha Jijini Mwanza.
Profesa Komba alisema kuwa chuo kinatarajia kuwa na vitivo sita kuanzia mwezi September mwaka huu,alivitaja vitivo hivyo kuwa ni pamoja na ‘Education, Law, Business Administration,Sociology, Mass Communication, and Medicine’.
Alisema kuanzia mwezi Septemba 2012 chuo kitapokea wanafunzi wanafunzi wengi ikilinganishwa na sasa wachache ambao ni 176 kati yao wavulana108 na wasichana78.na walimu 13 na wafanyakazi ambao si walimu 17.
Kuhusu ada inayolipwa katika chuo hicho ni Tshs.2,600,000 kwa wanafunzi wa Kitivo cha Medicine ambapo Bodi ya mikopo huwakopesha kiwango chote hicho kutokana na umuhimu wao.
Aidha kwa vitivo vingine ada ni Tshs.950,000 kwa mwaka ambayo hulipwa kwa awamu mbili.ambapo Bodi ya mikopo huwakopesha Tshs.475,000/= kiasi kinacho salia hulipa wenyewe.
Alisema kuwa wanfunzi 50 wa kitivo cha Medicine kitaanzia Songea wakati miundombinu ya chuo kikuu cha tiba ikikamilishwa Peramiho,ikikamilika watakwenda kuendelea na masomo yao kwa mika mitano huko Peramiho.
Hilo ni jengo la Utawala la chuo kikuu cha SAUT Songea

.