Thursday, June 28, 2012

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ASIKITISHWA KITENDO CHA KINYAMA KILICHO FANYWA NA WATU WALIYEMSHAMBULIA DAKTARI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ameliambia Bunge wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa waheshimiwa wabunge leo ,kuwa serikali imesikitishwa na kitendo cha watu waliyehusika katika kumshambulia Daktari hadi kumsababishia maumivu katika mwili wake.
Amesema anamuombea Mungu  ili aendelee vizuri na kwamba uchunguzi unaendelea wa kupata watu waliyehusika na tukio hilo.
Kuhusu mgomo wa madaktari Pinda amesema kuwa serikali iko katika harakati za kutafuta waganga kutoka katika taasisi mbalimbali ili kuokoa maisha ya wagonjwa walioko katika hospitali ambazo madaktari wake wako katika mgomo mkiwemo Madaktari maaskari pamoja na wale waliostaafu ,wakati serikali ikifanya taratibu za suluhu kufuatia mgomo wa madaktari.

Wednesday, June 27, 2012

MADAKTARI WAMRUDIE MUNGU WAO WAACHE MGOMO MAANA WANAO ATHIRIKA NA WANANCHI WASIO NA HATIA WALA UWEZO WA KUWATIMIZIA MADAI YAO.

Wakati Daktari Jijini Dar es Salaam yuko ICU kwa kupigwa na watu wasiyejulikana, Madaktari wa hospitali ya Mkoa Songea nao wako katika mgomo baridi wagonjwa wamefurika  hosipitalini hapo bila msaada.
   Lakini hawa walikula kiapo kuwa watalitumikia taifa kwa uwezo wao wote, ambao wamechukua dhamana ya maisha ya wananchi wa nchi hii, Lakini wamesahau kuwa walikula kiapo cha utii kwa taifa.
  Pia Serikali nayo ifikie mahali iwatekelezee madaktari hao na watumishi wengine wa kada mbalimbali wanao dai maslahi yao ili kuepusha dhahama zinazotokea kwenye migomo, halafu haipendezi ni aibu kwa nchi yenye serikali sikivu  ifike mahali serikali isema sasa migomo basi,  na inawezekana.

Tuesday, June 26, 2012

OPERESHENI ya polisi Ruvuma yashika silaha 17,Risasi,madwa ya kulevya na pombe haramu.

RPC Ruvuma kamishina Msaidizi Deusdedit Nsimeki akiwaeleza waandishi wa habari mafanikio ya Operesheni iliyoendeshwa na Polisi ambayo silaha 17 zimekamatwa,risasi,pombe haramu madawa ya kulevya pamoja na wizi na unyang'anyi wa kutumia silaha na wizi.
 Kamanda akijibu hoja na mwaswali kutoka kwa waandishi.
Baadhi ya waandishi wakitafakali jinsi Operesheni kamata silaha ilivyofanikiwa.
Kamanda,Gerson Msigwa TBC katikati na Mosesi Konara kulia wakisikiliza maoni na usahuri kutoka kwa waandishi hao leo.


KAMANDA wa Polisi Mkoa Ruvuma Kamishina Msaidizi Deusdedit Nsimeki ameaambia waandishi wa habari katika ukumbi wa Polisi mkoa leo kuwa,silaha 17  zimekamatwa zikiwemo short gun  3,na  Rifle 3 magobole 11, pamoja na risasi na kesi 7 za watuhumiwa ziko mahakamani.
  Aidha Kamanda Nsimeki alisema katika Operesheni hiyo,kesi 10 zilizohusisha bangi ziko mahakamani ,pamoja na kesi za pombe haramu ya gongo lita 60.5 zilizokamatwa zilizowahusisha watuhumiwa wauzaji na wanywaji wa pombe hiyo.
    Nyingine na unyang’anyi wa kutumia nguvu kesi moja na unyang’anyi wa kutumia silaha watuhumiwa 12, kati yao 6 wapo mahakamani ,pamoja na wizi wa diseli,nondo 147  za kutengenezea madaraja, zilizosadikiwa kuibwa kwenye kampuni ujenzi wa barabara, Pia wizi wa mbuzi 7 na kesi yake ipo mahakamani ikiwa ni pamoja na uzururaji mitaani bila kazi maalumu
    Kamanda Nsimeki ametoa wito kwa wananchi wa mipakani kuacha kutumia silaha wanazozimiliki kisheria  kuazimisha kwa watu ambao hawajui matumizi yake kama ni ya uahalifu au la.Alisema zoezi la kusaka silaha zinazotumiwa kinyume cha sheria linaendelea ikiwa ni zoezi endelevu.

Thursday, June 21, 2012

Serikali mkoani Ruvuma inampango wa kuwakopesha wakulima ili waachane na jembe la mkono

Bwana Mwambungu amewaambia waandishi wa habari kuwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ni wazalishaji wazuri wa zao la mahindi kwa kutumia jembe la mkono,na kama watatumia Matrekta na kuliacha jembe la mkono wazalisha mara dufu.
Kwa hiyo Serikali ya Mkoa huo itawapelekea wananchi matrekta ya kukopesha wakulima,maana msimu huu mahindi ni mengi yatauzwa na kubakia na ziada kwa chakula chao ,mkoa umetimiza kaulimbiu ya kilimo kwanza kwa vitendo.

Sunday, June 17, 2012

SALAAM ZA JUMAPILI KWA WATUMIJI WA MITANDANO YA KIJAMII MATUKIO YA MKOA WA LINDI

 Kijana huyo anaonekana akiendesha naiskeli kwenye mchanga pembeni mwa bahari,ni miongoni mwa akazi wa Mji wa Lindi Jioni kubaridhi kando ya bahari wakipunda upepo.
 Lakini wanapo kuwapo wenyeji na wageni hawakosikani basi siku hiyo nami pia nilipata muda wa kwenda kwenye bandari ya Mkoa wa Lindi ambayo sikuhizi haifanyikazi kama zamani.
 Asubuhi moja baada ya kumaliza shughuli Kilwa Masoko,tulikuwa tukijiandaa kwenda kilwa Kivinje kuendelea na shughuli zetu,kama unavyo Bwana Juma Nyumayo akiwa na begi lake tayari kuelekea standi ya mabasi hapo Kilwa Masoko.
 Hiyo ndiyo madhari ya ufukwe wa Pwani ya Lindi na vivutio vya Mikoko,ambayo imeenea Pwani yote ya Mwambao mwa Bahari ya Hindi.
 Wakazi wa Kilwa Masoko,Kisiwani na hata kilwa Kivinje ni wavuvi,Bwana Juma nyumayo anaonyeshwa na mvuvi wa Kilwa Masoko samaki  katika soko lao ambaye anauzwa kwa shilingi 20 elfu.
Hapo ni shamba la kutengeneza chumvi  yenye madini ya joto.  mkoani Lindi,ni aina ya ajira wanchi hao wamejiajiri kwenye ukusanyaji wa chuchi.

m


Thursday, June 14, 2012

VIONGOZI NA WATENDAJI WAWAJIBIKE KIKAMILIFU KWA WANANCHI –MKUU WA WILAYA YA SONGEA

 Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Joeph Joseph Mkirikiti akizungumza na waandhi wa habari ofisni kwake leo.Mjini Songea.
 Bwana Mkirikiti akiwaonyesha waandishi wa habari daftari la wakulima wa Manispaa ya Songe Mjini Magharibi lililo andaliwa na Mkuu wa Wilaya aliyestaafu Bw.Thomas Sabaya.na yeye anaanda dafutari la wafanya biashara wa manispaa ya Songea.
Waandishi wa habari wakiwa ofisini kwa mkuu wa Wilaya wakimsikiliza mikakati aliyoiweka ya viongozi na waendaji kuwajibika,maana uwajibikaji ni ngao ya maendeleo ya wananchi.
Waandishi wako makini kumsikiliza mkuu huyo leo ofisini kwake.





MKUU wa Wilaya ya Songea Bwana Joseph Joseph Mkirikiti ametoa rai kwa viongozi na Watendaji wa Serikali kuwajibika kikamilifu kwa wananchi ambao wao wanawalipia mishahara,na kwamba waache kufanya kazi kwa mazoea.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambao leo kuwa  rai hiyo ameshaitoa kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Songea Vijijini na hatimaye ataongea na waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri zote mbili za Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini..
         Bw.Mkirikiti alisema kuwa  wananchi wa Manispaa,Songea Vijijini na Mkoa mzima kwa jumla watumie fursa zilizopo katika kuwaondolea umasikini wa kipato kwani kutokana na takwimu za mkoa mwaka 2006 ,kipato cha mwananchi wa Songea ni Tshs, 156,000/= kwa mwaka.ambacho hakitoshelezi mahitaji ya mwanachi huyo.
        Aidha alisema wakitumia fursa hizo watazalisha zaidi watauza mazao yao ambapo watapata fedha zitakazo inua misha yao.Na kwamba yote hayo hayawezi kufanikiwa iwapo uwajibikaji utakuwa haufanyiki kikamilifu.
       Kutokana na hilo mkuu huyo amewsihi  watendaji hao wawajibike kwa wananchi katika kujibia kero zao  mbalimbali zikiwemo zinazohusiana na ardhi na wala wasigeuke kuwa madalali wa ardhi.
    Kuhusu changamoto zilizopo katika Wilaya zake, alisema zimeshaanza kushughulikiwa zikiwemo za umeme, ambao ulikuwa haueleweki vizuri lakini sasa upo katika hali nzuri,lakini alichokiona kuwa ni tatizo la uwajibikaji kwa watendaji wa “Tanesco” wa kufanya kazi kwa mazoea.
     Ametoa wito kwa vijana kutumia fursa ya Boda ya Msumbiji kwa kufanya biashara za mipakani,na kufanya bishara zao ndogondogo katika maeneo yaliyoruhusiwa badala ya kupanga barabarani na kuwa kero katika Manispaa.