Wednesday, June 13, 2012

HIVYO NI KWELI ? AKINA MAMA WANAMOYO MGUMU HIVYO? TAFAKARI!

Wewe na mie tuchunguze vizuri photo hiyo, ni dampo la takataka eneo moja huko Mtwara,lakini ukichunguza sana utaona ni uchafu uliyokuwa pamoja na binadamu,binadamu aliyezaliwa na mwanamke.
Ni kitoto kichanga kilichozaliwa na mama huko Mtwara na kukitupa kwenye lindi la mikusanyiko ya kila aina ya uchafu,Hivyo wimbo wa nani kama mama una maana yoyote kwa akina mama wenye moyo wa ukatili kama huyo? .je ni kitu gani kilicho msibu mama huyo hadi kufikia kufanya kitendo hicho kiovu.( Source Mitandao ya Kijamii ).

Saturday, June 9, 2012

SAFARI HII YA KIKAZI LINDI NA MTWARA NIMEJIFUNZA MENGI.

 Wenyeji wa Mji wa Lindi wanajishughulisha na ukusanyaji wa chumvi na kuiwekea mqdini joto,wajipatia kipato kutokana na kazi hiyo.
 Jioni nilikuwa natokea zangu bandarini Lindi mjini kuona jinsi majengo ya bandari hiyo yalivyo telekezwa
Hilo nalo ni eneo jingine ambalo chumvi inakusanywa na wakazi hao wa Mji wa Lindi,chumvi ambayo soko lake liko Dar es Salaam.
 Huyo na Mwanataaluma wa habari Kanda ya Kusini katika shughuli za kikazi Mtwara na Lindi Bw.Juma Nyumayo akiwa anaondoka kutoka Kilwa Masoko na Kuelekea Kilwa Kivijne kuendelea na shughuli hivi karibuni.
Hizo na ofisi za Bandari ya Lindi ambayo imetelekezwa,haifanyi kazi kama mwanzo ambapo meli zilikuwa zikitia nanga katika bandari hiyo.
Hilo na baadhi ya majengo yaliyojengwa enzi ya utawala wa kisultani mwambao wa Pwani ya Afrika mashariki,Hiyo miti siyo mapambo bali ni miti iliyoota ndani ya jengo na kubomoa kuta zake,Utalii usisubili wazungu kuja kuoana maajabu ya kale,na jinsi babu zetu walivyo weza kujenga majumba bila ya kutumia sementi au tofali.
 Nilikuwa nashangaa kuona mchanga ulivyo jaa kwenye eneo ambapo meli zilikuwa zikitia nanga enzi zake za MV Lindi ikitamba baharini siku mbili kutoka Dar es Salaam hadi Lindi,Tiketi unaisotea wiki mbili kwa bei ya halali Mlango wa nyuma siku moja au mbili unasafiri,Hizo hapo ni meli ambazo zinakarabatiwa ziludishwe Zanzibar.
 Pwani ya Lindi jioni watu wanapunga upepo
Wengine wanaogelea,wanacheza basi mradi wanajiburudisha kwenye bahari ya maji ua chumvi,hiyo ndiyo safari yetu na Bw.Nyumayo mikoa ya Mtwara na Lindi tutaendelea kipindi kijacho.

MKOROSHO UKITUNZWA VIZURI UNATOA MAZAO MENGI,WAKULIMA WA ZAO HILO KATIKA MIKOA YA RUVUMA,MTWARA NA LINDI WAMEHAKIKISHIWA SOKO LA UHAKIKA WA ZAO HILO

 Korosho ilipaliliwa inapendeza licha ya kuwa zao la bishara,shamba kama hilo lililoko Wilaya ya Lindi vijijini ni safi,pia hata uokotaji wa korosho zilizodondoka na rahisi,pia hata matunda yake " mabibo' wenyeji wa mikoa ya Mtwara huwa wanatengeneza pombe ya mambibo wanayoiita Uraka.
Walanguzi waliingilia soko la zao hilo kwa kasi kwa wakulima ambapo waliuuza korosho zao kwa bei ya hasara kwa sababu ya shida za wakulima wa zao hilo,lakini sasa Serikali imetoa angalizo kwa walanguzi na wakulia wapelekekorosho zao kwenye vyama vya Ushirika.

Sunday, June 3, 2012

HAPA KWETU SHEREHE NI CHAKULA'SHEREHE KULYA' MAMBO HAYO

 Msosi wa nguvu ulikuwa unapakuliwa tayari kwenda kwa kamwali Evaristi Jahazi na wapambe wake baada ya kumzawadia au kufupa.ni msosi kwelikweli .
Baadhi ya akina mama wakishuhudia tendo la kufupa na kurudisha MAJAMANDA kwa mama wa mtoto huyo ambayo yeye alikuwa akiwapa wenzake kwa shughuli kama hizo."Chama kiuyai" By Nguni People.


Mama kulia Evaristo katika na kaka Zenobius Matembo kushoto wakiwa nyumbani jana baada ya kutoka kanisani.

JANA MANISPAA YA SONGEA MKOA WA RUVUMA WATOTO WALIPATA KOMONIO YA KWANZA EVARISTO JAHAZI ALIKUWA MMOJA WAO

 Evaristo Jahazi mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mwembe chai Manispaa ya Songea Jana alipata Komoni ya kwanza katika Imani ya Kanisa Katoliki la Mitume.Amependeza na amefurahi kuingia katika hatua ya pili ya Imani ya Kumkiri Kristo.
 Hapo Evaristo akiwa na kaka yake Zenobius Matembo baada ya lutoka kanisani jana katika kanisa dogo la Matarawe Songea ambapo alipopatia Sakramenti hiyo ya kwanza.







Hapo ametulia  Bwana Evaristo.

KUNA KITU KIKUBWA KATIKA NGAO YA TAIFA

Hilo ni fumbo kubwa kwa watanzania ni Nembo inayo pendeza lakini ni ya kuichunguza na kuifahamu vyema.Ikienda sambamba na Ujumbe wake 'UHURU NA UMOJA' laiti kama watu wangelewa umuhimu wa Ngao ya Taifa na fumbo lake sidhani kama kungetokea baadha ya watu kuukataa umoja,Umoja huo ndiyo unatufanya tunaitwa watanzani 'wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania' Bila ya hivyo kutakuwa na Watanganyika,Wazanzibar na waPemba,Ambao wajaa Dar au Bongo ( Bara )
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliona mbali,na akakibuni kitu ambacho kina fumbo kubwa sana ,lakini kinapendeza na kuvutia Wa - Tanzania lakini sasa kinachukuliwa kinyume na matakwa ya Mwasisi huyo.

Utatu wa Roho Mtakati ni Umoja kwa imani ya Kanisa katoliki la Mitume Ilikuwa Jumapili ua jana

 Utatu Mtakatifu ni fumbo la Imani kwa waumini wa Kanisa Katoliki la Mitume,Utatu huo ni wa Baba,Mwana na Roho Mtakatifu.Ni Umoja katika Fumbo hilo Padre Otieno anasema Dunia inakubwa na jamii inayo kosa umoja ndani yao,ndiyo maana kuna matukio ya kila mara ambayo haya mpendezi Mungu.
 Hiyo ilikuwa ibada ya Kwanza katika mfululizo wa misa zinazo pangwa kila Jumapili katika Kanisa Kuu la Mathiasi Mulumba Kalemba la Jimbo kuu la Songea.
Padri huyo katika akifukiza ubani kwenye Altare Jimboni hapo jana,katika ibada ya Fumbo hilo.