Wednesday, May 2, 2012

MSANII ATHUMAN KENETH LAITI KAMA ATAPATA MUUNGWANA WA KUSAIDIA MASOMO YAKE DAR ES SALAAM ATAKUWA WA KUTUMAINIWA

 Kijana huyo anasoma Simba Theater Dar es salaam mwaka mmoja na nusu,sasa anakabiliwa na ukata wa kumalizia kozi yake ya kucheza na nyoka na sarakasi.
Kijana Mwanawane kwa jina la usanii aliburudisha umati wa watu siku ya Mei Mosi katika uwanja wa Majimaji Mjini Songea..Anaomba kupatiwa msaada huo,iwapo umeguswa kumsaidia kijana huyo namba zake za simu ni.( 0713- 843554 na 0752-994017 ) Saidia kuza kipaji cha msanii huyo.kutoa ni moyo na siyo utajiri.

BAADA YA MAJADILIANO WAWAKILISHI WALISOMA HOJA NA UTEKELEZAJI WAKE KATIKA KILA HALMASHAURI

 Waliyowakilisha hoja huyo ni mwaalimu Luya Ngonyani ( Katibu CWT Mkoa ) amewakilisha Tunduru
 Wapili ni Bwana Idd Alimbe Mponda DAS Mbunga ,aliwakilisha Mbinga
 Mkaguzi mkuu wa shule Wilaya ya Namtumbo Bibi Sekela Mwamwezi ,amewakilisha Namtumbo.
Bi.Enea Mpogole afisa elimu Vielelezo Songea Vijijini aliwakilisha Manispaa na Songea Vijijini
Mafunzo hayo yalikuwa mazuri na ya msingi kwa matarajio ya kuondoa kkk kwa wanafunzi wanao maliza elimu ya msingi bila kuwa na stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu.

HAKUNA MABADILIKO YA MTAALA WA ELIMU ,ILA KUNA MABORESHO YA MTAALA HUO – DKT MUSHI

 Dkt Mushi akielezea Tafakuri ya maboresho ya mitaala na mkakati wa mafunzo kwa wadau,katika ukumbi wa Maliasili Songea Ruruma jana kwenye mafunzo kwa wadau wa elimu mkoani humo.
 Afiaslimu Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo akimtambulisha wadau wa elimu kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania wa kwanza kushoto kabla ya kuanza mafunzo hapo jana katika ukumbi wa Maliasili Songea.
 Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Paul Mushi wakwanza kushoto.
Picha ya pamoja ya pili ambapo nami nikiwemo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Mushi wa katikati yangu.


MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Paul S,D.Mushi alisema hayo kwenye semina ya kazi kwa wadau wa elimu wa Wilaya za Mkoa wa Ruvuma zilizo jumuisha Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri,Makatibu tawala wa Wilaya,maafisaelimu,wakaguzi wa shule,katika ukumbi wa Maliasili Songea jana.

Dkt Mushi alisema kuwa watu waache imani potofu kuwa elimu inadorora kwa sababu ya mitaala ya elimu inabadilika kila mara,siyo kweli isipokuwa kuna maboresho ya mtaala ambapo imeboreshwa siyo zaidi ya mara 5 katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru.
   Aidha Dkt Mushi alisema Taasisi ya elimu imeweka mikakati ya kuinua elimu ili kuijenga nchi,kwa njia shirikishi kuanzia ngazi ya chini kabisa kwa lengo la kuwajengea watoto wamalizapo elimu ya msingi wajue kusoma,kuandika na kuhesabu (kkk).
Alisema wadau wa elimu wakiwa na mkakati wa kujenga stadi za msingi za kkk,nao watumia vikao katika wilaya na Halmashauri zao,na halmashauri hizo zitatumia midahalo ya wazi,katika ngazi zote,kaya,shule,Tarafa,Wilaya,Mkoa,Kanda hadi Taifa.
Alisema watu waguswe kwa pamoja sio kulaumiana na kunung’unika na kumtafuta mchawi kuhusu changamoto za elimu,bali kila mmoja kujipima binafsi jinsi anavyoweza kuwajibika  kila mdau ana wajibu wa kuguza hali ya mdondoko wa elimu nchini.
   Wakati huo huo wadau wa mafunzo hayo wamemhakikishia kuwa changamoto zote zilizoainishwa katika mafunzo hayo yatatekelezwa kwa kila Halmashuri ili kuondoa kero ya kkk kwa wanafunzi kutokana na hoja walizoziibua kwenye makundi ya majadiliano kwa kila Halmashauri.
    Baada ya majadiliano hayo kila wilaya ilitoa haoja walizoziibua ambapo Tunduru ilitolewa na Mwalimu Luya Ngonyani ( katibu wa CWT Mkoa wa Ruvuma),Manispaa na Songea Vijijini ilitolewa na Enea Mpogole Afisa elimu Vielelezo,Mbinga ilisomwa na Idd Alimbe  Mponda ( DAS Mbinga ) na Namtumbo ilitolewa na Sekela Mwamwezi Mkaguzi mkuu wa shule wa Wilaya.
   Leo Dkt Mushi ataelekea Jijini Mbeya kwa mafunzo kama hayo,hatimaye Mtwara Lindi kwa shughuli kama hizohizo.

KWENYE CHANGAMOTO ZA ELIMU WATU TUSINYOOSHEANE VIDOLE - DKT MUSHI TET

 Dkta Paul S.D.Mushi kurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania alisema kuwa katika changamaoto za elimu watu tusinyoosheane vidole wakati akitoa mada katika mafunzo ya kazi kwa wadau wa elimu Mkoani ruvuma leo katika ukumbi wa Songea Club.zaidi mada utapata kupitia Blog hii.
Wadau wakijadili mada katika vikundi
Picha ya pamoja na wadau wa elimu Mkoani Ruvuma leo.

Tuesday, May 1, 2012

MEI MOSI 2012,NI MISHAHARA DUNI,KODI KUBWA NA MFUMUKO WA BEI NI PIGO KWA MFANYAKAZI .LAKINI..........SONGEA MKOA WA RUVUMA UWANJANI SIKU HIYO KULIKUWA HIVI.

 Madaktari wa hospitali ya Mkoa Ruvuma Songea wakipitambele ya jukwaa wakiwa wanafanya upasuaji kwa mgonjwa siku ya Mei Mosi 2012 ,mbele ya mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Said Thabit Mwambungu
 katibu wa Chama cha TALGWU Bibi Pili Maganga uwanja wa majimaji Songea Mei Mosi 2012
 kikundi cha Jakaya cha lizombe kutoka Lizaboni Manispaa ya Songea wakitumbuiza Mei Mosi Uwanja wa majimaji jana.
 Dr.Broady Komba mjumbe wa baraza la TALGWA Taifa kwenye uwanja wa majimaji kuadhimisha Mei Mosi 2012 Mjini Songea Jana.
 Bi Theodosia Kasapira Katibu wa CWT Manispaa ya Songea katika uwanja wa majimaji jana ,Mei Mosi ,lakini wa walimu wa Manispaa hiyo wamezawadiwa Tshs.40,000 na cheti kama wafanya kazi bora.inatisha,mhudumu anapata Tshs.150,000 na zaidi,kweli walimu ni wito.
 Mwali Chete wa kulia akiwa na walimu wenzake katika jukwaa la majimaji akishuhudia walimu wenzake wakipata Tshs.40.000/=  kwa ufanya kazi bora na bora kufanya kazi.uwanja wa Majimaji Mei Mosi jana.
Maandamano yanapita mbele ya mgeni rasmi Mei Mosi jana Songea Mkoani Ruvuma .

MENEJA WA KIWANJA CHA NDEGE SONGEA APATA UFANYA KAZI BORA, ANAHAKI YA KUPATA TUZO HIYO MAANA NDEGE SASA ZINATUA

Bwana Valentine V.Fasha Air Port Manager SONGEA - RUVUMA - TANZANIA


MENEJA  wa uwanja wa ndege Songea Bwana Velentine  V. Fasha amesema kuwa ndege zinazo tua zinachukua abiria 13,kutoka Songea -Dar es Salaam na Dar es Salaam Songea.
Alisema kuwa iwapo mtu akikata tiketi wiki moja kabla atalipa nauli Tshs.250,000  ambapo mtu akikata tiketi zaidi ya wiki moja atalipa Tshs 350,000.Amesema leo kuna usafiri huo wa ndege.
Bw. Fasha amejinyakulia kitita cha Tshs.1,000,000 na cheti kwa ufanya kazi bora,Mtu anapofanya kazi yake kwa umakini na uaminifu kibusara apatiwe tuzo.
Mei  Mosi mwaka huu ni ‘ MISHAHARA DUNI,KODI KUBWA NA MFUMIKO WA BEI NI PIGO KWA WAFANYA KAZI’ kauli hiyo inaeleweka ! ! ! Nawatakia Mei Mosi njema wasomaji wote wa Blog hii.

MEI MOSI MKUU WA MKOA WA RUVUMA BWANA SAID THABIT MWAMBUNGU AWATAKA WAAAJIRI WASIZALISHE MADENI YASIYO YA LAZIMA

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said Thabiti Mwambungu akihutumia wananchi katika uwanja wa majimaji mjini Songea siku ya Mei Mosi leo.

 Baadhi ya viongozi waliyoandamana na Mkuu wa Mkoa.
Baadhi ya viongizi waliyoa andamana na mkuu wa mkoa wa Ruvuma leo Mei Mosi uwanja wa majimaji Mjini Songea



BWANA Mwambungu alisema hayo leo kwenye maadhimisho Mei Mosi inayoa adhimishwa duniani kote,katika uwanja wa majimaji mjini Songea ,akihutubia maelfu ya wqafanya kazi ambao kati yao 160 walitunukiwa fedha na vyeti kwa utendaji bora wao wa kazi.
Aidha mkuu huyo ametoa wito kwa viongozi wa dini,viongozi waina zote kuhamasisha wananchi kujitokeza kutoa maoni yao wakati wajumbe wa Tume ya katiba mpya watakapo wasili.
Ameongezea pia kuwa sambamba na kuhamasisha wananchi bila ya kujali itikadi za vyama vyo kujitokeza katika sensa ya kuhesabu watu itakayofanyika mwaka huu nchi nzima.
Alisema sensa ni uti wa mgongo wa maendeleo ya uchumi wa taifa,hivyo ni vyema watu watimize wajibu wao katika sensa ya kujua idadi ya watu ili serikali iweze kupanga shughuli zake za maendeleo kwa wananchi wake.
Mei mosi kwa kawaida wafanya kazi pamoja na kupewa tuzo lakini pia wanamatarajio makubwa ya kusikia serikali kupandisha viwango vya mishahara kwa watumishi wake ingawa hakitoshelezi malengo ya kila mmoja.