Saturday, February 4, 2012

WASHIKA BUNDUKI WA TIMU YA MLALE JKT IMETOKA SULUHU NA MAJIMAJI KATIKA UWANJA WA MAJIMAJI MJINI SONGEA

 Timu ya JKT Mlale leo katika pambano la kuwania tatu bora itakayoingia fainali katika Ligi ya Taifa ya Daraja la kwanza ambayo leo viwanja vya majima Songea,Sokoine Mbeya na Jamhuri Morogoro nyasi zimeng'oka.iliyo toka sare na Majimaji ya rezorezo.
 Timu ya Mlale JKT kabla ya kwenda mapumziko.
 Mchezji wa timu ya JKT Mlale Bw.Edward Malimi aliyelala baada ya kuchezewa rafu na mchezaji wa timu ya majimaji.
 Kikosi hicho kikisubiri baraka ya mgeni Rasmi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mpira wa miguu mkoani Ruvuma Bwana Joseph Mapunda.

Edward Malimi Mchezaji wa Mlale JKT akipata matibabu.baada ya kuumizwa na mchezaji wa timu ya majimaji.

MICHEZO ! ! ! TIMU YA MAJIMAJI AU WANALIZOMBE WAMETOKA SARE NA WASHIKA BUNDUKI WA MLALE JKT. LEO

 Hicho ni kikosi cha wana- lizombe majimaji wakiwa tayari kupambana na JKT Mlale katika uwanja wa majimaji leo.
 Benchi la tiimu ya Majimaji wa kwanza Kocha wa timu hiyo Mchezaji wa zamani Peter Mhina akiangali timu yake inavyo pambana na washika bunduki hao wa Mlale JKT leo katika pambano la Ligi ya taifa Daraja la kwanza.
 Goli kipa wa JKT Damas Victor Manyika akiokoa mpira wa hatari kipindi cha kwanza katika uwanja wa majimaji leo.
 Kikoai cha Mlale JKT kikiwa fit kwa pambano na Majimaji
Ilikuwa hatari katika lango la JKT mlale katika kipindi cha kwanza.



LIGI ya Taifa Daraja la kwanza iliyoendelea leo katika kiwanja cha majimaji Mjini Songea leo,kati ya timu za Majimaji na Mlale JKT wameshindwa kutambiana mbele ya wapenzi wa timu zote mbili.

 Katika kipindi cha kwanza timu zote mbili zilicheza katika kiwango kinacho fanana,ingwa majimaji walikosa mabao mawili ya wazi,hadi filimbi ikipigwa ya kipindi cha kwanza hakuwepo aliyeona mlango wa mwenzake.

Katika kipindi cha pili JKT walilielemea  sana lango la majimaji lakini  juhudi zao hazikuzaa matunda.wakatoka rezo rezo .na kugawana pointi.

Kwa mujibu wa katibu Mkuu wa Timu ya Majimaji Bwana Henry Kabera,alisema kuwa leo kulikuwa na viwanja vitatu vilivyo endelea na Ligi hiyo alivitaja viwanja hivyo kuwa ni pamoja na Majimaji  Ruvuma,Mbeya na Morogoro.

Kabera alisema Timu za majimaji,JKT na Polisi Iringa wana point 7 kila mmoja Mbeya City ina point 10 ambapo Prison Mbeya ina point 5,kutokana na matokeo ya leo Majimaji itakuwa na point 8 na Mlale JKT pia point 8,

Aidha magoli keepers wa timu zote walikuwa makini katika kulinda milango yao,Bwana Damas David Manyika wa JKT na Rambon Asheri wa timu ya Majimaji walitetea hadi kipenga cha mwisho.

Thursday, February 2, 2012

MAJAMBAZI SITA MBARONI KWA RUVUMA KUJERUHI NA KUPORA ZAIDI YA 4 MILIONI KWA TUMIA MILIPUKO


WATU sita ( 6 ) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa ujambazi wa kutumia milipuko,mapanga na visu,Mkongotema Tarafa ya Madaba Mkoani Ruvuma usiku wa kuamkia tarehe moja Februari mwaka huu.
Kamannda wa Polisi wa mkoa huo,Kamanda Michael Kamuhanda amewambia wandishi wa habari kuwa majambazi hao kabla ya kufanya uhalifu huo walipofika kwa Bwana Remigius Ngunja walipiga milipoko mine hewani kutishia wanakijiji wasiweze kutoa msaada.
Kamanda Kamuhanda aliyataja majambazi yahu kuwa ni pamoja na Baraka Beda ( 25 ) mkazi wa Morogoro,Salum Ahmadi ( 45 ) mkazi wa Mtwara na Stanley Mtega ( 20 ) mkazi wa Ludewa.
Na wengine walikamatwa kwenye msko wa polisi ni pamoja na Peter Mbilinyi ( 25 ) ,mkazi wa Mkongotema,Mfalme Rashidi ( 30 ) mkazi wa Hanga Ngadinda na Jemsi  Mtewele ( 21 ) mkazi wa magingo.
Alisema wote kwa pamoja wako mahabusu wakati upelelezi ukiendelea,kwa tuhuma za kukutwa na  milipuko ,ambayo hutolewa kwa kibali kwa wachimba madini,barabara ,na vikosi vya usalama.
Alisema majambazi hayo yalikwenda nyumbani kwa Bwana Remigius Nguja na kuwamuru atoe fedha,aliposita basi walimkatakata kwa mapanga kichwani,mgongoni na mikononi,kisha wakamwendea mkewe Bibi Oktaviana Danda  wakamtishia kuwa watamkata mikono ndipo walipowapa zaidi ya shilingi 3,000,000 na kutokomea gizani.
Baada ya bkufanya uhalifu hu walikwenda kwa nyumbani kwa Bwana  Igno ambapo walimkuta mlinzi Bwana Awito Mbilinyi,kwa kuona hivyo aliwaonyesha kwa boss kwa kuwa hawamjui naye aliwaambia Boss hayupo labda mkamuulize mke wake.ataambia alipo.
 wakamuuliza boss wako yuko wapi,
Kamuhanda alisema majambazi hayo yalikuwa yakifuatilia fedha shilingi 15 milioni ambazo walisikia mtu mmoja katika kijiji hicho anazo bila ya kuwa na uhakika na mwenye fedha.
 Walipomwendea mke wa Igno kumuuliza Igno alipata mwanya wa kutoroka majambazi ,Mkewe alibakia na kizazaa cha kuonyesha fedha zilipo, na kuporwa shilingi 1,026,000.
Aidha Kamuhanda alisema baada ya msako wa polisi wa Madaba wakishirikiana na Polisi wa Songea Mjini , waliwakuta watuhumiwa kwenye gari lenye namba za usajili T.435DHT Costa ya kutoka Madaba kwenda Songea

Wednesday, February 1, 2012

MGOMO WA MADAKTARI UKICHANGIWA NA POSHO KUBWA YA WABUNGE UNAWAPASUA WATU VICHWA

 Waandishi wa habari Bwana Juma Nyumayo kushoto mwenye shati na Benson Mapundwa kulia mwenye T - Shirt yenye ufito mwekundu wakijadiliana jinsi Serikali ilivyo amua kuhusu mgomo wa madaltari ,ambao Mhe.Waziri mkuu Mizengo Pinda alivyo waambia madaktari hao kufanya ili kuinusuru ajira yao.
Aidha mkanganyiko unajitokeza pale wabunge walipojipangia posho ya shilingi 200,000 kwa siku,hilo bado wananchi wengi wanashindwa kuelewa,na maswali maengi wanajiuliza,kama serikali inauwezo wa kuwalipa wabunge posho ya shilingi 200,000 kwa kikao,kwanini watumishi wa Umma wakiwemo Madaktari hao wasilipwe wanacho dai?.
Tufike mahali tutambue kila mtumishi ana umuhimu wake pale alipoajiriwa,na anastahili kulipwa kulingana na mabadiliko ya maisha hasa kwenye mfumuko wa bei.
Kinacho leta shida ni pale wanaogoma wanapokosa mshikamano wa kupanaga wagome vipi,na wakigoma je serikali ina fedha za kuweza kulipa wanacho kidai.
Ndiyo maana serikali imechukua uamuzi mgumu wa kuwapa masharti madaktari kurejea kazini ama kuendelea na mgomo,ili serikali ifanye juhudi za kutafuta madaktari wengine kwa lengo la nusuru maisha ya watanzania wasio na hatia.Kweli leo Madaktari kutoka jeshini wako Muhimbili wanafanya kazi,Ingwa sijambo zuri kuwanyima madaktari hao wanacho kidai,lakini pia si vibaya serikali kuwaweka pembeni hadi hapo itakapo kuwa na uwezo wa kuwatekelezea wanacho kidai.wakati maisha ya wananchi ipo kwenye usalama.

Monday, January 30, 2012

Wazazi kuchangia chakula shule ya sekondari Kalembo WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari Kalembo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wanachangia sh. 30,000 kwa muhula kwa ajili ya kupatiwa chakula cha mchana na uji wakati wa asubuhi,ingawa kiasi hicho hakitoshi. Mkuu wa shule ya sekondari Kalembo Bwana Bosco Haule alizungumzia umuhimu wa kutoa chakula kwa wanafunzi wanaosoma shule za msingi na sekondari mkoani hapo na nchi nzima kwa ujumla alipoitembelea ofisi za TUJIFUNZE leo. Bw.Haule alisema kuwa utaratibu wa kutoa chakula katika shule yake haukuanza hivi karibuni,bali ulianza toka mwaka 2005,kwa kutumia Bodi ya shule kuwahamasisha wazazi wenye watoto ambao wanasoma katika shule hiyo kwa kuchangia sh.30,000 kwa muhula. Alisema mchango wa sh.30,000 kwa muhula kwa kipindi hiki akitoshi,lakini kwa kubana matumizi wamefanikiwa kutoa uji na chakula cha mchana ,ambacho ni ugali kwa maharage,ingawa bei ya maharge hayo iko juu ikilinganishwa na bei ya mahindi katika mkoa wa Ruvuma. Kuhusu walimu Bw.Haule alisema walimu nao ili waweze kufanya kazi kwa usahii,na wao wanapata chai na chakula cha mchana kwa kuchangia sh.10,000 kila mmoja. Aidha Mkuu wa Shule huyo alisema kuwa kwa wanafunzi ambao wazazi wao hawakuchangia fedha au nafaka kwa ajili ya chakula

Mkuu wa shule ya Kalembo liyoko Matogoro nje kidogo na Manispaa ya Songea Bwana Bosco Haule akielezea jinsi alivyo fanikiwa kuwapa chakula cha mchana wanafunzi wa shule yake.Ansema ili chakula kipatikane shuleni ni vyema kufanya mikutano na wazazi wakubaliane kuchanga fedha na kiasi cha kuchangisha kwa kila mzazi.



WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari Kalembo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wanachangia sh. 30,000 kwa muhula kwa ajili ya kupatiwa chakula cha mchana na uji wakati wa asubuhi,ingawa kiasi hicho hakitoshi.

Mkuu wa shule ya sekondari Kalembo Bwana Bosco Haule alizungumzia umuhimu wa kutoa chakula kwa wanafunzi wanaosoma shule za msingi na sekondari  mkoani hapo na nchi nzima kwa ujumla alipoitembelea ofisi za TUJIFUNZE leo.
Bw.Haule alisema kuwa utaratibu wa kutoa chakula katika shule yake haukuanza hivi karibuni,bali ulianza toka mwaka 2005,kwa kutumia Bodi ya shule kuwahamasisha  wazazi wenye watoto ambao wanasoma katika shule hiyo kwa kuchangia sh.30,000 kwa muhula.
Alisema mchango wa sh.30,000 kwa muhula kwa kipindi hiki akitoshi,lakini kwa kubana matumizi wamefanikiwa kutoa uji na chakula cha mchana ,ambacho ni ugali kwa maharage,ingawa bei ya maharge hayo iko juu ikilinganishwa na bei ya mahindi katika mkoa wa Ruvuma.
Kuhusu walimu Bw.Haule alisema walimu nao ili waweze kufanya kazi kwa usahii,na wao wanapata chai na chakula cha mchana kwa kuchangia sh.10,000 kila mmoja.
Aidha Mkuu wa Shule huyo alisema kuwa kwa wanafunzi ambao wazazi wao hawakuchangia fedha au nafaka kwa ajili ya chakula cha watoto wao,hawapati chakula,ili wazazi wenye watoto hao waone umuhimu wa kupata chakula kwa wanafunzi.Nakwamba kila mwanafunzi anatumia sh.350/=  kwa siku.

ONA CLIP NILIYOIPATA KWA KARIBU KWENYE AJALI HIYO WAKATI BUS LETU LINAPITA ENEO LA TUKIO

Clip au video hiyo inaonyesha kipande cha tukio kilivyo tokea,bus hilo lilitangulia hapo jana  nasi tuli kuwa nyuma na Bus la Summry ya kwenda Songea wakati nikitokea Dar es Salaam kutoka Kilimanjaro nikokuwa kikazi kwa wiki moja.

Sunday, January 29, 2012

Mvua na zinazonyesha za sababisha ajali ya New Force Bus liendalo Mbeya kutoka Mbeya jana

i
 Eneo hilo la Nyololo kilometa chache kufika Makamabo Mkoani Iringa ni eneo baya hasa wakati wa mvua kuna utelezi sana.jana siku ya Jumamosi Basi  ' bus' New Force one lilokuwa likitokea Dar es Salaam lilipinduka,na kusababisha ajali.kwa kuwa Bus letu La Kampuni ya Sumry lilisimama mbali kidogo na Tukio ,ndiyo maana picha ya jirani haikupatikana.kama unavyoona juu kwenye malori ndipo kwenye ajali.
Lakini utaona clip hiyo niliyoipata  bus letu lilipo simama. kwa hiyo madereva wanapaswa kuwa waangalifi wakati wa 'overtaking lorries' wakati wa mvua na kwenye miteremko.