Friday, January 27, 2012

USEMI WA BONGO NIMEUSHUHUDIA LEO HAPA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mpiga picha wa Blog hii leo alipata nafasi ya kuona jinsi wabongo wanavyo jishughulisha na maisha,hapo ni eneo la Feri Jijini Dar es salaam maarufu kwa uzaji wa samaki wabichi pia wanaokaangwa.wakazi  wengi wanatoka kila pembe ya Jiji hilo kufika hapo kwenda kununua samaki wa kwenda kuwauza baada ya kuwakaanga,wasomesha watoto wao,wanajenga,aidha mahitaji yo yote muhimu wanapata kutokana na shughuli hizo,' Hiyo ndiyo bongo'
 Pilika pilika foleni ya magari ni kitu cha kawaida hasa muda wa asubuhi watu wanakwenda kazini na muda wa kurudi kazini.Hapo ni maeneo ya Manzese  Dar es salaam.
 Wanafunzi wasukuma mikokoteni ya kuuzia maji nao wako katika harakati ili mradi wawahi kwenye maeneo husika.Mpiga picha aliwakuta hao maeneo ya Mabibo Jijini Dar es salaam Leo.
Wenye baiskeli na watembea kwa mguu katika Jiji hilo ni wengi kushinda wanaokuwa kwenye usafiri,Lakini yote ni mema Jiji au mji hauwezi kuwa na sifa kama watu wa ina na nafasi tofauti watakosekana wote kwa pamoja ndiyo wanaofanya Jiji liitwe hivyo.


JIJI la Dar es Salaam wameliita bongo kutokana na watu wa Jiji hilo hutumia akili sana ili waweze kuishi katika Jiji hilo liitwalo Dar es Salaam,maana si dhani watu hao wana lala saa ngapi maana magari usiku kucha yanapita kuelekea yaendako  na yale yatokako.Mkazi mmoja hakupenda jina lake lijulikane maeeneo ya Feri ambako asilimia kubwa ya wakazi wa Jiji  Hilo ndipo wanapo patia maisha yao,alisema .
‘ Saa  kumi ya usiku kuna baadhi ya wafanyakazi wanaamka kujiandaa kwenda kwenye vituo vya daladala,na wengine wanajiandaa kuja hapa Feri kuwasubiri wavuvi kutoka kuvua samaki ili wanunue waende kuwakaanga na kuwauza,na asilimia kubwa ni akina mama.’
Lazima kutumia akili,kwenye uzalishaji mali ujasiliamali mdogomdogo,biashara za kuuza maji,matunda,mboga,Juisi,vyakula,plastiki za maji vyuma chakavu mama na baba ntilie.
Pia wapiga debe,waombaji,matapeli wanaotumia bongo zao kujifanya maofisa wa serikali au shirika Fulani,wanaojifanya wanauza simu ama saa za bei mbaya ,ambao wamewaliza wasafiri wengi Stendi kuu ya  mabasi yendeyo mikoani .Ubungo kwa kuwauzia vipande vya sabuni ama kibao wamevifunga  kwa ustadi kwenye bahasha ya kaki na kumkabidhi msafiri kwenye basi anapo fungua anakuta sabuni au kibao basi,Jamaa anatokomea mkwenye mabasi.hiyo ndiyo bongo.
Kwa utaratibu huo wasafiri wanatakiwa wawe macho,simu na saa mbona zimejaa madukani siku hizi! Kwa nini unataka ‘short cut’waogopeni sana watu hao sanacho kuonyesha sicho atakacho kukukabidhi baada ya kumpa fedha hata angevaa na kuwa nadhifu kiasi gani Wabongo hao.Samahani sio samaki mmoja akioza ndiyo wote hapana ila baadhi ya Wa – Bongo ni wajanja.  

Wednesday, January 25, 2012

MADHARI YA MANISPAA YA MOSHI MJI MSAFI KATI YA MANISPAA NILIZO TEMBELEA

Milipokuwa katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro,kwenye Round about yao ambapo mbele kuna jengo La Chama kikuu cha Ushirika Moshi ( KNCU ).
Aidha nikaenda tena kwenye Stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani Moshi Mjini.
Huo ni mji wa Manispaa ya Moshi unavyo onekana.

Monday, January 23, 2012

NI MUDA MREFU SIPO KWENYE MTANDAO,WASOMAJI WA BLOG HII NIKO KIKAZI MKOANI KILIMANJARO

 Mt Kilimanjaro ni mlima mrefu katika Afrika nipo huku
 Kibo mountain at Kilimanjaro Tanzania another Mawenzi not seen.
Tujielimishe Kanda ya Kaskazini Moshi Kilimanjaro  Mhariri wa Kanda hii ni Bibi Josephine Sanga Niko naye tunafanya kazi muhimu ya Kanda hii.

Friday, January 13, 2012

MADHARI YA MIJI YA DODOMA NA MOROGORO YANAVYO VUTIA WAGENI KATIKA UPANDAJI WA MAUA

 Kabla ya kuingia stand kuu ya mabasi katika Manispaa ya Dodoma utakutana na 'roundabout' hiyo ndipo utaingia katika Stand ya mabasi.
 Lakini ukiwa karibu na 'roundabout' hiyo mbele yako utaliona jengo la ukumbi wa Bunge linalo onekana mbele ya miti

Na hapo chini ni 'round about' mjini Morogoro baada ya kuipita 'roundabout' ya Stand kuu ya mabasi Msamvu.Ama kweli maua yanapendezesha mji kama yatatunzwa vyema.

Do you agreed with Shannon and weaver’s model ,and Wilbur Schramm and the Berlo Model. Argued that communication is not without barriers


.
Those scholars said that the barriers are related to:-
·        Lack of knowledge
·        Distraction
·        Lack of concentration
·        Education background
·        Physical impairments
·        Emotions and attitudes
·        Age
·        Socio-economics status and
            Appropriateness

Thursday, January 12, 2012

BAADA YA KAZI NI KUJIBURUDISHA NA VINYWAJI BARIDI

 Baada ya shughuli zangu tulitulia kwenye duka moja tukapata soda baridi,tukiwa na Kaka yangu Mzee Ally  mwenye kofia na Dada yangu Mrs Mnose,kimamba kilosa hivi karibuni.
 Hao ni dada Mrs mnose,kaka yangu Mzee Ally na aneno Mziwanza wote wa Kimamba wakipata soda,
Wakiwa wakibadilishana nawazo baada ya kupata soda.

Nilipokuwa Kimamba Kilosa Mkoa wa Morogoro baada ya Likizo yangu Nikutana walimu

 Ni picha ya pamoja ya walimu,mwenye kofia mwalimu Mnose na wa pili mwenye suluwali nyeusi ni mwalimu mkuu Bwana Kajika Gallan wote wa shule ya msingi Usagara Kimamba - Kilosa
 Bwana Mnose
 Bwana Gallan
 Bwana Mnose na shemeji yake Bi.Christina Hilaliyo
Mwalimu mkuu Bwana Kajika Gallan akiwa ofisini kwake