Thursday, January 12, 2012

LIKIZO NILIVYOITUMIA NIKIWA NYUMBANI DODOMA ILOANDAMANA NA UKARABATI WA NYUMBA YANGU ILIYOTEKETEA NA MOTO TAREHE 28/12/2011 MANISPAA YA DODOMA

a
 Sintosahau siku ambayo Mke wangu na mjukuu wangu Sara na mama mkwe Coleta ambayo wangepoteza maisha yao kwa kifo kibaya cha moto,ukliyotokea tarehe 28/12/2011 saa 1.30 usiku,moto uliyoanzia sitting room na dining room wakati Mrs Sikapundwa akiwa ndani na watoto wakiwa chumba kingine,ambapo mama huyo aliskia mlio kama bom,kumbe zilikuwa TV vikipasuka ndipo alipo gundua kuwa hatari.Mama ni yule mwenye nguo nyeupe na Sarah ni yule aliyeshika kiuno.
 Nilikuwa nashangaa jinsi moto ulivyo tekekteza mlango na dirisha.ama kweli kama siku za kufa mtu bado ,chuki na hila za binadamu haziwezi kufua dafu.Lakini watu husema kwa nini kumwingilia Mungu kazi yake?,kazi ya kuua ni ya Mungu peke yake,wengine wanamwingila.
Ukianagalia miujiza ya Mungu ,huwezi amini,kwenye ngzi ndogo kuna dirisha la blue,basi kwenye dirisha lile ndipo Mke wangu Mrs E.Sikapundwa alipovutwa na watu waliyofika kwenye tukio hilo siku hiyo ambayo shetani alitawala katika nyumba ile,lakini Mungu alikataa.
Nawashukuru majirani,Kikosi cha kuzima moto cha Manispaa ya Dodoma,Walimu wa shule za msingi za manispaa hiyo hususani shule ya msingi Makole ambapo mama huyo anafundisha hapo,Jumuiya tunayosali ya Makole na watu wote waliyoziokoa roho za wanafamilia yangu.sina cha kuwalipa bali na sema asante,

BREAKIN G NEWS AFGHANISTAN

Car bomb kills five people including distrhict governors,in south Afghanistan.

Wednesday, January 11, 2012

MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZINASBABISHA USAFIRI WA MABASI YAENDEYO KILOSA NA KURUDI MOROGORO KUWA MGUMU KUPITIA MELELA,MKATA,KIMAMBA HADI KWA KUWA NA BARABARA YA VUMBI KWA MIAKA KADHAA SASA

a
 Basi hilo limeharibika katika maeno ya Mkara Ranch ,kutokana na mvua zilizonyesha mfululizo na kusababisha barabara kuwa na matope,na kwamba magari mengi yanakata spring.
 Hilo ni basi ambalo nalo limekata spring lilivyoingia kwenye mashimo maeneo ya Faruma si mabli sana kutoka Kimamba.wamiliki wa mabasi hayo wanashindwa kuelewa kwa nini serikali inashindwa kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami?
Hiyo ndiyo barabara ya kutoka kilosa kupitia Kimamba,Mkata ,Melela hadi Morogoro,eneo hilo ndilo safi kidogo,isitoshe hata ukarabati haupo kwenye barabara hiyo,haijulikani ni kwa sababu haijatengewa fedha za Tan road za matengenezo,ama Halmashuri au Mkaoa wenye jibuni Waziri mwenye dhana lakini pia na Mbunge wao wa Kilosa,anaona na anapita kwenye barabara hiyo nadhani hata ifimbia macho barabara hiyo ilwe kwenye kiwango cha lami.

kilio cha wakulima wa Wilaya ya Kilosa,kinagonga mwamba kila mara kwa uongozi wa Wilaya hiyo wanapopeleka kesi za kuliwa mazao yao na ng'ombe wa wafugaji wa kimasai

 Makundi kwa makundi ya ng'ombe wa wafugaji wa kabila la wamasia yamekuwa kero na hasara kubwa kwa wakulima wa wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.
Wakulima wa Tarafa ya Kimamba,Madoto,Rudewa Msowero, wanapata shida sana na wafugaji hao ambao wanalisha ngombe wao kwenye mashamba ya watu kwa makusudi.'mashamba tuna kodishwa kwakuwa maneo tunayolima na mashamba ya mkonge ya mwei wa kukezaji,wakati  mazoa yakikomaa wamasai wanaingiza ng'ombe zao kulisha,ukipeleka kesi hiyo kwenye uongozi wa wilaya wanakuambia nenda tunashughulikia,utapigwa kalenda,kwa kuwa wamasai hao wana fedha za kutoa kwa wakubwa na wakulima hatuna kitu.' walisema wakulima hao ambao hawakupende majina yao yajulikane.na kwamba walisema viongozi wa ngazi zote wananufaika na kuliwa kwa mazao ya wakulima ktika wilaya hiyo.
Jeuri ya fedha inawapa kichwa maji wamasai wafugaji,wakulima walala hoi wanambulia patupu,Ukweli Serikali ijaribu kuangalia hakiza wa wakulima hao,bila ubaguzi wa nani ana fedha na mwengine hana basi akose haki yake,ndiyo kila mika kuna kuwa na mapigano kati ya wakulima na wafugaji hao katika wilaya hiyo.

SERIKALI IJARIBU KUIOKOA RELI YA KATI ,HALIYA RELI HIYO INASIKITISHA,TRAIN KUPITA KWENYE RELI ILIYO GUBIKWA NA NYASI NI HATARI ,HAKUNA USALAMA

Hiyo ni reli ya kati katika station ya Kimamba Kilosa Mkoa wa Morogoro,hali kama hiyo hapo ni station je katikati ya mikoa ya Dodoma,Tabora,Kigoma,shinyanga na Mwanza hali iko vipi.,Kama mwekezaji yupo basi ifanye jitihada ya kuwarudisha wafanya kazi wa magenge mabo mwanzo walikuwa wanaita pigilia,amabo walikuwa wakifanya usafi katika reli hiyo na wakaguzi wa reli,ili kuwe na usalama wa train. lakini sasa hawapo hao,kwa utaratibu huo ajali zitakosekana?
Reli ya kati ni muhimu sana kwa kusafirisha mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma,Mwanza na kurudisha mizigo mingine,aidha ilisaidia sana wasafiri amabo hawana kipato cha kutosha ,hasa nauli za mabasi,Hebu serikali hasa wizara ya miundo mbinu ijariku kulikwamua shirika hilo kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

MUHULA WA MASOMO KWA SHULE ZA MSINGI UMENZA JUMATATU WIKI HII KATIKA SHULE YA MSINGI USAGARA KIMAMBA KILOSA WANAFUNZI WANAONEKANA WENYE FURAHA

 Ni saa moja na nusu asubuhi ya Jumatatu wiki hii wanafunzi wa shule ya msingi Usagara Kimamba Kilosa Mkoa wa Morogoro wakiwa kwenye sare zao za shule kutoka awali wenye sare za kijani hadi darasa la saba wakiimba wimbo wa Taifa na wimbo wa shule ,wakiwa na walimu wao wakiwa na ari ya kuanza ngwe ya kwanza ya kazi yao ya kuelimisha Taifa hili.
 Wanafunzi wa Awali wakiwa na kaka na dada zao kwenye mistari ,tayari kwa kuingia madarasani.
 Hao ni wanafunzi wa darasa la saba ambao wanaingia darasa hilo kwa mara ya kwanza kutoka darasa la sita.
 Baadhi ya walimu wa shule hiyo waliyo kutwa na blog hii asubuhi hiyo wakiwa wakisubiri wanafunzi kuingia madarasani ili wakafanye kazi yao ya kufundisha.Ambapo hapo awali kazi hii nyeti ilikuwa ni kazi ya wito,bali sasa imekuwa ni kazi kama kazi nyingine,wanaingia hata wale wasiyo na wito kwa kuwa walikosa kazi.walimu kama hao wanakosa maadili ya ualimu.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba waliyokuwa wakifanya usafi kwenye ofisi ya mwalimu mkuu wakijisifia kuwa waote watafaulu mtihani,shule hiyo ina wanafunzi 65 wa Awali na 540 wa shule ya msingi na kufanya idadi ya wanafunzi 605.

Sunday, January 1, 2012

NAWATAKIENI HERI KWA MWAKA MPYA 2012 UWE WENYE AMANI ,UTULIVU,NA FARAJA DUNIANI,MSHIKAMANO WA WATU WALIYOKATA TAMAA YA MAISHA .

NI muda mrefu kiasi sijaonekana katika mtandao wa Blog TUJIFUNZE KUSINI kwakuwa  ni ko likizo  nyumbani Dodoma.ambako niliunguliwa na nyumba hivyo umeme nategemea kesho au kesho kutwa tutakuwa sote hewani
 Nawatakieni Jumapili njema ya mwaka mpya wa 2012  juma la kwanza la mwaka  mpya.