Thursday, August 4, 2011

Profesa Mbele kesho anaelekea Dar es salaam kuwapokea wanafunzi wake wawili ambao wanakuja kwenye ziara ya mafunzo ya elimu ya juu,hivyo bado yupo Tanzania,miji ya Iringa na Mbeya

 Waandishi hao wa habari mjini hapa wamekuwa na faraja kubwa kukutana na Profesa Mbele ana kwa ana kwani Profesa huyo ni mara yao ya kwanza kukuta,ila kwenye mtandao wa Blog,hivyo wamepata chakula cha jioni kiitwacho mchemsho wa kuku,ndizi,nyanya chungu na njegere,lakini kwa Profesa hana matatizo na vyakula vyetu kwani yeye ni mzaliwa wa mkoa huu wa Ruvuma Wilaya ya Mbinga Matengo ( Litembo )
 Hapa Profesa Mbele kabla ya wanahabari kuwasili katika ukumbi wa Serengeti Mjini hapa jioni hii ya tarehe 4/8/2011
Waandishi wa habari nao wanamambo wametaka kujua wasomi wa Marekani wa elimu ya juu ni sawa na wasomi wa elimu ya juu nchini Tanzania? Profesa aliwaambia kuwa wasomi wa Marekani wanasoma masomo mengi akatolea mfano kama mwanafunzi anasomea lugha huyo atasoma masomo mengi ili awe na ufahamu mpana katika elimu yake.Tofauti na elimu ya juu nchini kwetu.
 Profesa Mbele anakwenda Dar es salaam kesho kupokea wanafunzi wake wanao fika kwenye ziara ya mafunzo,atakuwepo nao hadi tarehe 5/9/2011 kwa shughuli hiyo tu.Prof.anazichunguza noti mpya za Tanzania.
Inapendeza kukutana wanamtandao wa blog hata siku moja hamjawahi kulkutana ila kwenye mtandao.atakapo kuwepo Iringa atapenda kukutana na Mzee wa matukio,Blogger wa Iringa,na wa Mbeya.Aliyosimama naye Profesa Mbele mwenye shati leusi na ukosi mweupe ni baadhi ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma wakibadilishana mawazo na mgeni wao.

PROFESA JOSEPH MBELE AONGEA NA BAADHI YA WANACHAMA WA RUVUMA PRESS CLUB SERENGETI JIONI HII MJINI SONGEA BAADA YA KUTOKA MBAMBA - BAY

 Profesa Joseph Mbele wa Northfield Minnesota United States aliyevaa shati leusi na ukosi mweupe akiwa na baadhi ya wanachama wa Ruvuma Press Club katika ukumbi wa Serengeti katika Manispaa ya Songea jioni hii baada ya Prf. huyo kutokea Mbamba - Bay  ziwa Nyasa,kupata habari na pupata picha za mwambao mwa ziwa hilo.Wa kwanza kulia ni shemeji yake Prof.jina halikupatikana,wa pili mwenye sweeta yenye mistari ni Blogger Bw.Sikapundwa ( mwandishi wa habari ) wanne mwenye miwani ni Bw.Mwakanosya wa Nipashe.
 Dada Cresensia kapinga  mwenye gauni lekundu ni miongoni mwa waandishi wa habari wa club hiyo wakibadilishana nawaza na Prf.Mbele katika ukumbi wa serengeti mjini Songea.
 Ni picha ya pamoja na Prf,Mbele wakati akielezea jinsi wazazi wa Marekani wanavyo wasaidia watoto wao baada ya kutoka shuleni,iwapo watakwama katika somo ambalo wamepewa kazi ya kufanya nyumbani ( home work ) Hii inaonyesha jinsi wazazi wa -Tanzania wasivyo kuwa makini katika kufuatilia watoto wao wanaosoma na kile wanachojifunza kwa siku ile.
Profesa Mbele akizishangaa noti mpya za shilingi 2,000,5,000 na 10,000 za Tanzania  maana tangu noti hizo zianse kutumika ni mara yake ya kwanza kuzitumia baada ya kuingia nchini.Mwandishi wa Nipashe Bwana Gedion Mwakanosya aliyesimama akitoa maelezo mafupi kwa Profesa kuhusu noti hizo jioni hii katika ukumbi wa Serengeti Mjini Songea.

Wednesday, August 3, 2011

BLOG YA TUJIFUNZE KUSINI INAWATAKIA WAISLAM WOTE DUNIANI MFUKUNGO WA MWEZI MTUKUFU KATIKA KUTENDA MEMA

Wafanya biashara wasiutumie mwezi huu vibaya kwa  kupandisha bei bidhaa muhimu kwa ajili ya daku na kufuturu,kwa waliofunga.ni mwezi wa kutenda mema,kutenda mema ni kuacha mabaya na kufanya matendo yanayo mpendeza Mungu.Kuna baadhi ya wafanya biashara hutumia mwezi wa mfungo kama ni mwezi wa kuchuma,wasifanye hivyo kwa nini bei zisibakie zilezile za juzi kabla ya mfungo?

Tuesday, August 2, 2011

SHEHENA KUBWA YA MAHARAGE IMEKUSANYWA NA WAUZA NAFAKA SODECO MAINISPAA YA SONGEA HUSAFIRISHA NJE YA MKOA

Hayo ni magunia ya maharage ambayo yamepangwa hapo yakingojea kusafirishwa kwenye nje ya mkoa huu wa Ruvuma.wafanya biashara wanafuatia mazao haya ya mahindi na maharage vijijini kwa wakulima.wakiyafikisha katika soko hili wanauza kilo moja ya mahindi ni shilingi 300/= maharage shilingi 850/=.

Wakati kilo moja ya maharage katika soko kuu la songea ni shilingi 1000/=,wanaokoboa na kusaga unga wa mahindi wana jaza kwenye mifuko ya kilo 30 na kusafirisha mkoa wa Lindi kuuza.


MJI WA SONGEA LEO UNAVYO ONEKANA

 Ni mtaa mmojawapo katika Manispaa hii ya Songea ambayo jana imempoteza Meya wake aliyefariki hospitali ya Peramiho na kuzikwa Lizaboni nyumbani kwake.
Hivi ndivyo wakazi wa mji huu walivyokuwa wakihangaika katika ujenzi wa Taifa kila mmoja jinsi alivyojipanga toka asubuhi hadi blog hii ilipomkuta.

MANISPAA YA SONGEA JANA IMEINGIWA NA MAJONZI MAKUBWA BAADA YA KAELFU YA WAKAZI WAKE KWENDA KWENYE MAZISHI YA MSTAHIKI MEYA ALLY MANYA NUMBANI KWAKE LIZABONI

Wananchi na waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Songea wamempoteza Mstahiki Meya ally Manya aliyezikwa nymbani kwake Lizaboni,kiongozi wa mazishi hayo alikuwa Waziri wa habari na Vijana Mhe.Emanuel Nchimbi ambaye aliongoza maelfu wa waombolezaji katika mazishi ya mstahiki Meya huyo.

Aliweka mikakati kadhaa ya kuinua manispaa hii kimaendeleo na usafi lakini mipango ya Mungu imefanya malengo yake yasitimie.Mungu ailaze roho  ya marehemu Manya mahali peme peponi Amina.

Wakati wa uhai wake Mstahiki Meya Ally Manya akiongea na wadau wa habari na wana habari katika ukumbi wa Songeaa club mwaka huu.

Monday, August 1, 2011

BLOGGER YASINTA NGONYANI NA MMEWE BWANA TOSBJOIN KLAESSON NA MTOTO WAO ERIK KLAESSON KUTOKA SWIDEN WATMBELE OFISI ZA TUJIFUNZE KUSINI

 Kuja kwake nyumbani Tanzania Blogger Yasinta Ngonyani na Mr wake Klaesson Mkoani Ruvuma kumempatia fursa ya kutembelea ofisi za Blog ya TUJIFUNZE KUSINI kuziona,ni ugeni mkubwa kwa TUJIFUNZE kutembelewa na Blogger wa nchi za nje,tuna sema karibu tena katika ofisi zetu.Hapa nia Mr ana Mrs Tosbjooin katika ofisi ya TUJIFUNZE Jana.
 Hapa ni kijana wao Erik Klaesson akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya TUJIFUNZE KUSINI jana katika Manispaa ya Songea Matarawe.
 Mr Klaesson akiwa katika ofisi ya Mhariri msaidizi wa TUJIFUNZE KUSINI Bwana Juma Nyumayo hapa jana.
 Bw.Juma Nyumayo akimwonyesha picha ya zamani ya Bw.Sikapundwa aliyopiga mwaka 1990 katika Manispaa ya Moshi,Blogger yasinta Ngonyani klaesson katika chumba cha habari news room jana.
 Erik ni mtaalamu pia wa kupiga picha,hapo alikuwa akipiga matukio katika chumba cha habari sabasaba Matarawe hapo jana.
 Bw.Nyumayo anawaeleza namna mashine za TUJIFUNZE zinavyofanya kazi
 Hapa wanaonyeshwa mashine ya kukata karatasi Polar
 Hatimaye wakiwa chumba cha Computer.Wageni wetu wanaishi nchini Swiden wapo Mkoani Ruvuma kwa mapumziko,kesho kutwa wanatarajia kurudi nyumbani kwao Swiden,tunawatakia safari njema.