Sunday, May 1, 2011

PAPA JOHN PAULO ATHIBITISHWA KUWA MWENYE HERI MUNGU AMPE BARAKA

Waumini wa Roman Catholic Duniani jana wameungana na wenzao Vatican City kwenye mkesha wa ibada ya uthibitisho wa Marehemu Papa John Paulo kuwa mwenye heri.Juma pili ya Pili ya Pasaka Makanisa mengi yametumia nafasi hii kumshukuru  Mungu katika kumfanya Papa huyo kuwa mwenye heri.

SEND - OFF YA CATHERINE ILIKUWA NA MAMBO MAZURI KWELI HASA KWA WANYWAJI STADI

 Hizi sherehe nazo wakati mwingine wapiga picha wanaweza wakakukuta hujajiandaa wana kuchukua tuu,ulikuwa usiku wa katikati ya sherehe walinipiga picha hii,nakama ninge kuwa bingwa wa kumimina maji sijui ingekuweje.lakini yote mema kwa siku hiyo.
 Baba na Mama Dr.Tonya wa Hospitali ya Peramiho wakienda kutoa nasaha kwa Binti yao Catherine Mwikwa na wageni waalikwa.katika ukumbi wa Songea Club.
Catherine Mwikwa alipewa zawadi nyingi zikiwemo za utamaduni kama huo kingoni wanauita mpasa almaarufu kwa kukalia wageni,wakati wa raha na taabu.

MEI MOSI NA MBWEMBWE ZAKE WENGINE WANANEEMEKA WENGINE HIVYO HIVYO TENA.

 Maandamano ya magari kutoka matawi mbalimbali ya sehemu za kazi yakielekea kwenye maonyesho ya Mei mosi katika uwanja wa majimaji Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
 Tawi la TUGHE la Manispaa ya Songea wakielekea uwanjani majimaji kwenye maonyesho na hotuba za Mei Mosi mwaka huu  kiwilaya zimefanyika wilayani hapa leo.

Wengine wapata zawadi ya fedha na vyeti na wengine patuou

LIGAMBUSA NI NGOMA MCHANGANYIKO NA MGANDA INAASILI YA UMANDA

 Kikundi cha Kasukilo kikicheza mbele ya jukwaa la mgeni rasmi siku ya Mei Mosi wakiwatakia wafanya kazi kufanya kazi kwa bidii na nidhamu kazini.
 Ligambusa ni kikundi cha Kasukilo Salumu Ligambusa cha Lizaboni  Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma,ni ngoma inayochezwa wakati maalumu kama vile sherehe mbalimbali za kitaifa,asili ya ngoma hii ni mwambao mwa ziwa nyasa hasa Umanda.
 Hiyo ni ngoma ya Ligambusa ikipigwa kama gita  ,pia kama kinanda kwa kuvuta kamba  kwa mguu yenye manyanga juu ya ngoma,basi inapendeza kweli kweli.ukiiona karibu ( live )
Picha ya pamoja ya kikundi hicho maarufu kwa jina la Kasukilo Ligambusa Lizaboni,mji maarufu sana hapa Songea.

NGOMA ZA MKOA HUU LEO ZILITUMBUIZA KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI

 Kikundi cha Mrisho Jakaya cha Lizaboni Manispaa ya Songea kikitumbuiza Mei Mosi mwaka huu na mkuu wa kikundi hicho ni Bwana Pius Michael
 Kikundi cha Lizombe ya ukweli sio photocopy wakitumbuiza kabla na baada ya hotuba za wageni mbalimbali Mkoani hapa.
Picha ya pamoja ya wanalizombe hao mwenye sutu ya orange ni Bwana Pius Michael mkuu wa kikundi hicho.

JUMAPILI YA PILI YA PASAKA PAMOJA NA MEI MOSI KAZI SIO ADHABU BALI NA BARAKA

 Baada ya Yesu Kristu kufufuka wafuasi wake waliingiwa na woga hivyo alijifungia ndani pamoja,Lakini ili neno litimie Yesu aliwatokea na kuwaambia 'Amani iwe kwenu'.ndipo mahubiri katika ibada hiyo iliyofanyika katika kanisa kuu la Jimbo kuu Songea.yalisema  tuiombee nchi yetu iwe na amani.Pia Mei Mosi tuwaombee wafanya kazi na waajiri kutimiza wajibu wao kama waajiri na wafanya kazi kama waajiriwa.Maana hali ni mbaya,wafanya kazi wanafanyakazi katika mazingira magumu,hawapati stahili zao.




kwaya ya Matias Mlumba Kalemba iliyo kolezea ibada ya leo ya jumapili ya pili ya Pasaka na Mei Mosi sherehe zilizofanyika  kiwilaya katika uwanja wa maji maji  manispaa ya Songea  Mkoani Ruvuma.

MEI MOSI MWAKA HUU WAFANYA KAZI WAMETAKIWA KUJIANDAA ILI BAADA YA KUSTAAFU WAISHI MAISHA MAREFU

 Mei Mosi mwaka huu kiwilaya imefanyika katika uwanja wa maji maji.Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Thomas Ole Sabaya.katika hotuba yake amewataka wafanya kazi waandae vyema maisha yao baada ya kustaafu kwao.Alisema wajiandae kiuhalali na sio kuiba maana watafungwa..
Mkuu huyo amewapongeza wote waliozawadiwa kwa kufanya kazi kwa bidii na wengine waige mifano yao,pia alisema wanaopata zawadi kweli wawe wanasifa sio zamu yao imefiaka wapewe.
 Mkuu wa Wilaya Bw.Sabaya anampa shilingi laki mbili na cheti mwali Eva Kazimoto wa shule ya sekondari Ruvuma.Mfanyakazi wa TANROAD ndiye aliyepata zawadi kubwa kuliko wote kwa kupata sh.700,0000.
 Maandamano ya magari ya taasisi mbalimbali zikielekea kupita mbele ya mgeni rasmi kuonyesha shughuli zao.
 Mfanyakazi akikabidhiwa sh.200,000 na cheti katika kilele cha Mei Mosi kilichofanyika kiwilaya katika uwanja wa majimaji  manispaa ya Songea leo.