Monday, April 25, 2011

JUMA TATU YA PASAKA , NILITEMBELEA KUONA RELI YA KATI YA DAR ES SALAAM HADI KIGOMA NILIONA KAMA HIVYOO!!1

 Hapa ni Dodoma Railway Station ukiangalia mbele yako Train inaelekea kigoma,Ukweli miundo mbinu ya Shirika hili ni mibaya ndiyo maana ajali nyungi zinatokea kila mara katika Reli ya kati kwa sababu reli hii imesahaulika hakuna usafi ,hakuna uangalizi wa kuchunguza mataluma yaliyo tolewa na wahujumu wa mali ya umma.
Hapa Reli hii inaelekea Dar es salaam ona ilivyo kuwa na nyasi nyingi ,sasa hapa ni mjini Dodoma je huko katikati ya safari kama vile Zuzu, Malampaka,na sehemu nyingine kukoje,tatizo yale magenge ya wafanya kazi wa Reli hayapo tena.Serikali inusuru Reli hii kwa kuwa ni kiungo pekee cha safirisha mizigo kwenda nchi jirani.

Sunday, April 24, 2011

WATAALAMU WA KUCHIMBA NA KUSAFISHA SEHEMU NYAO FOOT PRINT LAITONI ARUSHA ZINAENDELEA

 Huyu kiumbe aliyeishi Laitoni Arusha nyayo zao zipo Laitoni zimehifadhiwa kitaalamu na sasa zimekuwa kivutio na chanzo cha ingizia fedha za kigeni kwa shughuli za utalii.
 Hayo ni mafuvu ya viumbe hao ambao inasemekana kuwa hawakuwa na lungha ila walikuwa wakitoa sauti tu
 Mtangazaji wa TBC akihojiana na mtaalamu wa mambo ya kale katika kijiji cha laitoni,akisema vijana wa kimasai wamefundishwa jinsi ya kupokea na kutembeza watalii.Alisema serikali kwa kushirikiana Wizara ya Utalii na maliasili na Ujenzi zimeweka miundo mbinu ya barabara kuwa bora ya kupitika majira yote ya mwaka.
Wataalamu wa nje na wandani ya nchi wakisafisha nyao ( foot Print ) za Binadamu wa kwanza aliyeishi eneo hilo la kihistoria Laitoni Jijini Arusha - Tanzania.

Nyimbo za kumsifu bwana zilisikika katika Ibada ya Pasaka makole Dodoma leo


Blog hii inaungana na wakristo wote duniani kuadhimisha kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo kwa Ibada na nyimbo kama hivyo

Mtaalamu  wa nota katika muziki akikolezea kwaya ya Parokia ya Makole siku ya Pasaka leo Manispaa ya Dodoma.
l
 Picha ya pamoja ya wanakwaya hawa wakati wakiimba ule wimbo wa Aleluya bwana amefufuka aleluya.
Wana - kwaya hao wakitoka nje baada ya Ibada ya kwanza kanisani hapo.

Nyoka na sifa zao Dr.Victor Mwafongo

 Dokta Victor Mwafongo anachanganua aina za nyoka.Alitaja kuwa ni pamoja na nyoka wa :-
  • Wa shimoni
  • Miti  
  • Baharini
  • Misitu
Wapo wenye sumu kali kama green mamba ( Cobra ) wenye sumu wana meno marefu ya juu,wale wenye meno madogo madogomadogo hawana sumu.

Wale watu wanaochezea nyoka kuwa wanawatoa meno ndipo wanacheza nao nyoka hao haijalisha anasumu au laa.

UFUFUKO WA YESU KRISTU ULETE AMANI,UMOJANA NA MSHIKAMANO MIONGONI MWA WATANZANIA

 Heri ya pasaka kwa watu wote Duniani kwaa  wanao mwamini na wasio mwamini,Padre Adam Mbando wa Parokia ya Makole Manispaa ya Dodoma akiwa mbele ya Altare akisubiri vipaji.' Ufufuko wa Yesu Kristo ni ishara ya uko mbozi wa binadamu wenye dhambi,hivyo watu wazidi kusali sana ili kuiombea nchi yetu maana kunajitokeza matendo yanayoonyesha uvunjifu wa amani' Alisema Padre Mbando.
 Aleluye Bwana amefufuka,aleluya imeenea duniani kote kwa watu wenye mapenzi mema.Padre Adam mbando wa Parokia ya Makole Manispaa ya Dodoma,Amesema watu wanatakiwa wafufuke na Bwana wetu Yesu Kristo.Alisema Baadhi ya Wa- tanzania wanataka kuharibu kisiwa chetu cha Amani cha Tanzania.
Amani ikikosekana ubinadamu unapungua,Yesu Kristo aliteswa kisha akafa,siku ya tatu alifufuka,kuonyesha utukufu wake,na hakuna ufufuko bila ya kifo,na hakuna kalvari bila ya kuteswa.Na umaskini wa watanzania sio ni laana tuliyopewa na Mungu,hapana bali ni ukosefu wa uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo, kwa wale waliopewa dhamana ya kuongoza nchi.
 
 Kwaya ya Mtakatifu Kaloli lwanga iliyo kolezea Ibada ya Pasaka ya asubuhi katika kanisa la parokia ya Makole katika Manispaa ya Dodoma na Mkesha wa Pasaka.
Honhera zao wanakwaya hao Mungu awabariki wazidi kukoleza katika Ibada mbalimbali katika Parokia ya Makole.

SIKUKUU ZINA MAMBO YAKE ILIKUWA HIVI JUMAMOSI KUU ONE WAY MJINI DODOMA

Hekaheka za maandalizi ya sikukuu ya Pasaka zilikuwa zikijitokeza kila uendapo katika Manispaa ya Dodoma Jumamosi Kuu,watu walikuwa wakitafuta mahitaji kwa ajili ya Pasaka.Lakini kutokana na umati wa watu katika mitaa ambayo ni mifinyu kwa ajili ya watu na magari na pikipiki,Dereva wa Taxi  ambaye alikuwa nyingi asubuhi subuhi alijikuta anamkwaruza mwendesha pikipiki.Ikawa pata shika washukuru Mungu Trafic hawakutokea.

Pombe hizi jamani zinaleta mambo hasa wakati huu wa sikukuu,Serikali inashauri waendesha vyombo vya moto wawe makini siku hizo,na wasiwe nyingi wakiwepo barabarani lakini haisaidii.Tufanye nini kuepuka ajali?