Ni siku pekee kwa wakristo kukumbuka siku ambayo Yesu Kristo anakamatwa na kuteswa kisha kutundikwa Msalabani kwa ajili ya dhambi za wanadamu baada ya Adamu na Hawa kukiuka maagizo waliyopewa na Mungu.
Friday, April 22, 2011
Wednesday, April 20, 2011
HABARI KWA UFUPI KITENGO CHA HABARI,ELIMU NA MAWASILIANO KUANDAA TOLEO MAALUMU ARINE MOROGORO
Ni siku ya kwanza kabisa baada ya wajumbe wote kuwasili katika hotel ya Arine Inn eneo la Kola hill Morogoro.
Kitengo cha Habari ,Elimu na Mawasiliano na Wahariri wa Jarida la Elimu Tanzania (Ed- SDP ) wa kanda saba za Elimu Tanzania huwa wakikutana kuandaa Jarida hilo Mkoani Morogoro ili kuandika mambo muhimu kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.Wakwanza ni Mhariri wa Moshi kilimanjaro na Oliva kato wa Kitango cha habari wakiandika habari.
Mhariri Mstaafu wa tabora Bwana Lucas Ndanga wa kwanza na Kaimu Mhariri wa Morogoro Bwana Jems Tem wakiwa katika kuandika habari.
Baandaa ya kuchambua na kuandika habari hizo zimepelekwa kwenye Computer kwa Lyaout ambapo Dada Oliva kato akiwa kwenye Computer,Mratibu Msaidizi Bwana Ntambi Buyanzu,akisoma kwa masahihisho ambapoElizabeth Pangras mwenye bauni lenye maua akihakiki.
Wahudumu wa Hotel hii wakiwa tayari kwa mahanjumati kwa wanahabari hao baada ya kazi maalumu
Hapa na mie nikiwa na wanahabari wenzangu tukitoka Arine Inn kuelekea tulikofikia hapa Mjini morogoro

Thursday, April 14, 2011
WANANCHI WA MKOA WA RUVUMA WAMEPOTEZA TUMAINI YA KUONA SOKA TENA
Wapenzi wa soka wa ndani na nje ya mkoa wa Ruvuma wamepoteza tumaini ya kuona soka katika uwanja wa majimaji ( Wa- na lizombe ) baada ya Timu hiyo kushuka daraja.
Sijui alaumiwe nani katika kushuka Daraja Timu ya Majimaji,Ulaumiwe uongozi wa serikali ya mkoa?,wanaoongoza timu hiyo?,usajili mbaya wa wachezaji?,huduma mbovu kwa wachezaji hao?.hakuna wafadhili wa timu hiyo?.
Hebu wenzetu walio nje ya mkoa wa Ruvuma wenye uwezo kusaidia timu hiyo ili kurudisha hadhi yake kama miaka ya 70.
Wednesday, April 13, 2011
HONGERA SERIKALI YA MKOA WA MOROGORO KUJENGA SEKONDARI YA UKUMBOSHO WA SOKOINE
Naipongeza Serikali ya mkoa wa Morogoro kushirikiana na Wilaya ya Mvomero kuandaa Bilioni 12 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari itakayo pewa jina la Sokoine Memorial High Secondary School eneo alilofia aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine Wami Ruhinda.
Cha ajabu na cha kushangaza kuna baadhi ya viongozi mashuhuri katika mikoa fulani walionyesha juhudi zao katika uongozi na Mungu amewaita mbele za haki hawakufanyiwa kama ilivyo fanya Serikali ya Mkoa wa Morogoro.
Mfano mzuri na rahisi sana, Aliyekuwa Mbunge wa Songea Mjini Hayati Raurence Mtazama Gama ,Alifanya mambo mengi ya maendeleo katika mkoa wa Ruvuma,hadi leo wanasua sua kumpatia kitu chochote jina kama kumbu kumbu Mzee Gama.
Kuna shule ya sekondari inayojengwa Wilaya ya Namtumbo ya kidato cha tano na sita inayojengwa kwa ushirikiano wa wilaya zote za mkoa wa Ruvuma,Afisa Elimu wa mkoa huo alipendekeza sekondari hiyo iitwe Jina la Gama kumuenzi kutokana na juhudi alizozionyesha wakati alivyo kuwa mkuu wa mkoa huo,kilicho tokea huwezi kuamini baadhi ya wabunge alikataa kata kata kupewa sekondari hiyi jina la Gama. Makubwa wenyewe kwa wenyewe wanakataana.
DUNIANI KUNA MAMBO KWELI JAMANI TOKA LINI MAREHEMU ANAPOKEA MISHAHARA ?
Ukaguzi wa mahesabu ya fedha za serikali imebaini Halmashuri zetu zimejihusisha na malipo hewa.Malipo yaliyolipwa ni ya mishahara.Kinacho shangaza na haiingii akilini ya kumlipa mshahara marehemu.Inamana marehemu hao wanatoka kaburini kwenda benki kuchukua fedha?
Lakini kila mwaka watumishi wa Umma wanajaza fomu za kuhakikisha au kuhakiki malipo ya mishahara hewa,inamana Halmashauri hizo zilizokubwa na ulipaji mishahara hewa, huwa wanapeleka wapi fomu za uhakiki wa malipo hewa ya mishahara?
KUMBE SOKWE NAO WANA UTAWLA?
Hifadhi ya Taifa ya Gombe ni kivutio kikubwa sana kwa watalii,Hifadhi hiyo ina Sokwe ambao wana utawala wa kuachiana.Kwa mujibu wa wakuu wa hifadhi hiyo ni kwamba kiongozi wa sasa wa Sokwe hao ni mkali sana.Inasemekana kuwa aliwahi kujamiiana na mama yake hivyo aliugua sana.
Aidha sokwe akiugua wanatabia ya kujitafutia dawa ya majani au mizizi,wakitumia dawa hizo wanapona.Sokwe hao wanapenda kuwa karibu na binadamu.Karibu Tanzania ukajionee maajabu ya vivutio mbalimbali.
Subscribe to:
Posts (Atom)