Saturday, January 15, 2011

UPEPO MKALI ULIYOEZUA MAJUMBA YA WATU SONGEA MWAKA JANA, ULIPUTUPA MABLI MADISHI YA TV YA WATU LIKIWEPO NA LA TUJIFUNZE KUSINI

Fundi Gama mtaalamu wa kuweka TV Dish katika Manispaa ya Songea,akitafuta Channels katika Dish la TUJIFUNZE KUSINI baada ya Kurushwa na upepo mkali mwaka naja.aliyesimama karibu naye ni Second master wa Sekondari Lizaboni,na aliyevaa koti akiwaangalia ni Mhariri wa Msaidizi Bwana Juma Nyumayo  wa TUJIFUNZE KUSINI akishuhudia utaalamu wa mafundi hao,pia ni watumishi wa Umma.

Thursday, January 13, 2011

HOSPITAL YA MKOA SONGEA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MADAKTARI BINGWA


HOSPITAL ya mkoa Songea inakabiliwa na upungufu wa madaktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi na upasuaji,watoto,( Physician ),wa magojwa ya akili,na wahuduma za mionzi.

Mganga mkuu wa hospital hiyo, Dr. Daniel Malekela,amesema hayo alipotembelewa na mwandishi wa Blog hii ofisini kwake leo hii,kuwa ni pamoja na madaktari wa kawaida wanao hitajika kulingana na taasisi hii ilivyo kubwa.

Wednesday, January 12, 2011

SHEREHE ZA MIAKA 47 YA MAPIDUZI ZANZIBAR WAFUNGWA 33 WASAMEHEWA KATI YAO MWANAMKE MMOJA

Rais Dr Ally Mohamed Shen wa Zanzibar amewasamehe wafungwa 33 kati yao mmoja ni mfungwa wa kike.Waliosamehewa kifungo ni  pamoja na wazee na wenye magonjwa mbalimbali.wakati wa maazimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

MWENYE MACHO HAMBIWI TAZAMA,,JINSI MIUNDOMBINU ILIVYO BORESHWA NCHINI

Huo ni mfano tu mmojawapo wa jinsi serikali ya Awamu ya nne ilivyo boresha miundombinu yake,hapo unapopandisha kuingia Iringa mjini kwa bas,lori gari digo,pikipiki baiskeli au kwa miguu.Tunategemea na barabara ya masasi,Tunduru hadi Mbamba Bay itakuwa hivyo Mhe Magufuli alione hilo Kusini  wananchi wanapenda kuona barabara za lami kama wanavyo faidika wananchi wa kaskazini peke yao.

MONKEYS IN MIKUMI NATIONAL PARK MOROGORO REGION TANZANIA ARE INTERESTED ANIMALS


This monkey knows that in bus or lorries he can get something to eat such as ,bananas, mangos, chocolates, loaf of bread  from the passengers or drivers.

Once bus or lorry passing  through, this monkey run after it looking  something to eat, you can find such monkeys also in Ruwaha,Kitonga, my dear  I would like to invite you one day to see how this animals behave like man.  

Monday, January 10, 2011

WAHADHIRI NA WANACHUO UDOM WAGOMA KUDAI POSHO NA MASLAHI

Hivyo migomo ndiyo njia pekee ya usuluhisho wa kupata haki za watu?,katika taasisi za serikali au taasisi binafsi?,Ifike mahali sasa Serikali na vyombo vyake kukaa chini na kutafuta vyanzo vya migomo,na kulitafutia suluhisho.Mgomo wa UDOM ni wa pili ukifuatiwa na huu wa sasa.wanafunzi wa Kitovu cha Social waligoma kudai fedha za Field nasikaia Serikali ikawalipa.

Kwa mtindo huo,hata Wahadhiri nao wameamua  kuungana na  wanachuo ambao wanamadai mbalimbali ili walipwe  stahili  zao au madai yao. Kama ndivyo kwanini  Serikali na vyombo vyake vingojee migomo ndipo malipo yafanyike? Sijui  wewe na mimi  tunalionaje jambo hili?.litaendelea hadi lini? Ni nani alaumiwe wahadhiri,wanachuo ama Serikali?

Sunday, January 2, 2011

SALAMU ZA MWAKA MPYA WA 2011 KWA WATANZANIA RAIS KIKWETE ATARAJIA KUUNDA TUME YA KATIBA YA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakayaa  Kikwete,anatarajia kuunda tume ya marekebisho ya Katiba ya Tanzania, ambayo wadau mbalimbali wa vyama vya siasa,wasomi ,wananchi wote wenye mawazo yenye kuleta mshikamano wa pamoja wa kulieta maendeleo ya taifa,siku alipowatakia wananchi Heri ya mwaka mpya wa 2011.

Alisema kuwa jambo hilo ni jema,ila ilahitaji busara ya hali ya juu katika kupata Katiba,alisema hakuna haja ya malumbano,bali kila mwananchi anahitajika kuchangia mawazo yake,kulingana na mahitaji ya jambo lenyewe..