Mheshimiwa Mizengo kayanza Pinda ( Mbunge ) wa Katavi apishwa kuwa waziri Mkuu wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chamwino Ikuli nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma ,wakati wabunge wa Chama cha CHADEMA hawakuonekana katika sherehe hizo,Swali hawakualikwa,ama wametekeleza kauli ya aliyekuwa akitaka kiti cha Urais kushindwa Dkt Slaa Kutomtambua Kikwete kama ndivyo tuwaelewe vipi?.wewe na mimi tutafakkari,Je shughuli za kuapishwa waziri Mkuu hazikufanikiwa,na Rais Jakaya Kikwete hawezi kuhutubia Bunge la kumi la mwaka 2010 kwa kuwa wabunge wa CHADEMA wamesusia,Ni aibu kwa wapenda amani,pia ni mashaka kwa wale waliojenga imani kuwa ni chama kitakacho tawala nchi hapo baadaye.Lakini kama ilikuwa babahati yako ya kuwa Rais subira ni muhimu.Mheshimiwa Mizengo Pinda akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete Chamwino Ikulu Dodoma Leo
Thursday, November 18, 2010
Dkt Slaa kutomtambua Rais Kikwete kunazua maswali mengi miongoni mwa watanzania
Dkt Slaa wa CHADEMA katika Hekaheka za kutafuata Urais wa Tanzania 2010 ( Source Christian Sikapundwa)
KUFUATIA kauli ya Dkt Wilbroad Slaa ya kutomtambua Rais wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete,kunazua maswali mengi kwa baadhi ya watanzania wenye akili sawasawa, wenye kujua asiyekubali kushindwa si mshindani.
Kwa mujibu wa kauli hiyo wabunge wa chama chake cha CHADEMA nao bila kujua, kwa makusudi, kuwa waliapa mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda kuwa watakuwa waaminifu, watailinda,wataitete katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumalizia kusema Mungu awasaidie.
Lakini cha ajabu haohao waliosema hivyo, kwa kufuata kauli ya Slaa asiyekubali kushindwa na kutomtambua Rais Kikwete,leo wamekataa kushiriki kuapishwa kwa waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Mizengo Pinda, katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma.
Zaidi ya hayo wanaendelea kuwa watasusia hotuba ya Mhe.Rais Kikwete, itakayo tolewa leo moja kwa moja na Vyombo vya habari, kufuatia kauli ya Rais wao Dkt Slaa, aliyeshindwa kuwa Rais halali wa nchi hii, hivyo wanataka wananchi na jamii ya kimataifa ambayo ilithibitishiwa na watazamaji wa ndani na nje wakiwemo TEMCO, SADC,EAC,EU, UN kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wahaki. CHADEMA wanataka kujenga Tanzania ya namna gani?.
Wananchi wanaanza kuwa na maswali mengi kufuatia uamuzi wa wabunge hao kati yao ni wasomi, hivyo hao wamesoma vyuo gani ambako hawakujifunza Saikolojia,Lojiki ya mambo yanavyo kwenda katika ulimwengu huu.
Kuchaguliwa au kutochaguliwa ni matakwa ya yule atakaye kukuchagua au kutokuchagua,hivyo hayo hawayajui? au mradi kuuonyesha ulimwengu kuwa wao wanaweza kususia,hivyo ni wote walikubaliana au ni ‘msafala wa mamba na kenge nao wapo’.
Kama utafanikiwa kusoma Blog hii, jaribu kumrudia Mungu wako na kusema Eee Mungu nisamehe,na urudi Tanzania maana ninyi tunakuwa na mashaka nanyi,mnaelekea kubaya,wale wenzenu wamezoea,wamekulia katika hekeheka za kutengena na familia zao,kwetu ni jambo geni linahitaji maandalizi ya kutosha.
Watanzania hawajui, na hao wafuasi ambao wanawashabikia si lolote,hawana mbinu za kujihami,kutokana na hali zao zilivyo,tusipoteze amani na utulivu tuliouzoea, Baadhi ya nchi duniani zimekubaliana na matokeo uchaguzi 2010 na sheria,kanuni na taratibu zilizotawala uchaguzi huo zilifutwa ikiwa ni pamoja na kandaa uwanja sawa wa ushindani hapakuwa na malalamiko.
Hivyo hao waliosusia kuapishwa Waziri Mkuu Pinda,na baadaye kususia hotuba ya Rais Bungeni hapo baadaye,wataingia tena katika Mjengo wa Bunge? kuendelea na vikao vyake,wenyewe wanajionjaje kwa wenzao? Wabunge wenzao wa chama Tawala CCM na kambi vyingine za upinzani ambao si CHADEMA nao wanawaonaje? Jamii ya watanzania wanawaonaje? bado watakuwa na imani na chama hicho ( CHADEMA )
Tuesday, November 16, 2010
WAZIRI MKUU MIZENGO KAYANZA PETER PINDA ATHIBITISHWA KWA KURA 277 SAWA NA ASILIMIA 84.5 ZILIZOPIGWA NA WABUNGE WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda mbunge wa Jimbo la katavi amethibitishwa kwa Waziri Mkuu kwa kupigiwa kura na wabunge 328,ambapo kura zilizoharibika ni 2 sawa na asilimia 0.6,waliosema hapana 49 sawa na asilimia 4.9 na waliosema ndio ni 277 sawa na asilimia 84.5
Baada ya kuthibitishwa kwake Mhe.Pinga alimshukuru Mungu ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wahehsimiwa Wabunge kwa kuthibitisha kuwa Waziri Mkuu,aidha alisema kuwa atakuwa Waziri mkuu wa wabunge wote,waliomkataa na waliomkubali kwa lengo la kumsaidia mwananchi.
Alisema kuwa kweli yeye ni mtoto wa mkulima hivyo ameomba ushirikiano mkubwa na wabunge wote wakulenga mkulima,mfugaji,mvuvi na mrina asali,hata kukiwa na malumbano lakini yawe yana lenga kumtetea mwananchi mkulima.
Saturday, November 13, 2010
MKOA WA RUVUMA WAPOTEZA MRATIBU WA KIFUA KIKUU NA UKOMA BWANA RENE JOSEPH LEOPOLD MWIKWA BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MREFU KWA TATIZO LA KISUKARI NA MOYO
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU RENE JOSEPH LEOPOLD MWIKWA MRATIBU WA KIFUA KIKUKU NA UKOMA HOSPITAL YA MKOA WA RUVUMA ALIYEFARIKI TAREHE 12/11/2010 SAA 9 ALASIRI.
Alizaliwa tarehe 01/3/1952 Kidodi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro,akapata elimu ya msingi Lumango Luhembe kidodi.Hatimaye alipata elimu ya Sekondari nchini Uganda kidato cha kwanza hadi cha tatu,machafuko ya kisiasa yalivyoanza nchini Uganda ,Marehemu alirudi Tanzania .
Alivyorudi Tanzania alijiunga na chuo cha waganga wasaidizi ( watabibu ) Wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro,baada ya mafunzo hayo alipelekwa kuanza kazi ya ugnaga Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma mwaka 1976 ambapo alifanya kazi kwa muda mfupi.
Mwaka 1979 alihamishiwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambapo mwaka 1980 alikwenda kwa masomo ya stashahada chuo cha uganga Bumbuli Tanga mwaka 1982 alihitimu mafunzo yake na kurudi hosipitali ya mkoa wa Ruvuma kama Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma hadi mwka 2006.
Mwaka alianza kupata tatizo la kisukari na moyo,ambapo tarehe 26/12/2006 tatizo likazidi kuwa kubwa na akaendelea kuugua hadi tarehe 12/11/2010 saa 9 alasiri Mratibu Mwikwa akafariki katika hospitali ya mkoa ya Songea,Na mazishi yatafanyika tarehe 15/11/2010 Mjimweme katika manispaa ya Songea,ambako familia yake inaishi hapo.Marehemu ameacha mke na watoto kadhaa.
Atakumbukwa na watu wengi kwa utendaji wake wa kazi ambao haukuwa na mpaka,hakujali umbali wala unyanyapaa wa aina yoyote.Alikuwa mwepesi wa kutoa ushauri na kutoa msaada kwa wagonjwa wake,alikuwa mcheshi,mwingi wa tabasamu,na maneno ya kumtia mgonjwa faraja.Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi.
Friday, November 12, 2010
SPIKA WA KWANZA MWANAMKE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE.ANNE SHEMAMBA MAKINDA WA CCM ALIYE PATA KURA 265 SAWA NA ASILIMIA 74.2 AMEANZA KAZI YA KUAPISHA WA BUNGE MARA BAADA YA KUTANGAZWA KWAKE MJINI DODOMA LEO TAREHE 12/11/2010
Mheshimiwa Samwel John Sitta Spika aliyestaafu akimkimbatia Mhe. Anne Shemamba Makinda Spika wa CCM aliyechaguliwa na wabunge hao kwa kupata kura 265. sawa na asilimia 74.2 na kumshinda Mgombea wa nafasi hiyo Bwana Mabere Nyauchi Marando wa CHADEMA kwa kura 53 sawa na asilimia 16.2.Baada ya Mhe.Sitta kuaapa kuwa atahifadhi,atailinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Tanzania iliyowekwa..
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungaqno wa Tanzania aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo Mhe. Anne Shemamba Makinda akipeana mikono na Mhe.John Momose Cheyo baada ya kuapa kuwa atakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Rashid Ally Abdalah akipeana mikono na Spika wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anne Shemamba Makinda baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge hilo na kuahidi kuwa ataendesha Bunge hilo kwa kanuni za Bunge zilizo wekwa kwa mujibu bila upendeleo.
Saturday, November 6, 2010
DOKTA JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEAPISHWA LEO KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO IJAYO
Baada ya kuapishwa Rais na Makamu wa Rais waliombewa Duwa na madhehebu ya kidini ili kuwaombea waongoze kwa amani na utulivu.Kisha alikaribishwa kuwahutubia wananchi alisema hawezi kusema mengi,mengi atasema siku ya kuhutubua Bunge siku chache zijazo.
Ametoa shukurani kwa Mungu,na wananchi kuchagua CCM kwa kuona jinsi walivyo jiandaa kulitumikia taifa.Alisema watembeeni kifua mbele kwani watanazia bado wanaipenda CCM,pia alimshukuru Makamu wa Rais na mke wake kwa kumsaidia katika kufanikisha azima ya kuwa Rais.
Aidha alisema hakuweza kusahau viongozi wa vyama vya siasa vilivyotoa hamasa kubwa kwa CCM,Alisema uchaguzi umepita sasa watu wagange yajayo.Katika baadhi ya maeneo kulipandikizwa sumu mbaya ya kuwagawa watanzania aliomba yaachwe hayo.
Alisema watanzania wasiaharibu sifa ya Tanzania ya amani na utulivu kwa lengo la kupata madaraka.pia aliwapongeza Tume ya Uchaguzi jinsi ilivyo fanikisha uchaguzi huu uluyopita,vyombo vya usalama na vyombo vya habari .
Ametoa shukurani kwa Mungu,na wananchi kuchagua CCM kwa kuona jinsi walivyo jiandaa kulitumikia taifa.Alisema watembeeni kifua mbele kwani watanazia bado wanaipenda CCM,pia alimshukuru Makamu wa Rais na mke wake kwa kumsaidia katika kufanikisha azima ya kuwa Rais.
Aidha alisema hakuweza kusahau viongozi wa vyama vya siasa vilivyotoa hamasa kubwa kwa CCM,Alisema uchaguzi umepita sasa watu wagange yajayo.Katika baadhi ya maeneo kulipandikizwa sumu mbaya ya kuwagawa watanzania aliomba yaachwe hayo.
Alisema watanzania wasiaharibu sifa ya Tanzania ya amani na utulivu kwa lengo la kupata madaraka.pia aliwapongeza Tume ya Uchaguzi jinsi ilivyo fanikisha uchaguzi huu uluyopita,vyombo vya usalama na vyombo vya habari .
Friday, November 5, 2010
DOKTA JAKAYA KIKWETE ATANGAZWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BAADA YA KUPATA ASILIMIA 61.17
Dokta Jakaya Kikwete atangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kushinda kwa asilimia 61.17,akifuatiwa na Dokta Willbroad Slaa wa CHADEMA kwa asilimia 26.34 na hakufika kwenye matangazo hayo,ambapo mshidi wa tatu ni Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata asilimia 8,06.
Profesa Lipumba alimpongeza Dokta Kikwete kwa ushindi aliyoupata na kumpatia Ilani ya CUF isaidie kuleta Demokrasia nchini,katika ahadi kadhaa zilizo ahidiwa wakati wa kuwaomba wanachi ridhaa ya kuiongoza nchi.kama vile ajila kwa vijana,kuboresha elimu,miundombinu na ustawi wa jamii.
Dkt Kikwete kawashukuru watanzania wote kwa kuichagua CCM,Tume ya Uchaguzi,Vyombo vya habari kwa mchango wao,Wangalizi wa Uchaguzi,na kuwaeleza wananchi kuwa uchaguzi umepita kwa utulivu na Amani.
Profesa Lipumba alimpongeza Dokta Kikwete kwa ushindi aliyoupata na kumpatia Ilani ya CUF isaidie kuleta Demokrasia nchini,katika ahadi kadhaa zilizo ahidiwa wakati wa kuwaomba wanachi ridhaa ya kuiongoza nchi.kama vile ajila kwa vijana,kuboresha elimu,miundombinu na ustawi wa jamii.
Dkt Kikwete kawashukuru watanzania wote kwa kuichagua CCM,Tume ya Uchaguzi,Vyombo vya habari kwa mchango wao,Wangalizi wa Uchaguzi,na kuwaeleza wananchi kuwa uchaguzi umepita kwa utulivu na Amani.
Subscribe to:
Posts (Atom)





