Tuesday, November 16, 2010

WAZIRI MKUU MIZENGO KAYANZA PETER PINDA ATHIBITISHWA KWA KURA 277 SAWA NA ASILIMIA 84.5 ZILIZOPIGWA NA WABUNGE WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda mbunge wa Jimbo la katavi amethibitishwa  kwa Waziri Mkuu kwa kupigiwa kura na wabunge 328,ambapo kura zilizoharibika ni 2 sawa na asilimia 0.6,waliosema hapana 49 sawa na asilimia 4.9 na waliosema ndio ni 277 sawa na asilimia 84.5

Baada ya kuthibitishwa kwake Mhe.Pinga alimshukuru Mungu ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wahehsimiwa Wabunge kwa kuthibitisha kuwa Waziri Mkuu,aidha alisema kuwa atakuwa Waziri mkuu wa wabunge wote,waliomkataa na waliomkubali kwa lengo la kumsaidia mwananchi.

Alisema kuwa kweli yeye ni mtoto wa mkulima hivyo ameomba ushirikiano mkubwa na wabunge wote wakulenga mkulima,mfugaji,mvuvi na mrina asali,hata kukiwa na malumbano lakini yawe yana lenga  kumtetea mwananchi mkulima.


Saturday, November 13, 2010

MKOA WA RUVUMA WAPOTEZA MRATIBU WA KIFUA KIKUU NA UKOMA BWANA RENE JOSEPH LEOPOLD MWIKWA BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MREFU KWA TATIZO LA KISUKARI NA MOYO


HISTORIA FUPI YA MAREHEMU RENE JOSEPH LEOPOLD MWIKWA MRATIBU WA KIFUA KIKUKU NA UKOMA HOSPITAL YA MKOA WA RUVUMA ALIYEFARIKI TAREHE 12/11/2010 SAA 9 ALASIRI.

Alizaliwa tarehe 01/3/1952 Kidodi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro,akapata elimu ya msingi Lumango Luhembe kidodi.Hatimaye alipata elimu ya Sekondari nchini Uganda kidato cha kwanza hadi cha tatu,machafuko ya kisiasa yalivyoanza nchini Uganda,Marehemu alirudi Tanzania.

Alivyorudi Tanzania alijiunga na chuo cha waganga wasaidizi ( watabibu ) Wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro,baada ya mafunzo hayo alipelekwa kuanza kazi ya ugnaga Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma mwaka 1976 ambapo alifanya kazi kwa muda mfupi.

Mwaka 1979 alihamishiwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambapo mwaka 1980 alikwenda kwa masomo ya stashahada  chuo cha uganga Bumbuli  Tanga mwaka 1982 alihitimu mafunzo yake na kurudi hosipitali ya mkoa wa Ruvuma kama Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma hadi mwka 2006.

Mwaka alianza kupata tatizo la kisukari na moyo,ambapo tarehe 26/12/2006 tatizo likazidi kuwa kubwa na akaendelea kuugua hadi tarehe 12/11/2010 saa 9 alasiri Mratibu Mwikwa akafariki katika hospitali ya mkoa ya Songea,Na mazishi yatafanyika tarehe 15/11/2010 Mjimweme katika manispaa ya Songea,ambako  familia yake inaishi hapo.Marehemu ameacha mke na watoto kadhaa.

Atakumbukwa na watu wengi kwa utendaji wake wa kazi ambao haukuwa na mpaka,hakujali umbali wala unyanyapaa wa aina yoyote.Alikuwa mwepesi wa kutoa ushauri na kutoa msaada kwa wagonjwa wake,alikuwa mcheshi,mwingi wa tabasamu,na maneno ya kumtia mgonjwa faraja.Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi.

Friday, November 12, 2010

SPIKA WA KWANZA MWANAMKE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE.ANNE SHEMAMBA MAKINDA WA CCM ALIYE PATA KURA 265 SAWA NA ASILIMIA 74.2 AMEANZA KAZI YA KUAPISHA WA BUNGE MARA BAADA YA KUTANGAZWA KWAKE MJINI DODOMA LEO TAREHE 12/11/2010

 Mheshimiwa Samwel John Sitta  Spika aliyestaafu akimkimbatia Mhe. Anne Shemamba Makinda Spika wa CCM  aliyechaguliwa na wabunge hao kwa kupata kura 265. sawa na asilimia 74.2 na kumshinda Mgombea wa  nafasi hiyo Bwana Mabere Nyauchi Marando wa CHADEMA  kwa kura 53 sawa na asilimia 16.2.Baada ya Mhe.Sitta kuaapa kuwa atahifadhi,atailinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Tanzania iliyowekwa..
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungaqno wa Tanzania aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo Mhe. Anne Shemamba Makinda akipeana mikono na Mhe.John Momose Cheyo baada ya kuapa kuwa atakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Rashid Ally Abdalah akipeana mikono na Spika wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anne Shemamba Makinda baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge hilo na kuahidi kuwa ataendesha Bunge hilo kwa kanuni za Bunge zilizo wekwa kwa mujibu  bila upendeleo.

Saturday, November 6, 2010

DOKTA JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEAPISHWA LEO KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO IJAYO

Baada ya kuapishwa Rais na Makamu wa Rais waliombewa Duwa na madhehebu ya kidini ili kuwaombea waongoze kwa amani na utulivu.Kisha alikaribishwa kuwahutubia wananchi alisema hawezi kusema mengi,mengi atasema siku ya kuhutubua Bunge siku chache zijazo.

Ametoa shukurani kwa Mungu,na wananchi kuchagua CCM kwa kuona jinsi walivyo jiandaa kulitumikia taifa.Alisema watembeeni kifua mbele kwani watanazia bado wanaipenda CCM,pia alimshukuru Makamu wa Rais na mke wake kwa kumsaidia katika kufanikisha azima ya kuwa Rais.

Aidha alisema hakuweza kusahau viongozi wa vyama vya siasa vilivyotoa hamasa kubwa kwa CCM,Alisema uchaguzi umepita sasa watu wagange yajayo.Katika baadhi ya maeneo kulipandikizwa sumu mbaya ya kuwagawa watanzania  aliomba yaachwe hayo.


Alisema  watanzania wasiaharibu sifa ya Tanzania ya amani na utulivu kwa lengo la kupata madaraka.pia aliwapongeza Tume ya Uchaguzi jinsi ilivyo fanikisha uchaguzi huu uluyopita,vyombo vya usalama na vyombo vya habari .

Friday, November 5, 2010

DOKTA JAKAYA KIKWETE ATANGAZWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BAADA YA KUPATA ASILIMIA 61.17

Dokta Jakaya Kikwete atangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kushinda kwa asilimia 61.17,akifuatiwa na Dokta Willbroad Slaa wa CHADEMA kwa asilimia 26.34 na hakufika kwenye matangazo hayo,ambapo mshidi wa tatu ni Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata asilimia 8,06.

Profesa Lipumba alimpongeza Dokta Kikwete kwa ushindi aliyoupata na kumpatia Ilani ya CUF isaidie kuleta Demokrasia nchini,katika ahadi kadhaa zilizo ahidiwa wakati wa kuwaomba wanachi ridhaa ya kuiongoza nchi.kama vile ajila kwa vijana,kuboresha elimu,miundombinu na ustawi wa jamii.

Dkt Kikwete kawashukuru watanzania wote kwa kuichagua CCM,Tume ya Uchaguzi,Vyombo vya habari kwa mchango wao,Wangalizi wa Uchaguzi,na kuwaeleza wananchi kuwa uchaguzi umepita kwa utulivu na Amani.

WABUNGE WA MKOA WA RUVUMA WA CCM WAMO NDANI YA BUNGE BAADA YA KUSHINDA KATIKA MAJIMBO YAO,CHADEME YAPATA VITI VYA UDIWANI JIMBO LA SONGEA MJINI UBUNGE DOKTA EMANUEL NCHIMBI ABWAGA WA CHADEMA

Dokta Emanuel Nchimbi atetea kiti chake cha Ubunge katika jimbo lake la Songea Mjini baada ya kumshinda mpinzani wake Advocate Mbogolo wa CHADEMA aliyewania nafasi hiyo kwa mara nne sasa na kuambulia patupu,asikate tamaa ipo siku ndoto yake itakamilika ya kuingia Jengo la Bunge la Jamhuri ya Tanzania ( Picha na Christian Sikapundwa)

Thursday, November 4, 2010

LEONI LEO KIKWETE,LIPUMBA AU SLAA !! KUKAMILISHA NDOTO YA KUINGIA IKULU BAADAYE LEO IJUMAA YA TAREHE 5 NOVEMBA 2010 KUWA RAIS WA TANZANIA KWA MIAKA MITANO IJAYO

Pamoja na kumaliza hekaheka za kampeni za Urais Ubunge na Udiwani ikaingia ngwe nyingine ya upigaji wa kura tarehe 31.10.31 2010 ulikamilika kwa Amani na Utulivu mkubwa,wananchi walitimiza haki yao ya msingi kumchagua kiongozi wanaye mtaka.

Ikaingia hatua ya mwisho ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo,ambapo vyama vyilivyo ng'ara kwenye majimbo mengi katika nafasi za Ubunge na Udiwani vimeibuka kuwa washindi ,na matokeo ya nafasi ya Urais yameendelea kutangazwa na leo ndiyo atangazwa mshindi kwa nafasi ya Urais kulingana na uwingi wa majimbo aliyopata ushindi na kujumuisha  matoke.Na kuibuka kidedea leo.

Vyama vilivyoingia katika kinyang'anyiro vilivyo shindwa vikubali matokeo,kukataa matokeo bila kufanya utafiti wa kutosha kwa wapiga kura wako,ni kushangaza watu.kushinda au kushindwa ni katokeo ya idadi ya wapiga kura waliyo kukubali au kukukataa.Na si rahisi kung'amua ni nani aliye nikubali au kukukataa kwa kuwa ilikuwa ni siri ya mpiga kura kwenye visanduku.

Lakini pia kushinda au kushndwa kusichukulie uwingi wa watu waliyojitokeza siku mgombea alipokwenda kunadi sera za chama chake,watu wanaweza wakawa wengi lakini siku ya kupiga kura wasiwe wengi au wakawa wengi lakini hawa kuwa na shahada ama walikuwa na shahada hawa kwenda kupiga kura yote yanawezekana kwa Binadamu.

Aidha cha msingi Tume ya Uchaguzi irekebishe utaratibu wa kuchelewesha kutangaza matokeo,ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo kuna sababisha maswali mengi kwa wapiga kura wenyewe,wanacha wa vyama mbalimbali na wagombea wenyewe,kwanini yanacheleweshwa.Matokeo yakitangazwa mapema yatapunguza malalamiko ya wapigiwa kura ya kuchakachuliwa kura zake.