Tuesday, January 13, 2015

BREAKING NEWS MIAKA 51 ZANZIBAR ELIMU YA MSINGI BURE , MITIHANI KIDATO CHA NNE NA SITA HAKUNA KUCHANGIA

Katika hotuba yake iliyodumu kwa muda wa saa 1.05 Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. All Mohamed Shein, alisema katika miaka 51 ya Mapinduzi Zanzibar kuna maendeleo makubwa yaliyopatikana yakiwemo miundo mbinu mbalimbali.,kilimo na shughuli kadhaa za maendeleo zimepatikana

Aidha alisema kuwa zao la karafuu limezidi kuwa na thamani ambapo kilo moja ya karafuu ni shilingi 16,000. kwa sasa na katika Sekta ya afya jengo la upasuaji kichwa na uti wa mgongo limekamilika ambalo litasaidia sana kwa wagonjwa wa aina hiyo kupata huduma hiyo  kwa haraka.Na kwamba wazee watapata huduma ya afya bila kuchangia huduma za matibabu.

Pia amesema katika Sekta ya Elimu imeboreka kwa kuwa na walimu wa kutosha ingawa kuna idadi ndogo inahitajika kutimiza lengo lakini idadi iliyoko inakidhi mahitaji, vyumba vya madarasa na maabara pamoja na vifaa vya kufundishia na kujifunzia vikiwemo vitabu vipo ya kutosha, ambapo ametangaza rasmi katika kumalizia hotuba yake kuwa katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 elimu ya msingi itakuwa bure na kwamba michango ya mitihani kwa vidato vya nne na sita haitakuwepo.
 

 Alisema kuwa maelezo mengine kuhusu Sekta hiyo itajulikana baadaye,Sherehe ya miaka 51 ya Mapinduzi Zanzibar ilipambwa kwa halaiki,Vikosi ya Ulinzi na Usalama na Burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili pamoja na muziki wa kizazi kipya na burudani kibao.