Saturday, September 27, 2014

VIPEPERUSHI VYA KUTISHIA WANANCHI NA WAJUMBE WA BUNGE MAALUMU VYA SAMBAZWA NA WATU WASIYO JULIKANA KATIKA MANISPAA YA DODOMA JANA VYEYE VICHWA VYA HABARI OFAUTI

Hapa ni eneo la Bohari Mkoa wa Dodoma ambapo kuna ulinzi mkali wa polisi kwa ajili ya kuzuia  maandamano kuelekea Viwanja wa Bunge kusababisha vurugu.

Baadhi ya vipeperushi hivyo kilicho patikana na Blog hii inasema." ONYO Dodoma si mahali pa kufuga wezi wa fedha za Umma.Utakayeingia Bungeni kuanzia kesho,yatakayo kupata utajuta" mwisho wa kunukuu. Hivyo  vilisambazwa jana.
Lakini ilikuwa ni kelele za mlango,wajumbe wa Bunge Maalumu waliendelea na shughuli zao kama kawaida na hakuna chochote kilicho tokea kifuatia vipeperushi hivyo.

Thursday, September 18, 2014

VIJANA WANASEMA MAANDAMANO HAYANA NAFASI KWAO KWA KUWA HAYATAWASAIDIA KWENYE KUTATUA MATATIZO YAO YA AJIRA

 Vijana wa hawa wanawashangaa UKAWA ambao walitaka kufanya maandamano kuelekea Bungeni hapa Dodoma.Vijana hawa wamejiajiri katika uuzaji wa matunda
Huyu Kijana na mwenyekiti wa Bodaboda katika manispaa ya Dodoma akielekea kijiweni kwao.Ambapo hawa wamejiajiri kwenye bodaboda.

 Matunda nayo ni muhimu ambayo yamekuwa ni ajira kwa vijana

Kijana huyu amejiajiri na hapa yupo ofisini kwake.

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOANI DODOMA IMEWEKA ULINZI KUZUNGUKA MAENEO YANAYO ZUNGUKA MAJENGO YA BUNGE YALIKUWA NA ULINZI MKALI KUFUATIA MAANDAMANO YA UKAWA YALIYOTARAJIWA KUFANYIKA LEO MJINI HAPA.

 Barabara zinazo pita jirani na majengo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo zili zungushiwa Utepe wa njano na askari polisi wakiwa na magari yao,askali wenye farasi, wenye mbwa walionekana wakiwa kwenye maeneo hayo.

Hayo yametokea kufuatia maandamano ya UKAWA yaliyotarajiwa kufanyika mjini hapa hapa.
Baadhi ya wananchi walibaki wakishangaa na kusubiri wayaone maandamano hayo ambayo walitarajia kuzunguka mnara wa Bohari na stendi ya mabasi,lakini mpaka saa moja usiku hakuna maandamano yaliyojiokeza hapa Bohari.
Wakati wengene wakijiandaa na maandamano katika mzunguko wa mnara huu,vijana hawa walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kujitafutia riziki na familia zao.

Tuesday, September 16, 2014

FREEMAN MBOWE ASHINDA KWA KISHINDO NAFASI YA UWENYEKITI WA CHAMA CHA CHADEMA KATIKA MKUTANO MKUU WA CHAMA HICHO ,NA KUTOA TAMKO LA MGOMO USIO NA KIKOMO KWA TAIFA LOTE IWAPO BUNGE MAALUMU KA KATIBA LITAENDELEA KUJADILI RASIMU ZA KATIBA HIYO

Mheshimiwa Freeman Mbowe amepata ushindi wa kishindo kufuatia uchaguzi wa nafasi ya uenyekiti kwenye Chama chake cha CHADEMA katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Jijijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Aidha baada ya uchaguzi huo Mhe. Mbowe alitoa tamko la maandamano yasiyo na kikomo kwa nchi nzima ,iwapo Bunge Maalumu la Katiba litaendelea kujadili Rasimu ya Katiba hiyo kwa madai kuwa kuendelea na mjadala wa Rasimu ya Katiba ni kuhujumu fedha za watanzania.

Wachambuzi wa mambo wasio wababaishaji wanahoji,Mhe.Mbowe alikuwa wapi kupinga Bunge hilo lisiendelee wakati lilipo anza akiwa Mjumbe wa Bunge hilo? mbona  na yeye alishapokea fedha hizo kwa nini asingezikataa maana kwa kufanya vile naye alikuwa mmoja wa wahujumu wa fedha hizo  za watanzania.

Wanafalsafa  wanajihoji,kulikoni  inawezekana,kuwa mtu anaweza kupoteza umaarufu wake bila ya kujielewa kwani wengi hupoteza umaarufu wao kwa kufanya vituko ambavyo jamii inavishangaa.kwa kufanya kitu kizuri katika wakati mbaya. 'Inaupasa tuwe na Demokrasia yenye nasaha ili nchi iendelee uwa na Amani,Utulivu,Upendo na Maelewano baina ya watawala na watawaliwa'

Friday, September 12, 2014

MWENYEKITI WA TCD MHE. MOMOSE CHEYO ASEMA RAIS JAKAYA KIKWETE ALIKUTANA NA TCD NA SIYO ALIKUTANA NA UKAWA MJINI DODOMA

Hayo yalisemwa na mwenyekiti huyo kwenye kipindi cha Jambo kinachorushwa na TBC1 kuwa hakupenda vichwa vya baadhi ya magazeti kuandika " Kikwete akutana na UKAWA Mjini Dodoma" bali ilitakiwa iwe Kikwete akutana na TCD Mjini Dodoma.

Aidha alisema kuwa mazungumzo yao na Rais yakifikia makubaliano,lakini cha ajabu bado kuna baadhi yao wamekuwa wagumu kurudi Bungeni kuendelea na majadiliano ya Rasim ya Katiba.

Alisema Bunge maalumu la Katiba lipo kisheria hivyo haliwezi kuvunjwa kwa ajili ya watu wachache walioko nje ya Bunge, bali litaendelea hadi tarehe 4/10/2014.na kwamba amewasihi wananchi kuwa waulivu kazi waliyo watuma inaendelea vizuri.

Na hakuna chama kinacho taka nchi iingie kwenye vurugu,aidha vijana wasichochewe na wachache hao kwa madai ya kuingia barabarani,kwani watakao pata madhara wao wenyewe watakuwa mbali hiyo ndiyo sifa ya wachochezi.

Saturday, September 6, 2014

MABADILIKO YA HALI YA HEWA KATIKA MANISPAA YA DODOMA KWA SIKU NNE MFULULIZO ,BARIDI,UPEPO NA MAWINGU UTAZANI TUKO NYANDA ZA JUU KUSINI

 Hiyo ndiyo Dodoma picha hizo zimepigwa baada ya kajua kujitokeza  kidogo lakini baridi ni palepale,mchana na usiku. Mzunguko wa Stendi kuu ya Mkoa wa Dodoma
 Kushoto kwako ni barabara kutokea Bungeni kuelekea mjini,na Kulia kwako ni barabara kutoka mjini kuelekea Bungeni au Morogoro.
 Barabara ya kuelekea Dodoma Sekondari
Kituo cha Bodaboda  Bohari jirani na Muungano Club na Dispensary ya Makole mkabala na maktaba ya Mkoa wa Dodoma

Friday, September 5, 2014

ZIARA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE MKOANI DODOMA ILIFANA KATIKA UZINDUZI WA MIRADI KADHAA YA MAENDELEO KATIKA AWAMU YAKE YA NNE KISHA KUZUNGUMZA NA WAZEE WA DODOMA

 Katika baadhi ya miradi ya Maendeleo iliyofanyiwa uzinduzi katika ziara ya kikazi Mkoani Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ni nyumba za Shirika la nyumba la Taifa Medeli katika Manispaa ya Dodoma.
 Nyumba hizo zinapangishwa na kuuwa kwa wananchi.Mwananchi yeyote anaweza akanunua kwakupitia mikopo katika Taasisi za fedha.
 Ukiwa nauweo unanunua nyumba katika Shirika la nyumba la Taifa
Mwenye macho hambiwi tazama Jinsi Serikali ya Awamu ya Nne ilivyo jitahidi kutimia ahadi zake wakati wa uchaguzi,Hiyo ni moja ya shughuli  za Serikali hii,bado miundo Mbinu ya Barabara,Reli Viwanja vya ndega pamoja na huduma mbalimbali za Jamii.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA MHE.GOFREY ZAMBI AWAPONGEZA WATOTO WADOGO WANACHAMA WA VICOBA DODOMA WAKATI AKIZINDUA VIKOBA ENDELEVU MKOANI DODOMA HIVI KARIBUNI

 Naibu Waziri wa Kilimo chakula na Ushirika Mhe.Godfrey Zambi akiwasalimia watoto wanachama waVIBOBA kabla hajafanya uzinduzi wa VICOBA endelevu mkoani Dodoma hivi karibuni.
 Mhe.Zambi akwasalimia watoto wa VICOBA na ni  wanachama waVicoba Mkoani Dodoma
 Akikagua bidhaa mbalimbali kutoka  VIKOBA
 Wkiwa tayari kupokea maandamano ya wanacha wa VICOBA katika viwanja vya Mwl. Nyerere Mjini Dodoma Hivi karibuni.
 Mh . Zambi akiangalia shati la kitenge kikundi cha VICOBA wakati akitembelea miradi ya wanavicoba kabla ya uzinduzi wa VICOBA Mjini Dodoma hivi karibuni.
 Maandamano ya wanachama wa VICOBA yakiingia katika viwanja vya Nyerere Square katika Manispaa ya Dodoma wakati Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhe.Godfrey Zambi akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa VICOBA Mkoani Dodoma hivi karibuni.
 Rais wa VICOBA Nchini Mhe. Devota Likokola Mkuwa kwenye nguo iliyoandikwa VICOBA akimweleza Mgeni rasmi umuhimu wa kuweka akiba kwa kutumia kitabu cha kuweka akiba.
 Mhe. Likokola akipokea maelezo kutoka LAPF Jinsi mfuko huo unavyo wasaidia wananchi waliosataafu na wale wanaopenda kujiunga ili wapatiwe mikopo hasa ya ujasiliamali.
 Rais wa VICOBA Mhe. Devota Likokola Mkuwa akitoa utambulisho kwa wanachama na wageni mbalimbali waalikwa katika uzinduzi huo Mkoani Dodoma hivi karibuni.
Mlezi wa VICOBA Mkoani Dodoma  Bw.Anthon Mavunde.kijana aliyeaminiwa,pia ni mwanasheria