Monday, September 9, 2013

SERIKALI YAAGIZA MIKOPO YA ELIMU YA JUU IRUIDISHWE ILI WENGINE

 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Dkt Shukuru Kawambwa akiongea na wahitimu wa Stashahada na Shahada ya Kompyuta Sayansi katika chuo cha St,Joseph Songea leo wanachuo 96 wamehitimu mafunzo hayo.




 Picha ya pamoja ya wahitimu wa Shahada ya kwanza katika Kompyuta Sayansi
 Picha ya pamoja ya wahitimu wa Stashahada
Picha ya pamoja ya wahitimu wa Stashahada

 Wahitimu wakila kiapo kabla hawajatunukiwa Stashahada na Shahada zao.
Mawaziri wakimsikiliza mtoa maelezo kwenye chumba cha Kompyuta sayansi



SERIKALI imewataka wanafunzi wa elimu ya juu ambao wanakopeshwa fedha na Bodi ya mikopo nchini kuirejesha mikopo hiyo,mara tu  wanapo malize elimu yao na kufanikiwa kupata ajira, kwa kulipa mikopo hiyo kuitafanya serikali kuweze kuwakopesha wanachuo wengine.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa kwenye mahafali ya nne yaliyofanyika St, Joseph  College of Information Technology Ruhuwiko nje kidogo ya Mji wa Songea leo.
Alisema serikali inahitaji kutoa elimu ya juu kwa wanachuo wote wenye sifa na vigezo vya kujiunga na vyuo vikuu nchini,na itajitahidi kutoa mikopo kwa kadiri ya uwezo wake ingawa idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa ni wengi,kwa hiyo waliyo kopeshwa wakirejesha mikopo hiyo wanachuo wenye kuhitaji mikopo hiyo watapata.
Aidha ameto rai kwa waajiri kuonyeshe ushirikiano wao na serikali  katika kukusanya fedha hizo kwa wahitimu ambao wamewaajiri, kurejesha mikopo hiyo kwenye bodi ya mikopo.na wasipo fanya hivyo hatua kadhaa zitachukuliwa zidi yao.
Alisema serikali imetengenga shilingi trioni 1.45 kwa wanafunzi wa elimu ya juu,Wizara kupitia elimu ya juu na bodi ya mikopo imeamua kuongeza kiwango cha mkopo kwa mwanafunzi wa elimu ya hiyo.
Katika mahafali hayo wanachuo 96 wamehitimu mafunzo yao na kutunukiwa Stashahada kwa wanachuo 39  katika Fani ya Uhandisi wa Sayansi ya Kompyuta na 58 shahada ya kwanza katika Uhandisi wa Sayansi ya Kompyuta.