Thursday, July 25, 2013

TUNAJIFUNZA STORI YA USTAARABU WA PWANI KWA KUTEMBELEA MAENDOA YA KISTORIA NA KUONA JINSI MABABUZETU WALIVYO FANYISHWA KAZI NA WAGENI WALIYOINGIA PWANI YA AFRIKA MASHARIKI KATIKA MJI WA BAGAMOYO

 Ukristo ulivyo ingia Bagamoyo,wamisionari walijenga jengo hilo kuwa la mapadre.
 Lakini pia walivyoingia Waarabu Bagamoyo wakafika na Ustaarabu wao wa kiislamu ambapo walikuwa wafanya biashara kwenda bara kutafuta pembe za ndovu na watumwa.jengo hilo ndilo lilikuwa la matajiri  wa kiarabu wafanya biashara jengo lililojengwa matumbawe.
 Hilo ni handaki ambalo lilijengwa na wamisionari kwa ajili ya kujihami na maadui ,hilo handaki limeenda kadi kanisani,nyumba za mapadre chini kwa chini.ambapo sasa halitumiki limewekewa mifuniko kwa ajili ya ukumbusho na watalli kwenda kuona mji Mkongwe wa kihistoria Bagamoyo.


Friday, July 19, 2013

MABOMBA YA GESI ASILIA YAPAKULIWA KATIKA BANDARI YA MTWARA WAZIRI MKUU WA MIZENGO PINDA ASHUHUDIA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda na wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Bw.Simba Kalia walishuhudia shehena ya mabomba ya kupitishia Gesi yakipakulia kutoka katika meli.
Baada ya ushuhuda huo Waziri Mkuu amarejea Mkoani Ruvuma kuendelea na Ziara yake ambapo leo amefanya ziara Muhukuru na kwenye daraja la Umoja wa Tanzania na Msumbiji.

VIONGOZI WA WATENDAJI WA TUJIFUNZE KUSINI JANA WALIUNGANA NA WANANCHI WA AFRIKA KUSINI KUMPONGEZA NA KUMTAKIA AFYA NJEAMA MWANAHARAKATI RAIS WA ZAMANI MZEE NELSON MANDELA MADIBA KWA KUTIMIZA MIAKA 95 YA KUZALIWA

VIONGOZI na watendaji wa TUJIFUNZE KUSINI jana walijumuika na wananchi wa Afrika Kusini katika maazimisho ya miaka 95 yakuzaliwa  mwanaharakati wa nchi hiyo aliyopinga ubaguzi wa rangi hadi kwenda jela kwa ajili ya kuwatetea wananchi wa nchi hiyo,na hatimaye akawa Rais ,na sasa Rais mstaafu mzee Nelson Mandela.
Tunamuombea Mungu ampunguzie makali ya kuugua kwake ,na apate afya njema kwani bado mchango wake  unahitajika.
Ambapo Mkewe alisema hali ya mzee huyo kwa sasa inatia matumaini,anaendelea vizuri,kwa hiyo Mungu ataendelea kumpa nguvu na kuwa na afya njema.Tunazidi kumuombea kwa Mungu afya yake irejee kama awali.

Wednesday, July 17, 2013

WANAHABARI WALIYORIPOTI AJALI ILIYOTOKEA KWENYE MSAFALA WA WAZIRI MKUU JANA ENEO LA NAMTUMBO WATIMULIWA KWENYE MSAFARA HUO, NA AJALI NYINGINE YATOKEA MBINGA GARI LA POLISI

WAKATI mwandishi wa Waziri Mkuu kuwatoa waandishi wawili wa mkoani Ruvuma  kwa kuripoti ajali iliyotokea kwenye msafara wa Waziri Mkuu jana katika eneo la Nantumbo , leo tena ajali nyingine imetokea kwenye ziara ya wilaya Mpya ya Nyasa na Mbinga ya gari la polisi.Hakuna aliyetangaza hiyo.

Kumbe ajali Zinapotokea za Waziri Mkuu hazitakiwi kutangazwa, Na waandishi wa habari ambao si wa Waziri Mkuu? Na waandishi wa Mawaziri wakuu wamepata mafunzo ya kuwakataza waandishi wengine wasitangaze matukio yanayotokeayawe  mazuri au mabaya katika Ziara ya Waziri Mkuu,na watangaze wao na wasipo tangaza basi, sasa nini maana ya uandishi wa habari?

Monday, July 15, 2013

WAZIRI MKUU WA JAMHURU YA MUUNGANO WA TANZANIA MIZENGO KAYANZA PINDA AWEKA JIWE LA MSINGI LA CHUO CHA UALIMU KIUMA BONITE TUNDURU

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Kayanza Pinda


WARIZRI Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Pinda ameweka jiwe la msingi chuo cha Ualimu Kiuma Bonite Tunduru ,Chuo  kinacho milikiwa na Mkurugenzi Dkt.Matomola,ikiwa ni Taasisi kubwa inayo unganisha Chuo cha Waganga,shule msingi na  sekondari na shughuli nyingine za maendeleo.
Mhe.Pinda alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa shirika hilo la Bonite ambalo linaliletea maendeli wananchi wa Tunduru, Mkoa wa Ruvuma na majirani pamoja na Taifa kwa ujumla.na kwamba alimshukuru sana Dkt Matomola kwa moyo wake wa uzalendo wa kuanzisha taasisi kubwa kama ile kwa manufaa ya taifa, badala ya kujinufaisha mwenyewe.
Aidha mhe.Pinda katika mkutano na  wananchi mjini Tunduru leo, alisema ushururu kwa watu wadogo wadogo usitozwe, maana unaleta kero kwa wananchi wa hali ya chini.
Kuhusu maendeleo ya elimu wilayani humo, Mhe. Pinda amemwambia Mkuu wa mkoa kuwa asili 30 ya watoto wote waliyo faulu kuingia Kidato cha kwanza, ambao hawaja ripoti waende shule mara moja.
Ambapo kuhusu ujenzi kwa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Namtumbo hadi Tunduru utaendelea kujengwa baada ya wakandarasi wa  awali kufukuzwa kwa kushinda kukamilisha katika muda waliyo pangiwa.
Waziri Mkuu amesikia kilio cha watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambao wamekaa  kwa miaka mingi bila kupata uhamisho kama vile ndiyo wamehamia, amewaambia mara baada ya kufika Songea ataangalia nini cha kufanya. ( Na. Juma Nyumayo katika Msafara wa Waziri Mkuu mkoani Ruvuma )

Saturday, July 13, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MKOANI RUVUMA NA MKUU WA MKOA WA MKOA HUO BWANA SAID THABIT MWAMBUNGU KUWA ,WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. MIZENGO PINDA ATAFANYA ZIARA MKOANI RUVUMA KWA SIKU 8

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe; Said Thabit Mwambungu akizungmza na waandishi wa habari
 Waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma wakifanya kazi zao,tayari kwa kuwapa wananch habari.,Peni/kamera na computer.
Waandishi wa habari ofisini kwa mkuu wa Mkoa


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda taanza ziara ya siku 8 katika mkoa wa Ruvuma kuanzia siku ya Jumatatu kuelekea wilaya ya Tunduru.

Akizungumza na waandishi wa  habari , Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Said Thabiti Mwambungu, kuwa Waziri Mkuu katika ziara hiyo atatembelea wilaya tano zote  za Mkoa huo na kukagua miradi, kuweka mawe ya msingi, kuzindua miradi na kuongea na wananchi.

Aliwataka wananchi katika Manispaa ya Songea kujitokeze kumlaki katika Ikulu ndogo Mjini Songea kesho Jumapili,na kuanza ziara Wilaya ya Tunduru, Namtumbo, Wilaya ya Nyasa na kuizindua Wilaya mpya ya Nyasa.

Baada ya hapo atakwenda wilaya ya mbinga, Songea Manispaa na Songea Vijijini na kuongea na wananchi na kisha  kurejea nyumbani siku ya Jumapili.


Friday, July 12, 2013

nimerudi tena wasomaji wa Blog ya TUJIFUNZE KUSINI baada ya kuadimika kwa muda kidogo

 Hapa nikitoka nje ya Ofisi ya TUJIFUNZE na wageni wangu waliyoitembelea ofisi hii leo ni wahasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga,Mie ni mwenye suti.
Mwenye suti nyeusi ni Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga akiwa na watendaji wake wawili tuikbadilishana mawazo.

MAAFISA KUTOKA KITENGO CHA UHASIBU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA WATEMBELA KITUO CHA UCHAJI KANDA YA KUSINI SONGE

 Wgeni hao walikuwa wakiambiwa shughuli zinazofanywa kwenye kituo hicho,na Mahriri wa TUJIFUNZE Kanda ya Kusini Bw.Christian Sikapundwa mwenye suti na tai sehemu ya ujaridi na ukunjaji wa magazeti.
 Pia hapo akiwaelekeze mashine ya kukata au kusafisha kazi zilizokwisha kuchapwa.
Hapo mkuu wa msafara huo Mweka hazina wa Halmashauri ya  Wilaya ya Mbinga bw.Stephen Sidagulu ,anayepiga picha ,akipiga picha mashine ya kukunja haipo pichani.
 Maelezo yakiendelea kutolewa sehemu ya ukunjaji wa magazeti.
Wikiangalie sehemu ya mashine kubwa ya kuchapa SORK ambayo inachapa magazeti makubwa ya TUJIFUNZE.
Aida walisema ni vigumu kutambua kama kuna mitambo mikubwa kiasi hicho, ukiwa unarudia mapokezi.Kwa kuwa ni nadra sana watu kuingizwa kiwandani hasa wakati wa uchapishaji nyaraka za siri za kiserikali  na machapishi mengine ya kijamii.