Monday, April 29, 2013

WASTAAFU WA UTUMISHI WA UMMA WALALAMIKIA UCHELEWESHWAJI WA MALIPO YA PESHENI ZAO BADALA YA MIEZI MITATU KULIPWA FEDHA HIZO NA HUCHELEWESHWA HADI MIEZI MINNE - RUVUMA

 Bwana Rashid Holela akielezea jinsi malipo ya wastaafu yanavyocheleweshwa katika Benki ya NMB tawi la Songea.Alisema fedha walizo fika kuzichukua zilikuwa zilipwe mwezi wa tatu lakini hadi leo tarehe 29/4/2013 fedha hizo hazijaingizwa.
Wasomaji wa Blog hii picha hiyo ya Bw.Rashid siyo 'Action' hapana anasema kwa jaziba akionyesha wazee wezake waliyo kaa katika ukuta wa Benki ya NMB bila kujua hatima yao kuhusu pesa hizo.Akimwambia Ripota na Mwakilishi wa Radio UHURU Mkoa wa Ruvuma Bwana Juma Nyumayo, kuwa waambie na wazee wengine wanakoisikia Radio hiyo kuwa wawaunge mkono maana kilio hicho wanaamini ni cha wengi ' aliyeshiba hamjui mwenye njaa' alisema Bw.Rashid.
 Bwana Rashid anasisitiza kuwa Serikali haiwatendei haki wazee waliofanya kazi serikalini wakiwa watumishi wa Umma. kwanza fedha tunazolipwa hazikidhi haja kutokana na maisha yalivyo kuwa magumu,pili pamoja na hicho kidogo kulipwa mapema, nacho kinacheleweshwa. Hivyo wanavyo fanya hivi hawaji kustaafu siku moja ? aliuliza Bw.Rashid.( Picha na Juma Nyumayo)
 Hapa Bw.Holela akimwita mzee mwenzake Bw. Mapunda afike apige picha pamoja ili kilio hicho kisiwe chake peke yake,wakati walikuwa pamoja wakiahangaika wapi wapate fedha,maana za Pesheni wenye zao wamegoma kuwapa.
 Huyo aliyesimama mwenye koti ndiye Mzee Tobiasi Mapunda kutoka Lituhi kuja Tawi la NMB Songea kufuatia Pesheni yake na kuambulia patupu.
Pamoja na kuwa na mwenzake Mzee mapunda lakini Bwana Holela Rashidi bado alikuwa akiendelea kulaumu utaratibu uliyo wekwa na Serikali wa kuwalipa Pesheni wastaafu kila baada ya miezi mitatu na kisha kupitiliza hadi miezi mnne.


WASTAAFU wa utumishi wa Umma katika Mkoa wa Ruvuma ,wanaulalamikia utaratibu wa malipo yao ya  Pesheni yanavyolipwa ambayo  hayaende kama serikali ilivyo tamka ya kulipwa kila baada  ya miezi mitatu mitatu.

Wakizungumza na Blog hii leo katika Manspaa ya Songea katika Tawi la Benki ya NMB walipo fika kuchukua fedha zao za mpesheni hawakuyaamini macho yao baada ya kukuta salio lao halitoshi.

Bwana Holela Rashidi anasema “ mpaka leo hii ni mwezi wa nne sasa hawajatuingizi fedha zetu za Pesheni ambazo zilitakiwa tuzichukue mwezi wa tatu, walituambia kuwa watakuwa wanatulipa kila baada ya miezi mitatu mitatu, lakini cha ajabu tunakwenda kwenye ITM kuangalia salio hakuna kilicho ingizwa.”

“Tumiitumikia nchi hii, leo serikali inatufanyia vitendo hivi, mbona ni manyanyaso makubwa  sana, wengine wanatoka mbali wilaya ya Mbinga kuja kufuata mafao yao na wanapoyakosa inawalazimu kukaa kwa jamaa zao, ambapo huleta kero kwa wenyeji wao” Alisema Bw.Rashidi.

Naye Mzee Tobias Mapunda ametoka Wilaya ya Mbinga,” anasema nimetoka Litui Wilaya ya Mbinga kuja kuchukua pesheni yangu ya miezi mitatu kama serikali ilivyo tuhaidi,lakini nilivyo angalia salio sikukuta fedha iliyoingizwa.na leo ni tarehe 29 mwezi wa nne, na fedhi hiyo ilibidi tulipwe tarehe 30 mwezi wa tatu”.

Aidha alisema kuwa tulienda hazina ndogo ya Mkoa wa Ruvuma ,na huko tuliambiwa fedha imishapelekwa Benki ya NMB Tawi la  Songea, lakini tulivyo fika kwa meneja wa Benki tawi hilo tuliambiwa fedha hazija fika, sasa tumlaumu nani ? kati ya Hazina na Benki? Huo ndiyo utaratibu wa serikali au ni utaratibu wa Hazina na Benki kuwaingiza Wastaafu katika madeni wasiyoyapanga ? aliuliza mzee Mapunda kwa uchungu mkubwa.

Hicho ndicho kilio cha wazee wa Utumishi wa Umma waliostaafu na walilitumikia taifa hili na kuliacha na watumishi wengine ambao na wao kuna siku watakuwa wastaafu kama walivyo wazee hao  Hivyo waliopewa dhama hiyo ya kuwatendea haki wazee hao wawahudumie wazee hao, sio wa mkoa wa Ruvuma peke yao, bali ugonjwa huu upo kwa nchi nzima, la kuwabeza wazee,lakini wanasahau kuwa na wao ni wazee wa baadaye.

Saturday, April 27, 2013

WANAKAMATI WAIENDA KUCHUKUA CHAKULA ,WAKALA NA KUNYWA NA KUTAKIANA AFYA KAMA PICHA ZITAKAZO JIELEZA


















KAMATI YA HARUSI ILIYOFANIKISHA HARUSI YA BWANA MPELASOKA SONGEA IMEVUNJA KAMATI KWA KULA NA KUNYWA FUATILIA PICHA HIZO.

 Bwana Mpelasoka Bwana harusi amitisha kamati yake kuvunja kamati kati Bwalo la Polisi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.Ambapo kila kamati ilijaribu kuelezea mafanikio ya siku hiyo na changamoto alizokutana nazo siku hiyo.
 Bwana Mpelasoka akishukuru wanakamati aliyesimsms
 Wa kwanza ni Mzazi upande wa Bwana Harusi
 Ambaye sasa alisimama na kuishukuru kamati hiyo
 Huyo ni Mama wa Bibi harusi amesafiri kutoka Bukoba hadi Songea kuja kuona Binti yake anakoishi ameishukuru sana kamati hiyo.
 Huyo ndiye mwekiti wa kamati hiyo aliyefanikisha kwa kiasi kikubwa.
 Upqnde wa Bw.Harusi akiishukuru kamati
 Dada huyo na Katibu wa kamati hiyo
 Dkt Mstaafu upande wa Bw.Harusi akiishukuru kamati
 Baba wa karibu wa Bwana harusi katika Manispaa hii ya Songea Haule Ok ,naye aliwashukuru wanakamati
Mzee Mwakanosya upande wa wazazi Bwana harusi.akishukuru

Friday, April 26, 2013

MIAKA 49 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR RAIS KIKWETE KATOA MSAMAHA WA WAFUNGWA 4,180

 Rais Kikwete akimaliza kukagua gwaride katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika sherehe za Miaka 49 wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,Uliyo anzishwa na Waasisi Baba wa Taifa na Aman Abed Karume
Picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
 Picha ya Rais wa Zanzibar Karume zilizo yumika na watoto wa halaiki wakati wakiimba wimbo maalumu.
 Halaiki walitengeneza maumbo mbalimbali yenye mafundisho.Umbo la kwanza lilikuwa miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 Kikosi cha bendera kilitoa heshima mbele ya Jukwaa kuu.
 Rais akielekea Jukwaani baada ya kukagua gwaride.
 Kama unavyona Herufi hizo
 Maumbo mbalimbali
Umbo hilo ni mazao ya biashara,Ninawapongeza waliofanya kazi hiyo ya kufundisha vijana hao ,wakawa mahili katika kutengeneza maumbo hayo kwa kutumia miili yao na mavazi yao.Nawapongeza sana,lakini cha ajabu bado kuna watu wanaobeza kazi za mwalimu,wanamacho lakini hawaoni wanaimani lakini hawa amini kazi za walimu.Kazi hiyo isingefanikiwa bila ya mwalimu kuingia hapo.Hata kama si mwalimu aliyofanikisha Halaiki hiyo,basi kafanya kazi ya mtu anaitwa mwalimu, japo hakupata Methodology.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa msamaha kwa wafungwa 4,180 ,ili waende kuungana na familia zao,na kwamba watakuwa wamepata fundisho na wataishi vyema kwenye jamii walizotoka.
Aidha msamaha huo haukuwausu waenye kifungo cha maisha, watumiaji madawa ya kulevya.
 
Maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilijumuisha Gwaride lilokuwa na Guard 10.ambazo zilikaguliwa na Rais. Na ndege za mafunzo za kivita zilionyesha umahili uliyotumika na marubani wa ndege hizo,ambapo ndege ya tano iliendeshwa na Luteni Kanali Sinzia.
Pia kukawa na watoto wa halaiki 2,695 wa kutoka Tanzania Bara na Tanzania Visiwani ambao walinyesha mazoezi ya viungo,kutengeneza maumbo mbalimbali yenye mafundisho.Na wazheza sarakasi 35 ambao walionyesha michezo kadhaa matika kustarehesha wananchi waliyofurika uwanja wa Uhuru.
Sherehe hizo zilipambwa na ngoma kutoka Tarime Mkoa wa Mara,Gonga kutoka Mkoa wa Kusini Pemba na Sindimba kutoka Mkoa wa Lindi na kwaya kutoka JKT  Masange  Tabora.

Thursday, April 25, 2013

WAENDESHA YEBOYEBO KATIKA MANISPAA YA SONGEA WANAPATA MAFUNZO YA SIKU 7 YA USALAMA BARABARANI

 Mkufunzi wa mafunzo ya waendesha yeboyebo wa Manispaa ya Songea Bw.Faustin Gabriel Matina kutoka kitengo cha Usalama barabarani Jijini Dar es Salaam alisema tunatoa mafunzo hayo kwa madereva ili wazifahamu alama zilizoko barabarani.Waendesha yeboyebo 400  watanufaika na mafunzo hayo ,ambapo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabiti Mwambungu alifungua mafunzo hayo.
 Mkufunzi akisisitiza alama hizo
 Mkufunzi Matina akisikiliza maswali kutoka kwa wanafunzi wake.
 Naibu Mwenyekiti wa waendesha yeboyebo Bw,Abed Nchimbi
 Waendesha yeboyebo
 Baadhi ya yeboyebo zao