Friday, November 30, 2012

WAHISANI WATAKABIDHI VIFAA VYA HOSPITALI YA MKOA WA SONGEA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI HAMSINI ( 50 MILIONI )

 Bi Biffa Barran Sulle akiwaelezea waandishi wa vymombo vya habari idadi ya vifaa vilivyo kuweko ndani ya container ,ambavyo kesho pamoja na viongozi wa UWT mkoa watakabidhi kwenye uongozi wa hospitali ya mkoa ya Songea.
Baadhi ya waandishi wa vyombo vya habari pamoja na uongozi wa UWT mkoa na mgeni wao Bi Sulle katika ukumbi wa Serengeti katika Manispaa ya Songea leo.

COORDINATOR wa wahisani hao Bibi Biffa Barran Sulle  The Tanzania Ecology Serving Foundation ( Country Coordinator ),akiongea na vyombo vya habari Mkoani hapa alisema kuwa Container la vifaa hivyo lipo njiani na kesho asubuhi kutakuwepo na makabidhiano na uongozi wa Hospitali ya mkoa.
 Bibi Sulle alivitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na vitanda 30 vya umeme,microscope moja,microscope kubwa mbili,taa ya upasuaji,taa malum ya buluu,taa yenye lensi,” Defilibrator tatu,Light boxe tatu za X – ray,matandiko 29,makasha 102  yenye vifaa vya hospiltali  na Sacs with clothes.
Vingine Side table 15,Dentist lamp,Dentist  chair,Toy  pieces mbili,box 10 za vifaa vya hospitali,box 10 za ring binders,Centrifuge for blood, Respirator mbili,Utrasound Scanner and,Lift for patients
Aidha alisema katika container hilo kuna vifaa  vya elimu,vikiwemo vitabu,box tano,Incubator kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda ( pre – mature

HOSPITALI YA MKOA YA SONGEA YAPATA MSAADA WA VIFAA VYA HOSPITALI TOKA DENMARK

   Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mheshimiwa Dokta Teresa Hovisa Luoga akizungumza na uongozi wa Hospitali ya mkoa ya Songea katika ukumbi wa Hospitali  pamoja na vyombo vya habari leo.
 Bibi Biffa Barran Sulle Tanzania Ecology Serving Foundation Country Coordinator akiandika vifaa  hospitali vilivyo kuwepo kwenye container
Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa Dokta Mallecela akito shukurani kwa wahisani,na Mheshimiwa Dkt Teresa Hovisa Luoga kwa  jitihadi alizozifanya ya kutafuta wahisani ambao wame toa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 50.


Mheshimiwa Dkt Teresa Hovisa Luoga alisema vifaa hivi vitakabidhiwa kesho katika hospitali ya Mkoa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Bibi Kuluthumu ,akikabidhiwa na ( Coordinator wa wahisani hao,Bibi Biffa Barran Sulle baada ya kupokea Container la VIFAA hivyo naye kukabidhi  kwa uongozi wa Hospitali ya mkoa kwa niaba ya Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Dokta Teresa  Hovisa Luoga vyenye thamani ya zaid ya shilingi milioni hamsini za kitanzania ( shilingi 50 milioni )
Aidha Mhe. mashindano ya usafi,kwani usafi upo ndani ya moyo wa mtu,na kwamba miti ya mlima wa matogoro imepungua hivyo ipandwe mingine ili upungufu wa maji usije ukajitokeza kama ilivyo jitokeza mwaka huu.
 Naye Bibi Biffa Barran Sulle wa Tanzania Ecology Serving  Foundation   Country Coordinator alisema vifaa hivyo ni Item 247. katika Container hilo.Dkt Hovisa alisema msaada huo umetolewa na wazee wastaafu wa Denmark waliyotembelea Hospitali ya mkoa na kuona upungufu wa vitendea kazi ndipo waliporudi kwao  na wakachangishana na kupata vifaa hivyo.
Sambamba na hayo Mhe.Dokta Hovisa ametoa wito kwa wananchi wa Manispaa ya Songea wenye maduka kuwa kila mtu mwenye duka apande mti wa maua,ili kuboresha usafi wa Manispaa hiyo.
Alisema Manispaa iingie kwenye

Tuesday, November 27, 2012

FAST JET AIR LINE YAZINDUA USAFIRI WA NDEGE YAKE KWA BEI POA

 Baadhi ya abiria ambao walikuwa katika uziduzi wa ndege ya Fast Jet Air line wakiwa ndani ya ndege hiho,wanasema ndege zote ni sawa,lia ndege hiyo nauli yake ni nafuu sana inayo mwezesha Matanzania yeyote kuweza kusafiri nayo.
 Baada ya kuzunguka hadi Zanzibar ,Fast Jet ilitua tena kati uwanja wa Mwalimu Nyerere,abilia waliyo kuwemo katika ndwgw hiyo alikuwa wakishuka.
Mwandishi wa habari wa TBC akimhoji mfanyakazi wa kampuni ya ndege hiyo.Mwenye koti leusi,ambapo alisema nauli za ndege hiyo yenye uwezo wa kuchukua abiria 200 itakuwa nafuu na wala siyo nguvu ya soda.amesema mtu anakwenda Mwanza kwa Tshs 40,000/=.
Alisema ndege hiyo itafanya safari zake za Mwanza na Arusha,kuna ndege nyingine zinategemewa kuletwa na kampuni hiyo.na kwamba mtu yeyeto ataweza kumudu nauli za ndege za kampuni hiyo.
Amesema maduka kadhaa yamefunguliwa ya kukatia tiketi,uwanja wa ndege,Double three na maeneo mengine Jijini Dar es Salaam..Aidha alisema kwa siku ya kwanza zaidi ya abiria 100 walikata tiketi zao kwamba hiyo ni dalili na mwanzo mzuri wa kampuni hiyo.

KINYEREZI KUJENGWA MIRADI MITATU YA UMEME WA GESI

Enjinia Felchism Mramba elezea jitiahada za shirika la Umeme linavyo jipanga kupunguza tatazo la umeme kwa wakazi wa Jijini Dar es Salaam kwa kuwa na miradi mitatu ya umeme wa Gesi maeneo ya Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.Alitaja miradi hiyo kuwa na Mradi wa MEGAWAT 159,wa MWGAWAT 240 NA wa MEGAWAT 300.Utakao anza mwaka ujao .

IFIKAPO MWAKA 2015 TATIZO LA UMEME LITAKUWA HADITHI - KIKWETE

 Rais Jakaya Kikwete awambia watanzania kuwa ifikapo mwaka 2015 tatizo la umeme litakuwa hadithi,kutokana na kuongezeka kwa umeme wa Gesi na makaa ya mawe ambayo ni mengi yatakayo zalisha umeme wa kutosha ukisha anza kuzalisha umeme.
Rais Dkt Jakaya Kikwete amewshukuru Watu wa Jamhuri ya China kwa kutoa fegha nyingi katika mzadi wa kuzalisha umeme wa Gesi.'Akufaae kwa dhiki ndiyo rafika' alisema Rais Kikwete wakati akizunguma Jijini Dar es Salaam kuhusu ufumbuzi wa tatizo la umeme wa kutegemea mvua kunyesha.

Wednesday, November 21, 2012

HOSIPTALI YA MKOA YA SONGEA IMEKUMBWA NA UHABA WA MAJI KUTOKANA NA UKAME ULIYO JITOKEZA KWA MWEZI MMOJA SASA

Moja ya jengo la majengo ya Hospitali ya Mkoa ya Songea,Jengo la upasuaji.ambapo maji yamekuwa tatizo kubwa katika ufanisi wa kazi katika Hospitali hiyo ya Mkoa.

WAANDISHI WA HABARI WA MAGAZETI VIJIJINI - TUJIFUNZE KANDA YA KUSINI WAMEANZA KUKUSANYA HABARI ZA GAZETI LAO

 Bwana Juma Nyumayo na Bw.Joram Mwaipopo wakisalimiana katika ofisi ya Mhariri kabla hajaanza safari ya kwenda Mkoani Lindi kuandika habari za TUJIFUNZE toleo la Desemba mwaka huu.
 Bwana Gedion Mwakanosya akiwa katika ofisi ya Tujifunze akisoma mambo muhimu anayotakiwa kwenda kuandika kwa ajili ya Gazeti hilo.karika mkoa wa Mtwara.
Bwana Juma Nyumayo mwenye T - Shirt ya mistari na waandishi wenzake wakisikiliza maelekezo ya kwenda kufanya katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Sunday, November 18, 2012

BREAKING NEWS WANANCHI WA JIJI LA NAIROBI WAFANYA MAANDAMANO YA AMANI YA MAUAJI YA ASKARI WALIYO ULIWA KUASHIRIA USALAMA WA RAIA HAUPO SALAMA NCHINI KENYA

NCHINI Kenya kumekumbwa na mauaji ya ugaidi ambapo maaskari 35 wamauawa kutokana na ugaidi uanao endelea  hivi sasa,ambapo bomu lililotegwa kwenye daladala limelipuka na kua abiria  5  Isilii Jijini Nairobi   na majerui 18 walipelekwa hospitali kwa matibabu.

BREAKING NEWS !! ( USAJILI WA WAPIGA KURA NCHINI KENYA UNAANZA KESHO.

USAJILI wa wapiga kura nchini Kenya unaanza kesho tarehe 19 /11/2012 hadi  tarehe 18 /12/2012 kwa wananchi wenye umri wa miaka 18 katika vituo 25 ambapo vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 11 jioni ( chanzo cha habari ni Mchapuko wa Habari K 24 )

Friday, November 16, 2012

WATUMISHI WATATU WA KITUO CHA MAGAZETI VIJIJINI KANDA YA KUSINI SONGEA WAAGWA LEO KATIKA HOTELI YA NIPASHE MJINI SONGEA RUVUMA



 Hiyo ndiyo meza kuu waliyo kaa wastaafu na wenzi wao wa katika mwenye tai na mkewe nia Bw.Siprian Tawete mstaafu mwaka 206,anayefuata kulia kwake mwenye kitambaa cheupe Bibi Feblonia Banda aliyestaafu mwaka 2010 na Mmewe Mr.Banda na wa tatu ni kwenye suti nyeusi amezibwa na ua Bw.Joramu Mwaipopo kushoto kwake ni Mkewe Mrs Mwaipopo.
 Bwana na Bibi Tawete
 Bibi na Bwana Banda
 Bwana na Bibi Mwaipopo
 Mfanya kazi aliyebakia kituoni Bw.John Mponda mlinzi na Mkewe.
 Bwana Charles Lukoto Mpiga chapa
 Wageni waalikwa wa kwanza Mke wa Mhariri msaidizi Bw. Juma Nyumayo ( Mrs Nyumayo)
 Mke wa aliyekuwa Mkuu wa kituo hicho (Marehemu Enos Mwabina) Mrs Mwabina

 Mrs Nyumayo
 Mhariri wa kituo hicho Bw.Christian Sikapundwa
Baadhi ya wasaidizi wa kituo katika kuelemewa na kazi Bw. Yusufu Kufakunoga chumba cha giza ( dark room ).


Kituo cha uchapaji Magazeti Vijijini ,Kanda ya Kusini leo kimewaaga wafanya kazi watatu waliyostaafu kwa miaka tofauti.

KITUO cha magazeti vijijini Kanda ya Kusini Songea ,kimewaaga wafayakazi watatu waliyostaafu kwa mujibu wa utumishi baada ya kufikisha miaka 60 wa umri kwa kuwafanyia tafrija fupi katika Hoteli ya Nipashe maeneo ya Mabatini katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Watumishi waliyo staafu kulingana na kupishana kwao ni pamoja na Bwana Siprian Tawete aliyekuwa Mlinzi mwaka 2005,Feblonia Banda Mtunza ofisi mwaka 2010 na watau ni Bwana Joramu Mwaipopo mlinzi aliyestaafu mwezi Juni 2012.

Tafrija hiyo imejumuisha wataafu na wenzi wao ,ambao wote wemepatiwa zawadi wao na wenzi wao,kama motisha katika utumishi wao walipokuwa kituoni hapo.

Kituo kimewatakia maisha mapya ya kujitegemea baada ya ukomo wa utumishi wao kituoni,na kwamba wao pia wamewatakia wafanya kazi waliyokuwemo katika ajira amani na mshikamano kazini.

Baada ya kustaafu watumishi hao Kituo kimebakiwa na watumishi sita tu kitu ambacho kitafanya kituo kizidiwe na majukumu katika utndaji kazi wao.

Monday, November 12, 2012

HISTORIA YA KILWA KISIWANI IMEIWAKA KISIWA HICHO KATIKA HISTIRIA YA URITHI WA DUNIA AMBAPO WATALII WANAKWENDA KUJIONEA MAAJABU YA MAJENGO YA MISIKITI INATUPASA NA SISI KWENDA KUONA MAAJABU HAYO

 Mnara wa Kilwa kivinje katika mji wa Kilwa kivinje mji ambao wenye historia ya waarabu na ustaarabu wa kiarabu wenye utawala wa Kisultani.
 Hilo ni jengo ambalo lipo pwani ya Halmashauri ya Lindi ambalo lilijengwa enzi ya utawala wa Kisultani
 Mwandishi wa habari na Mhariri Msaidizi wa Magazeti Vijijini Kanda ya Kusini Bw.Juma Nyumayo akisoma kibao kinacho elezea urithi wa Dunia kilichowekwa na UNESCO.kilicho katika kivuko cha kuvushia wakazi wa Kilwa kisiwani  Katika Mji wa Kilwa Masoko.
Asubuhi Bw.Juma Nyumayo akiwa katika mji wa Kilwa Masoko baada ya kumaliza kazi ,akionekana akielekea Lindi Mjini kuelendelea na kazi.

Tuesday, November 6, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI – MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA RUVUMA. • Yafanya Maadhimisho ya sita ( 6 ) ya siku,wiki ya Mlipa kodi tarehe 7/11/2013 Mkoani Ruvuma ( Kauli Mbiu ni “ ULIPAJI KODI WA HIARI KWA TAIFA LENYE MAFANIKIO.”) • Mlipa kodi anao mchango kubwa katika mafanikio ya TRA.

 Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma Bwana Apili Mbaruku akitoa taarifa ya Mamlaka ya TRA Mkoa wa Ruvuma leo kwenye ofisi yake kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusu maadhimisho ya siku ya mlipa kodi yatakayo fanyika kesho.katika Manispaa ya Songea.
 Afisa Elimu kwa Mlipa kodi Bw.Mefti Jackson wa Mamlaka ya TRA Mkoa wa Ruvuma ,ambapo kwa ushirikiano na Timu nzima ya Mamlaka ya TRA mkoani humo ,wameweza kuwapatia leseni za udereva waendesha yeboyebo na madereva wa magali.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja wa TRA Mkoa wa Ruvuma Bw.Apili Mbaruku,ofisini kwake
Watumishi wa TRA .
 Waandishi wa TBC na Channel Ten
Bwana.Juma Nyumayo wa kwanza mwenye kitabu akielezea jins Mamlaka hiyo ilivyo fanikiwa katika utoaji wa leseni kwa Yebo yebo.


MAMLAKA ya mapato Tanzania inatambua na kuwapongeza walipa kodi wote kwa mchango wao mkubwa katika mapato ya Serikali kwa mafanikio ya Taifa,ambapo lengo la Mamlaka ni kuimarisha utendaji wa kazi katika kuongeza makusanyo ya kodi na kuboresha huduma kwa walipa kodi wote.

MENEJA wa TRA Mkoa wa Ruvuma Bwana Apili Mbaruku, akisema hayo wakati akiongea na  waandishi wa vyombo mbalimbali wa Mkoa wa Ruvuma ofisini kwake leo,na kwamba katika maadhimisho hayo kutatolewa mafunzo ya kodi kwa walipa kodi kwa mtindo wa kuuliza maswali na majibu kwa wadau wao.

Mamlaka ya TRA inategemea kutoa msaada wa magodoro 12   kwenye Ward ya watoto katika Hospitali ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma yenye thamani ya shilingi laki nane ( sh.800,000/= ).

Aidha Bw. Mbaruku alisema kuwa Mamlaka ya TRA Mkoani Ruvuma, katika mwaka wa fedha wa 2011/2012,ilikusanya kodi kwa kiwango cha asilimia 109.5 % kwa kodi za ndani na asilimia 96 % kwa kodi ya Forodha.

Kuhusu kodi za ndani ililenga kukusanya shilingi bilioni 5.001/=,badala yake ikavuka malengo kwa kusanya shilingi bilioni 5.476/=,ambapo kodi ya Forodha ilifikia malengo kwa kukusanya shilingi bilioni 223.8/= kama ilivyolengwa kukusanya na kwamba makusanyo halisi yalikuwa zaidi kwa asilimia 31 % ya makusanyo halisi ya mwaka wa fedha wa 2010/2011.

Alisema kuwa katika kuboresha wa ukusanyaji kodi kwa njia ya vitalu,Mamlaka ya TRA mkoani Ruvuma imeweza kuandikisha walipa kodi zaidi ya 1,094 kwa mwaka wa 2011/2012 ,ni pamoja na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa tatu ulioanza mwaka 2008/2009 na kuendelea mwaka 2012/2013.

Kama mpango huo ulivyoanishwa,mkoa wa Ruvuma umewekewa mtandao wa leseni za udereva uliyowezesha makusanyio ya shilingi milioni 424.2/= na leseni zaidi ya 8,500 zilizotolewa mpya au kubadilishwa.

Friday, November 2, 2012

MVUA ZILIZOANZA KUNYESHA KATIKA MANISPAA YA SONGEA KUANZIA JANA ZIMEKUWA MKOMBOZI KWA WAKAZI WA MANISPAA HIYO WALIYOKUWA WAKIHAHA KUTAFUTA MAJI YA KUNYWA NA KUPIKIA KUTOKANA NA UHABA ULIYOJITOKEZA KWA MUDA MREFU

 Leo mji wa Songea ulipata neema ya mvua ,ikiashiria kuwa tatizo la maji katibu litatuliwa.
Wakati mvua ikinyesha watu wenye vyombo vya usafiri walikuwa kwenye vyombo vyao vya usafili wkienda kununu mafuta ili wendelee na shughuli zao za kilasiku.

HUDUMA YA MAFUTA AINA YA PETROLI NA DIZELI KATIKA MANISPAA YA SONGEA BADO INAENDELEA KUWA MBAYA ZAIDI KAMA UTAKAVYOONA FOLENI YA MAGARI NA PIKIPIKI KUELEKEA KWENYE KITUO CHA KISUMA PAI FILLING STATION

LEO katika Manispaa ya Songea pamoja na kuwa na foleni kubwa/ndefu ya magari na pikipiki kuelekea kwenye kituo cha Kisumapai Filling Station kupata huduma ya mafuta,lakini pia kulikuwa na mvua,lakini watu hawakujali hiyo mvua ili mradi wapate huduma hiyo.

 Hiyo ni foleni ya magari kuelekea kwa Kisuma Pai Filling Station,kituo peke yake katika Manispaa ya Songea ndiyo kinatoa huduma hiyo adimu kwa wenye vyombo vya usafiri.
 Hiyo nayo ni foleni ya pikipiki ambayo imeanzia mbali ikiwa ni foleni ya pikipiki na magari kuelekea Kisuma Pai filling Station kupata petroli na dizeli Leo katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Manispaa ya Songea ina vituovingi vinavyouza mafuta lakini ni kimoja tu ndicho kinacho uza mafuta,cha Kisuma pai Filling Station,kwa hivyo foleni ya magari na pikipiki zinakuwa ndefu kwenye kituo hicho cha kuuzia mafuta mjini hapa.

PIKIPIKI NA MAGARI YAWEKA FOLENI YA MAFUTA YA PETROL ,KITUONI KUNA DISELI KISUMAPAI JANA MANISPAA YA SONGEA

 Ni kituo cha kuuza mafuta KISUMAPAI FILLING STATION katika manispaa ya Songea jana kilikua kikiuza mafuta ya Dizeli.lakini foleni kubwa kama ya magali na pikipiki ilikuwa ilisubili huduma ya petroli hapo jana bila kuelewa kuwa petroli wanayo hitaji haikuwepo.
 Hiyo ni foleni iliyoanzia jengo la Chuo kikuu cha SAUT mjini Songe ikielekea kwenye Filling Station ya Kisuma pai ili wapate walau lita moja ya petroli hapo jana.
Shida ya huduma ya mafuta ya petroli na Dizeli katika Manipaa ya Songea,imefanya wenye pikipiki walanguliwe lita moja kwa sh.3,000/= hadi sh.7,000./= ni kituo kimoja tu ndiyo kilikuwa kikiuza Dizeli.