Thursday, October 27, 2011

BREAKING NEWS ! ! ! GARI LILILOKUWA LIKIPELEKA MITIHANI DAR ES SALAAM KUTOKA RUVUMA SONGEA LA PATA AJALI

Habari zilizopatikana kutokana baadhi ya watu waliyokuwepo kwenye Lori hilo inasema kuwa askari wawili majana yao hayakupatikana mara moja wameumia,na baadhi yao ni wazima.Habari zaidi utazipata kwenye vyombo vya habari.

NINANI ANAYE BEZA SEKONDARI WA KATA NCHINI ?

 Mkuu wa shule ya sekondari Kingerikiti Wilyani mbinga Mkoa wa Ruvuma Bwana Gisbert Kilian Kapinga Box 262 MBINGA Mob: 0788609366 akiwa ofisi za TUJIFUNZE KUSINI akifuatia Mock ya wilaya kwa Kidato cha Kwanza na Tatu inayochapwa TUJIFUNZE KUSINI
 Mkuu wa shule sekondari mikaranga Mbinga Bwana Francis Mwella ( Box 38 MBINGA Mob. 0756- 095848 ) maoni kuhusu mafanikio na changamoto zinazojitokeza kwenye sekondari za kata nchini.
Wakuu hao wakiwa ofisi ya TUJIFUNZE KUSINI wakijadili namna ya kuboresha zaidi Taaluma katika shule za sekondari za kata katika wilaya ya Mbinga,ambapo hatua ya kwanza wameanza kuchapisha mitihani ya wilaya yenye mfanano na mitihani ya mwisho ya kidato cha nne na sita.



SEKONDARI za kata nchini Tanzania zanamchango mkubwa kwa vijana ambao wangekosa nafasi ya kusoma elimu ya sekondari za serikali zilizoko na kuonyesha mafanikio makubwa kwa kutoa taaluma kama sekondari nyingine zilizoko iwapo kasoro ndogondogo zilizopo.

Usemi huu umetolewa leo na walimu wakuu wa shule za sekondari Wilaya ya Mbinga,ambapo Bwana Francis Mwella mkuu wa shule  Mikaranga Mbinga anasema kuwa kunawalimu 9 kutoka chuo kikuu Mlimani walifika kwenye mazoezi ya kufundisha, lakini kati ya hao 9 walimu watatu walisoma katika sekondari ya kata mikaranga.

Alisema kuwa kati ya mwaka 2006 hadi 2010 wanafunzi 42 wapo kidato cha tano na sita ambao wamesoma katika sekondari hiyo ya kata. ( 0788609366 ) kwa ufafanuzi zaidi wa mafanikio ya Sekondari za kata nchini.

Naye Mkuu wa shule wa Kingerikiti Bwana Gisbert Kilian Kapinga anasema kuna wanafunzi 40 waliyosoma shule ya sekondari ya kata Kingerikiti kati yao wanafunzi wane ( 4 ) wapo chuo kikuu mwaka wa kwanza.waliyo baki wapo A level ( Box 38, Mbinga,Mob. O756- 095848 ) iwapo utapenda kutoa maoni zaidi kuhusu sekondari za kata nchini Tanzania.

Aidha wakuu hao walisema kuwa iwapo changamoto ndogo ndogo zikitatuliwa shule hizo niza mafaniko makubwa. Walizitaja changamoto hizo kuwa ni mapoja na upungufu wa walimu hasa wa sayansi,maabara ya sayansi na vifaa vyake,miundombinu na kuwekea vipaumbele vya kutolea elimu katika shule hizo.

Shule za sekondari Wilaya ya Mbinga zenye umeme ni pamoja na Mikaranga sekondari wa jenereta la shule,Mkinga sekondari wa Sola,Lundo sekondari wa Sola na Kindimba sekondari umeme wa maji,njia ya kuelekea Litembo.

Wanaodharau sekondari za kata ,kama hazingekuwepo hao walienda vyuo vikuu kutoka wilaya moja tu wangekuwa wapi? Je Tanzania ina Skondari hizo ngapi? Kama idadi itakuwepo zimetoa wanafunzi wangapi waliyopo elimu ya juu?.




Wednesday, October 26, 2011

WIKI LA KISOMO KUFANYIKA MANISPAA YA SONGEA KATA YA MAJENGO KWA MAONYESHO MBALIMBALI

 Afisa Elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Bwana Nathaniel Yonas akizungumza na TUJIFUNZE KUSINI jana kwenye ofisi zao,kuwa maadhimisho ya Juma la Elimu Kiwilaya litafanyika katika Kata ya Majengo kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Majengo.Lengo la maadhimisho hayo ni kujumuika na mataifa mengine Ulimwenguni kuadhimisha na kutathimini maendeleo ya elimu ya watu wazima.
 Bibi Rose Mwombeki ni Afisa Elimu Vielelezo wa Manispaa ya Songea yuko katika Idara ya Elimu ya Watu Wazima Katika Manispaa hiyo.Kauli mbiu ya mwaka huu ni miaka 50 ya uhuru,elimu ya watu wazima ni ukombozi.



Pia Bwana Mpangala Honoratus naye ni Afisa Elimu Kilimo wa Elimu ya Watu Wazima wa Manispaa ya Songea.








WIKI  la kisomo Elimu ya Watu   Kiwilaya litafanyika katika Kata ya Majengo kwenye shule ya msingi ya Majengo kwa kukagua mabanda kadhaa ya maonyesho ya vikundi vya MUKEJA,VIKOBA vinavyoendeshwa na Elimu ya Watu Wazima kuifanya jamii iondokane na ujinga wa kutojua kusoma,kuandika na kuhesaba na kuwa wajasiliamali.

Afisa Elimu ya Watu Wazima katika Manispaa ya Songea Bwana Nathaniel Yonas alisema hayo kwenye ofisi za TUJIFUNZE KUSINI hivi karibuni alipotembelea ofisi hizo na kuelezea jinsi maadhimisho hayo yatakavyo fanyika.

Bw.Yonas alisema katika maadhimisho hayo kutakuwepo na maonyesho kutoka kwenye vikundi vya uzalishaji mali vya MUKEJA NA VICOBA,ambapo wanaonyesha na pia watauza vitu vitakavyo onyeshwa.

Alivitaja vitu hivyo kuwa ni pamoja na ufugaji,kuna maziwa,mayai ambapo wakulima ni pamoja na mboga,matunda pamoja na Sayansi- Kimu.kwa ujumla wake kutakuwa na vikundi saba kutoka MUKEJA na VICOBA nao wataonyesha shughuli zao na kuuza.

Aidha alisema kuwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Kituo cha Songea nayo itakuwa na maonyesho ya Moduli mbalimbali za masomo ya O Level na A Level kwa wanafunzi wa Taasisi hiyo na wa sekondari nyingine kwa ajili ya kusoma mada ambazo huwenda wasingezipata kutokana na uhaba wa vitabu katika shule za sekondari.

Pia alisema kituo cha ufundi stadi cha shule ya msingi Mfaranyaki chenye fani za useremali,uashi na sayansikimu vitashiriki katika maonyesho hayo.

Kituo cha ufundi Stadi Shule ya Msingi Mfaranyaki kina walimu watatu wa fani hizo wakiwemo mwalimu Simoni Humbuka wa fani ya Uashi,Bibi Salvins Mpunga wa Sayansi-Kimu na Bwana Kachanga Ndeka wa Useremala na Italia Mbano wa Sayansi _kimu

Maazimisho hayo ya Songea yaenda sawia na maazimisho ya miaka 50 ya UHURU wa Tanganyika ya kutafakari na kuoanisha mazuri na mabaya yaliyojitokeza ndani ya miaka 50 hiyo ya Uhuru katika Awamu zote nne za uongozi wa Urais katika nchi hii.Elimu hiyo ilivyo anza kashamili baadaye kulegalega na hatimaye kuanza tena kwa mfumo wa ujasiliamali na kujifunza.

Thursday, October 20, 2011

WAGENI WENGI WANATEMBELEA MITAMBO YA UCHAPAJI TUJIFUNZE KUSINI KUJIFUNZA

 Wgeni kutoka chuo cha ualimu Songea Mhasibu na Boharia walitembezwa kiwandani  hapo jana.
 wanaonyeshwa mashine ya kushona ( stitching machine )
 wakionyeshwa mtambo mdogo wa uchapaji GTO
 Wakionyeshwa mtambo mkubwa wa uchapishaji SORK
 Wakionyeshwa meza ya kuandalia kazi ( Light Ta ball )
 waimsikiliza fundi wa mashine kubwa ya uchapishaji akielezea akiwa juu.
 wanaangalia mashine hizo  kwa maini
wakiwa nje ya ofisi ya TUJIFUNZE KUSINI wakiaga.

MAGAZETI VIJIJINI YAMESAIDIA SANA KUFUTA UJINGA NCHINI KATIKA MIAKA 50 YA UHURU

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mhe.Charles Mhagama akielezea umuhimu wa Magazeti ya Kanda za elimu yalivyosaidia kufuta ujinga baada ya kupata UHURU,katika ofisi ya Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE KUSINI jana alipotembelea kuona na kutoa ushauri wa jinsi ya kuyaendeleza magazeti hayo kwa wananchi vijijini ambako magazeti mengine hayawafikiii kiurahisi.
 Mhariri Msaidizi Bwana Juma Nyumayo aliyesimama akimpa faili la nakala za magazeti ya NURU YETU ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini - Mbeya.
 Mhariri Mkuu wa Magazeti ya TUJIFUNZE KUSINI Bwana Christian Sikapundwa kipongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mhe.Charles Mhagama kwa Dhamana kubwa aliyopewa na wananchi ya kuwatumikia na kuiletea maendeleo Manispaa hiyo,bila kujali malumbano yanayosaidia kurudisha nyuma maendeleo ya Mji wa Songea.
 Mhariri Msaidizi wa Tujifunze Ofisini kwake akizungumza na Mtahiki Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama hayupo pichani jana.
 Bwana Juma Nyumayo akimsikiliza kwa makini Meya wa manispaa ya songea Charles Mhagama baada ya kusaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mhariri TUJIFUNZE KUSINI jana.
Meya Mhagama   akimsikiliza Mhariri  wa TUJIFUNZE Bw.Sikapundwa hayupo pichani hapo jana kwenye ofisi hiyo.


Magazeti ya Kanda  yametoa mchango mkubwa katika vijiji miaka 50 ya uhuru wa Tanzania

MAGAZETI ya elimu yametoa mchango mkubwa katika maeneo ya vijiji ambako magazeti mengine yalikuwa hayafikiki kwa urahisi,isitoshe wakati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akitaka kuleta maendeleo baada ya uhuru ,alianzisha Elimu ya Watu Wazima kwa lengo la kuondoa ujinga kwa wananchi wa nchi hii.

Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Charles Mhagama alisema hayo kwenye ofisi za Gazeti la TUJIFUNZE KUSINI wakati akiyapitia baadhi ya nakala za magazeti hayo ya kanda zote saba za elimu yaliyo kuwa yakichapwa na kusambazwa vijijini kwa bei ya Tsh.5  miaka ya nyuma.

Mstahiki Meya Mhagama alisema magazeti hayo wakati yalipokuwa yakichapishwa wananchi wa Kanda ya Kusini waliweza kupata habari za wenzao wa mikoa mingine,wa Mtwara walielewa habari za Songea,wa Mbinga walisoma habari za Ruangwa,  ‘ Hivyo serikali itoa msaada ili magazeti hayo yaweze kuchapishwa na kusambazwa vjijini kama mwanzo.

Magazeti hayo yaliachwa kuchapishwa mwaka 1995 bada ya mashirika yaliyokuwa yakitoa misaada kuacha kutoa misaada hiyo tena katika Kanda,Lakini Kanda ya Kusini imeendelea Kuyachapisha tangu mwaka 2006 hadi sasa ambapo sasa tunaandaa Toleo maalumu la miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.

Tuesday, October 18, 2011

MIAKA 50 YA UHURU OFISI YA TUJIFUNZE KUSINI INAANDAA TOLEO MAALUMU ,MAONI YA NAKARIBISHWA KUHUSU ELIMI YA WATU WAZIMA TANZANIA

 Maoni na mafaniio mbali mbali yanayo jitokeza ndani ya miaka 50 ya UHURU  yanazidi kutolewa,nawe unaweza kutoa kupitia Blog hii ama E - mail.christiansikapundwa@yahoo.com.nasi tutachapisha kwenye Toleo Maalimu  la mwezi Oktoba - Desemba ,karibu sana Motto wetu ( ELIMU HAINA MWISHO )
Ofisini kwa Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE Bw.Juma Nyumayo anapiga picha ambapo nakala za magazeti hayo zinapatikana.
 Huo ni mtambo wa kuchapishia Magazeti ya TUJIFUNZE KUSINI ambapo sasa linaandaliwa Toleo maalumu la miaka 50 ya UHURU..Fundi Bw.W.Kaimbe anawaelekeza wageni unavyo fanya kazi.
Hizo mezani ni nakala za matoleo ya magazeti ya Kanda 8 za elimu hapo awali zilizojumuisha na Zanzibar ambapo Mhariri wake alikuwa Bwana Salim Salim mwandishi mwandamizi maarufu sana Zanzibar sasa.

WATU 64,000 MOANI RUVUMA WAPO MAJUMBANI WENYE MAGONJWA YA AILI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Sasi ya RUVUMA MENTAL DISABILITIES ( RUMED ) Bwana Dadid Kakoyo akisoma Gazeti la TUJIFUNZE KUSINI kwenye ofisi ya Gazeti hilo kabla ajasaini kitabu cha wageni hapo jana alipotembelea kituo hicho.
Bwana Kakoyo anasaini kitabu cha wageni,TUJIFUNZE KUSINI inaanda Toleo Maalumu la miaka 50 ya UHURU,hivyo wageni wengi wanatembelea ili kujifunza ELIMU YA WATU WAZIMA MIAKA 50 ya UHURU imefanya nini katika Machapisho ya Magazeti ya Kisomo.
 Bw.Kikoyo akitoa maelezo namna ya kumsaidia mtu mwenye ugonjwa wa akili na kumweka katika mazingra ambayo yeye anajikuta yuko salama.kwa Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE KUSINI Bwana Juma Nyumayo aliyeshika kudevu akimsikiliza kwa makini mtaalamu huyo.
Hapo anamwambia Mhariri huyo kuwa magonjwa ya akili yanatokana na watu kujihusisha na madawa ya kulevya,kukata tamaa na kujiingiza kwenye ulevi wa kupindiia,na kukataliwa na familia zao,kwa kukosa amani,upendo na matumaini hivyo wanasononeka ( SONONA ).

KUTOKANA na tawimu za Mkoa wa Ruvuma zinaonyesha wagonjwa akili 64,000 wapo majumbani hawajatamuliwa bado,inaonyesha katika nyumba moja katika wilaya ya Namtumbo kuna mtu moja ama wawili wana matatizo ya aili.

Akizungumza kwenye ofisi za TUJIFUNZE KUSINI jana Mkuruganzi mtendaji wa  RUVUMA MENTAL DISABILITIES ( RUMED ) Bwana David Kakoyo,kuwa tafiti kadhaa zimeonyesha Mkoa una watu wengi wanaougua magonjwa ya akili lakini bado wako majumbani.

Bw.Kakoyo alisema kuwa hadi sasa ni wagonjwa 792 ndiyo waliyotambuliwa kimkoa,Mbamba – Bay,Mbinga , Namtumbo,Songea Vijijini, ambapo tafiti zimefanyika na kuwapata wagonjwa  kuwanzishiwa matibabu.
     Aidha alisema ubongo wa binadamu unahitaji msaada mkubwa sana wa ushauri nasaha,alisema katika kituo chao kitu cha kwanza wakimpata mgonjwa wa akili wanampiga na maji, na kumpa ushauri nasaha ili ajue kuwa yupo salama.
     Alisema watu wenye nia mbaya na watu wengine wanaweza kuutumia ubongo wa mtu mwingine kwa lengo baya,na kumfanya mtu yule akawa kama mtumwa wake akamtumia vile anavyo taka.
     Kuhusu kituo chake alisema kuwa anategemea kupata watoto 30 mwaka ujao ambao wana matatizo ya akili,alisema pamoja na asasi yake kujishughulisha na magonjwa ya akili lakini pia ametoa ushauri na saha kwa mabinti wawili yatima.
      Kufuatia ushauri huo mabinti hao sasa wanasoma elimu ya juu,ambapo mmoja amehifadhiwa anasoma mwaka wa pili Chuo Kikuu Mtwara tawi la SAUT,na wapili anasoma chuo kikuu cha ushirika Moshi.
      RUVUMA MENTAL DISABILITIES ( RUMED) wanapata msaada kutoka wa The Foundation for Civil Society .
      Bwana Kakoyo alianza utafiti kwa watu wenye magonjwa ya akili mwaka 2001 Wilayani Mbinga,mwaka 2006 alifanya utambulisho wa asasi yake na mwaka 2007 hadi 2009 ikafika hadi Wilayani kuanzia hapo Asasi hii ipo katika viwanja vya Sabasaba Matarawe mkoani Ruvuma  ndiyo makao makuu yalipo.





Monday, October 17, 2011

ELIMU YA WATU WAZIMA NI ELIMU YA KILA MMOJA WETU BWANA MPANGALA NA BI MWOMBEKI WAMESHUHUDIA HILO WALIPO JIFUNZA VITU WASIVYO VIJUA

 Afisa elimu vielelezo Bi. Rose Mwombeki wa Manispaa ya SONGEA akiwa ofisi za TUJIFUNZE ni ofisi yake pia kwa sababu afisa huyu yupo katika Kurugenzi ya Elimu ya Watu Wazima.
 Bwana Mpangala Afisaelimu kilimo wa Manispaa ya SONGEA alitembelea ofisi ya TUJIFUNZE kujifunza mambo mapya.
 Bw.Mpangala
 Bi. Mwombeki
 Maafisa hao wapo Paste Up Room wakipata maelezo ya Light table inayo tumika kuandaa kazi
 Wanapata maelezo namna mashine hizo za uchapaji zinzvyo fanya kazi.

MAAFISA ELIMU VIELELEZO NA KILIMO WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA WATEMBELEA OFISI YA TUJIFUNZE KUJIFUNZA

 Mhariri wa TUJIFUNZE Bwana Christian Sikapundwa  mwenye suti ya zambarao akiwaonyesha wageni maafisa Elimu Kilimo Bwana Honoratus Mpangala mwenye kaunda suti mikono mifupi na Afisa Vielelezo Bi- Rose Mwombeki,Mahazeti ya kisomo ya Kanda zote saba ambavyo vilikuwa vikichapa.
 Bi - Rose Mwombeki Afisaelimu Vielelezo Manispaa ya Songea
 Bwana Honoratus Mpangala Afisaelimu Kilimo wa Manispaa ya Songea walitembelea TUJIFUNZE leo
 Fundi mchapaji wa mashine Kubwa SORK Bwana Winifredy kaimbe akiwaonyesha wageni hao jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.
 Bi.Rose Mwombeki Afisaelimu Vielelezo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya TUJIFUNZE leo kabla ya kutembezwa kiwandani.
 Mhariri msaidizi wa TUJIFUNZE Bwana Juma Nyumayo wa kwanza  mwenye shati nyeupe akielezea maandalizi ya kuandaa Gazeti la TUJIFUNZE kwa ajili ya miaka 50 ya UHURU
 Wageni bado wanapata maelezo jinso Elimu ya Watu Wazima ilivyo kuwa ikichapisha Magazeti hayo ya Vijijini, mezani ni nakala za magazeti hayo ya Kanda za Elimu .
 Bwana Sikapundwa akiwaonyesha picha za Maafisa vielelezo wa Kanda ya Kusini
Wageni waipata maelezo ya mitambo ya  uchapaji iliyopelekwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa ajili ya kuchapisha Magazeti ya Wizara na kusambazwa kwa wananchi mjini na vijijini.

Saturday, October 15, 2011

ADHABU YA KUWAFUKUZA MADIWANI WAKE WATANO UNACHAMA WACCM WA UKOSEFU WA MAADILI WAFUTWA

 Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Bwana Emmanuel Mteming'ombe wakati wa mchakato wa kunadi wagombea wa Ubunge na Udiwani.
Mtahiki Meya wa Manispaa ya Songea Bwana Charles Mhagama wakati akijinadi wakati wa kuwania Udiwani katika Manispaa ya Songea  ambaye baadhi ya Madiwani wa CCM na Wapinzani waliwanya fujo wakati wakimchagua katika wadhifa huo aliokuwa nao sasa,ingawa bado baadhi hawautambui wadhifa wake.




KAMATI ya Siasa ya Halmashuri kuu ya Mkoa Mkoani Ruvuma  kupitia kikao chake kilichokaa hivi karibuni kimefuta adhabu ya kuwafukuza uanachama Madiwani watano wa Chama Hicho kutokana na kile kilichodaiwa ukosefu wa maadili wakati wa kumchagua Meya wa Manispaa hiyo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Bwana Emmanuel Mteming’ombe baada ya kupitia maelezo yaliyotolewa na Kamati ya siasa ya Wilaya ya kuwafukuza Madiwani hao,maelezo ya uteuzi wa Madiwani waliyofukuzwa uanachama na Kamati ya Siasa ya Wilaya,Kamati ya Mkoa imetengua uamuzi huo wa kuwafukuza madiwani hao uanachama. Na kuendelea na uanachama na udiwani wao kama mwanzo.

Aidha Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) Mkoa kimesikitishwa sana na vurugu na fujo zilizojitokeza katika Baraza la Madiwani wa kuchagua Meya wa Manispaa hiyo ,kufuatia vurugu hizo Chama Cha Mapinduzi Kimekemea na kulaani tabia hiyo ya kufanya vurugu katika vikao ambazo ni kinyume na kanuni za vikao na si tabia ya viongozi wanaotokana na CCM.

Bwana Mteming’ombe alisema kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa   kimeamua kutoa semina kwa Madiwani wote wanaotokana na chama hicho ili kuwaelimisha weledi juu ya kusimamia utekelezaji mzuri katika Halmashauri zao.

Pamoja na mambo mengine hali tete ya Baadhi ya Madiwani bila kujali Itikadi zao bado wanashikilia hali ya kutomtambua Meya wa Halmashauri hiyo Mstahiki Meya Charles Mhagama wa CCM Mbele ya Mkuu wa Moa huo alipokuwa akikagua shughuli za maendeleo katika Manispaa hiyo.

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AFUNGUA KIKAO CHA WADAU WA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI SONGEA



 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said  Mwambungu akiwa Ofisini kwake akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa huo,leo amezungumza na wadau wa Habari na Waandishi wa habari katika ukumbi wa CWT katika Manispaa ya Songea.
 Katibu Mkuu wa Ruvuma Press Club  aliyesika karatasi akiwa na mdau wa Habari Bibi Mwenda wa wanza mwenye suti ya mistari kabla ya kikao kuanza.
 Baadhi ya waandishi wa Habari wakisubiri kikao kuanza na kutuma habari kwenye vyombo vyao wanavyo viandikia.
 Bibi Joyce Joliga  mwandishi wa habari mwenye suti ya zambarao  nyepesi wakibadilishana mawazo na Bibi mdau wa habari na mjumbe wa kamati  ya Maadili Katika Club ya Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa huo.


MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said Mwambungu afungua kikao cha siku moja cha wadau wa Habari na waandishi wa Habari leo katika ukumbi wa CWT katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Bw. Mwambungu amewataka wadau wa habari utoa habari kwa waandishi wa habari kwani bila ushirikiano wao na waandishi wa habari wananchi watakosa habari ambazo ni haki yao kuzielewa.

Aidha na waandishi wa habari nao wanawajibika kufuata maadili ya kazi yao ya kuandika habari bila kuegemea upande mmoja,ambazo haziwezi kuumiza mtu au kumnufaisha mtu kwa matakwa yake.

Kikao hicho kimejumuisha waandishi wa mkoa wote wa Ruvuma na wadau kadhaa kutoka katika Manispaa ya Songea.